Nimeamua kuwa Atheist

Nimeamua kuwa Atheist

Sijui vipi niweke nieleweke.

Ila nahisi Kuna Atheist wa mkumbo kama mimi nilivyohitaji kuwa.

Na Kuna real atheist,sasa pengine hawa real one wako real pia ila hawa wa mkumbo Kuna muda kwenye real life uhisi Kuna vitu haviko sawa wanajikaza tu.

Unamkataa Mungu jamiiforum haafu in real life sio kweli
na kimsingi kwenye mkumbo hakuishii hapo, hata ndani ya imani
 
hii conclusion nilifikia baada ya oct 29 naamini Mungu yupo kwa definition ipo nguvu inayonizidi ilionipa uhai ila story za Mungu ni wa haki sijui ana upendo hazipo hayo ni mambo yaliletwa ili kututawala tu
unatafsiri vipi hali ya hapo middle east mkuu?
 
Wewe ndio mfano halisi nilichokisema humu kuwa kuna kutilia mashaka uwepo wa Mungu na kutilia mashaka yale yenye kuhusishwa na Mungu, sasa unakuta mtu anaenda kuwa atheist na kupinga uwepo wa Mungu kiujumla kisa tu hakubaliani au ana mashaka na madai ya huo upendo wa Mungu.

sasa mkuu wamemjua kupitia vitabu, sasa wamepata mashaka kutoka kwenye maelezo ya vitabu , hapo sasa si ni jambo la automatic tu? au
 
sasa mkuu wamemjua kupitia vitabu, sasa wamepata mashaka kutoka kwenye maelezo ya vitabu , hapo sasa si ni jambo la automatic tu? au
Umepata mashaka kwenye msingi mzima wa kuwepo Mungu au baadhi ya yale yenye kuelezwa kuhusu huyo Mungu? Kwa sababu mkuu ukitafakari zaidi utaona kuwa madai ya uwepo wa Mungu yapo kabla hata ya vitabu na ndio maana kuna ambao hawajawahi hata kuamini hivyo vitabu katika maisha yao ila wanaamini Mungu.
 
Kwa sababu mkuu ukitafakari zaidi utaona kuwa madai ya uwepo wa Mungu yapo kabla hata ya vitabu na ndio maana kuna ambao hawajawahi hata kuamini hivyo vitabu katika maisha yao ila wanaamini Mungu.
hili halina ubishi mkuu.

sasa wenye mashaka hoja yao kama umeielewa kwanza inafocus sana kwenye abrahamic dinis, kama vitabu ni vitakatifu na wao wamepata mashaka kwenye hivyo vitabu hapo sasa si automatic utata wa Mungu wa kwenye hivyo vitabu?
 
Ndio maana nauliza mashaka hayo kwenye msingi wa madai ya kuwepo Mungu au ni mashaka kwenye mambo yenye kuhusishwa na Mungu? Kwa sababu hata wa dini moja huwa wanatofautiana baadhi ya mambo kuhusu Mungu ila wote wanaamini huyo Mungu.
 
Sijui vipi niweke nieleweke.

Ila nahisi Kuna Atheist wa mkumbo kama mimi nilivyohitaji kuwa.

Na Kuna real atheist,sasa pengine hawa real one wako real pia ila hawa wa mkumbo Kuna muda kwenye real life uhisi Kuna vitu haviko sawa wanajikaza tu.

Unamkataa Mungu jamiiforum haafu in real life sio kweli
Nje ya jamiiforums naenda kanisani mkuu. Huwezi kuishi kwenye conservative society kama Tanzania bila kuvaa koti la dini.

Hata hivyo tunahoji uwepo wa Mungu tu, mafundisho mengine ya dini ni mazuri na yanafaa.

Pia imani ni suala binafsi sana. Wapo wengi wanaokiri hizi imani ila wana matendo maovu. Usichoke kutafuta majibu kutoka vyanzo mbalimbali.

Mwisho wa siku kile kilichopo ndani kabisa ya moyo wako ni wewe tu ndo unajua.
 
Kwanza kabisa, kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.

Narudia tena, kisichopo, hakithibitishiki kuwa hakipo.

Kwa sanabu hakipo, na kama hakipo, hakithibitishiki kuwa hakipo, uthibitisho unaendana na kilichopo.

Tunaweza kujenga hoja kama za proof by contradiction kuonesha contradiction zinazoonesha kitu fulani hakiwezi kuwapo. Katika hii dhana ya Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) hayupo, nimeelezea sana Epicurean Paradox mpaka michoro nimeiweka hapa. Google Epicurean Paradox, soma, ielewe, kama una swali kuhusiana an Epicurean Paradox lilete hapa.

