Kila mtu aamini anachokiamini,anayeamini Mungu yupo aishi kwa kumuamini Mungu na asiyeamini uwepo wa Mungu nae aishi maisha aliyo yachagua,
Hua sioni mantiki yeyote ile ya watu kubishana kuhusu uwepo wa Mungu au kutokuwepo, coz haya mabishano hayatokuja kua na mwisho wala kupata mshindi au mshindwa,
Kuna watu humu JF miaka na miaka wapo kwenye haya mabishano ya uwepo wa Mungu au kutokuwepo kwa Mungu,
Kwanini utumie nguvu na muda wako kubishana au kujadili hii issue? Wewe amini unachokiamini kisha piga kimya,
Hakuna haja ya kupangiana namna ya kuishi hasa kwenye mambo ya kiimani,
Sijaona hata mantiki ya mleta mada kuutangazia umma kuhusu uamuzi wake,
Kila mtu afuate anachokiona ni sawa kwake,tukutane mwisho wa safari kwa wenye kuamini.