Zaidi.

Mzigo wa uthibitisho unamuangukia yule anayesema kitu kipo.

Ndiyo maana Polisi wakija nyumbani kwako, wakisema una madawa ya kulevya, wao wanaosema una madawa ya kulevya wanatakiwa wafanye msako mpaka wayapate, wathibitishe yapo.

Hawakwambii wewe unayesema huna madawa ya kulevya uthibitishe huna madawa ya kulevya.

In principle, we cannot prove a negative, but we can show contradictions that shows the impossibility of a negative.

Swali la kuuliza hapa, ni kuwauliza wanaosema Mungu yupo, wathibitishe Mungu yupo.

Unasema Mungu yupo?

Kama unasema hivyo, thibitisha Mungu yupo.
Bro 🙌you have nailed it haiitaji maelezo mengi.
 
Ndio maana nauliza mashaka hayo kwenye msingi wa madai ya kuwepo Mungu au ni mashaka kwenye mambo yenye kuhusishwa na Mungu? Kwa sababu hata wa dini moja huwa wanatofautiana baadhi ya mambo kuhusu Mungu ila wote wanaamini huyo Mungu.
nafafanua kwa mara ya mwisho mkuu.

wao wanakataa au atleast kutilia shaka habari hizo kwa sababu wameona mapungufu/matatizo kutoka kwenye vitabu ambavyo vinasemekana vimetoka Kwake, na hawapati majibu ya kueleweka, hivyo habari za uwepo wake ni lazima ziwe na shaka --- hii haijalishi yupo au hayupo

natumai umeelewa mkuu
 
Basi mkuu naona nimeshindwa kueleweka japo mie nakuelewa vizuri tu.
 
UHURU JR nimekusoma mkuu, wewe umekiri kwamba ni "imani"
Ndio ni imani na ndio lengo kuu, ndio maana wenye kukubali kuamini na kufuata maamrisho inasemekana kuna malipo wanapata. Shida atheists wanakwambia wao hawataki chochote kinachoitwa imani kwa kuona imani ni jambo lisilo na ukweli.
 
Sasa hapo shida ipo wapi? Ukweli wa hizo imani ni upi?
 
Ndio ni imani na ndio lengo kuu, ndio maana wenye kukubali kuamini na kufuata maamrisho inasemekana kuna malipo wanapata. Shida atheists wanakwambia wao hawataki chochote kinachoitwa imani kwa kuona imani ni jambo lisilo na ukweli.
sasa mkuu haya mambo ni two way traffic --- we hujawahi ona au sikia wenye imani wanawatambia wasio na imani kwamba watachomwa?

kwa maoni yangu hapo ndo walipoanza kuvutana mashati, hali kadhalika kama wenye imani wanavyoeneza imani , wasio na imani na wao wana-counter

so kimsingi wenye imani wanasema hizo habari zio za kweli, kwa sababu kimsingi hazionekani
 
Mungu alipomuumba binadamu alimuonya juu ya mti wa maarifa ya ujuzi wa mema na mabaya

Mungu hataki ujue lolote baya

Kila kitu kwake ni kizuri, ni wewe tu na ujinga wako

Ndiyo maana Biblia inasema kuishi ni Kristo na kufa ni faida

Sasa nithibitishe Mungu yupo? Ni rahisi tu alisema na tufanye mtu kwa mfano wetu, mimi ni mfano wake

Mungu hafanyi lolote peke yake bila uwepo wako, alimwambia Mussa nyanyua fimbo elekeza upande wa bahari na bahari ikaachana na kutenga njia wana wa Israel wakapita, hakumuuliza Mussa je mmeshafika baharini nitoe maji mpite? Bali alimtumia Musa na fimbo

Ukiona humuoni Mungu kwenye maisha yako ujue umekaa na kusubiri kufanyiwa kila kitu na Mungu kwa maombi tu bila hata matendo

Mungu yupo na anafanya kazi ila siyo kwa njia na mbinu unazotaka wewe
 
Nenda kasome quantum physics, kasome relativity theory, general relativity theory, kasome all physics laws about the universe, kasome mambo yote ya Einstein and newton ukishaelewa vizuri basi kaa chini relax kunywa maji. KISHA TAFAKARI KUWA KILA KITU ULICHOKISOMA NI CHA KWELI, NA NI KWELI SAYANSI IPO SAHIHI. Lakini kosa ni moja unampima mungu kwa kutumia quantum physics ndio maana utaconclude mungu hayupo
 
Back
Top Bottom