Nimeamua kuwa Atheist

Kitu gani kimekusukuma hadi umefikia uamuzi wa kutokuua viumbe wengine?

Hivi unaweza kunipa tofauti ya maneno haya matatu?

1. Nature
2. Universe
3. God

Ni wapi Mungu alisema hapa duniani Hakutakuwa na Dhulma, uonevu au usaliti?

Yesu tu yeye mwenyewe alisalitiwa sembuse na wewe loose nut wa buza
 
watu kwa nyakati hii wapo kwenye mkanganyiko kuna dini nyingi , wanajuaje wameamini upande sahihi?
Lax swali lako ni dogo kwa maneno lakini lina maana pana na sahihi kwa watu wenye kutafuta ukweli na usahihi wa imani katika zama zetu. Linatakiwa lijibiwe kwa kirefu lakini inaniwia vigumu kueleza fikra za imani kwa maandishi. Lakini kama utakuwa unautafuta ukweli wa imani katika dini hizi tulizonazo soma vitabu vya hiyo imani halafu ulinganishe. Ukisubiri kuhubiriwa tu unaweza usipate ujumbe kamili.
 
sawa mkuu,

watu wameshika vitabu wamesoma na wameangukia pande tofauti na wote walikua na nia moja ya kuutafuta ukweli --- unalizungumziaje suala hilo
 
Sasa mkuu,kwa hiyo unajaribu kuniambia Kuna umuhimu mkubwa sana wa imani ya kidini katika jamii zetu?
 
Karen Armstrong.
Yeye alikuwa mtawa (nun) wa Kanisa Katoliki zamani, kisha akaacha utawa na kuwa mwandishi na mwanafalsafa wa dini.
Karen Armstrong ni mwandishi na mchambuzi wa dini kutoka Uingereza

Aliwahi kuwa mtawa wa Kanisa Katoliki (nun) akiwa kijana lakini baadaye akaacha utawa kutokana na changamoto za maisha ya kidini na kiimani

Baadaye akajikita kuandika vitabu kuhusu historia ya dini, falsafa ya imani na uelewa wa Mungu, akisisitiza mazungumzo kati ya waumini na wasioamini


Hizi ni aina za atheist according na uyu jamaa

Scientific / Rational atheist – Anakataa Mungu kwa sababu ya sayansi au mantiki


Experiential atheist – Kutokuamini kunatokana na uzoefu mbaya wa dini


Conceptual atheist – Hupinga taswira fulani ya Mungu, sio lazima kiroho chote


Moral protest atheist – Anakataa Mungu kutokana na uwepo wa uovu duniani


Apathetic atheist (Apatheism) – Hajali sana swali la Mungu

Najaribu kuvumbua na kuchimba kwamba wewe ni aina gani ya atheist

(Unajua nashangaa Nini hii ni maajabu)
 
Upo sahihi kwa maamuzi yako, mimi habari za kuamini mambo ambayo hayana majibu ya kueleweka nilishaachana nayo kitambo.

Umechelewa tu kujitambua.
 
Madai ya kutaka uthibitisho wa kuwepo Mungu ni atheists ndio huleta madai hayo, wao ndio hufanya hitimisho kwa kusema hakuna Mungu kwa sababu hakuna uthibitisho.
Anything asserted without evidence can be dismissed without evidence.

Madai ya kwamba Mungu yupo, yalianzia kwenu nyie Theists, waamini Mungu.

Ninyi ndio mlianza kusema kuna Mungu. Hivyo ninyi ndio mnapaswa kutoa uthibitisho wa huyo Mungu. Ili mthibitishe madai yenu ya kuwepo huyo Mungu.

Ukishindwa kuthibitisha Mungu yupo, ina maana madai yako ni ya UONGO. Na huyo Mungu unayedai yupo, Hayupo.

Huyo Mungu anakuwa dismissed automatically.

Falsafa ya uthibitisho inamtaka anayeanza kudai kitu kipo, ndio atoe uthibitisho wake.

Ukishindwa kuthibitisha madai yako, ina maana kwamba madai yako ni ya uongo. Na hicho unachodai kipo, hakipo.
 
Mungu anataka kuaminiwa kwa imani tu, hajataka athibitishwe kwa logic na akanushwe kwa falacy, kwani ufahamu wetu upo kinyume na uhalisia wake. Sisi ufahamu wetu unataka uwe kwenye mipaka ya wakati na mahali, wakati Mungu yupo kinyume na hicho.
Huyo Mungu yupo so insecure hadi anahitaji kuaminiwa?

Huyo Mungu akiaminiwa yupo, anafaidika nini?

Huyo Mungu asipoaminiwa, anapungukiwa nini?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
 
Huyo
Huyo Mungu akiaminiwa yupo anafaidika nini?

Kwa nini huyo Mungu anajificha kama mwali, halafu anataka kuaminiwa akiwa mafichoni?

Anacho ogopa kujulikana hadharani ni nini?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
 
Sasa hapo shida ipo wapi? Ukweli wa hizo imani ni upi?
Atheists hawataki chochote kinaitwa imani, na tambua imani sio dini na Mungu tu.

Huwezi kutafuta ukweli wa imani kwa kutaka uthibitisho nje ya imani, kwa sababu ukipata huo uthibitisho hiyo haitokuwa tena imani.
 
Sasa wanachosahau ni kwamba imani sio kwa masuala ya dini na Mungu tu, sasa mtu anaposema hataki imani kabisa hunishangaza.
 
Atheists hawataki chochote kinaitwa imani, na tambua imani sio dini na Mungu tu.

Huwezi kutafuta ukweli wa imani kwa kutaka uthibitisho nje ya imani, kwa sababu ukipata huo uthibitisho hiyo haitokuwa tena imani.
Sio kweli atheists hawataki chochote kinachoitwa imani .

Sasa wewe ndio umesema hauwezi tafuta ukweli kwenye imani na upo sawa kabisa , ila wanaoamini wanadai wanaweza , ndio maana tunataka kufahamu kivipi?
 
Hatuwezi kuelewana mkuu na si mara moja kuzungumzia issue ya uthibitisho, shida ni kwamba wewe unachukulia kuwa uthibitisho ndio hufanya kitu kuwepo yani kwamba mimi leo nikiuwa halafu mahakamani ukakosekana uthibitisho basi inafanya kuwa mie sijauwa na si kwamba umekosekana tu uthibitisho wa kunitia hatiayani.

Jielimishe mkuu kuhusu uthibitisho.
 
Sio kweli atheists hawataki chochote kinachoitwa imani .

Sasa wewe ndio umesema hauwezi tafuta ukweli kwenye imani na upo sawa kabisa , ila wanaoamini wanadai wanaweza , ndio maana tunataka kufahamu kivipi?
Kwani mara ngapi mnasema hamtaki imani mnataka kujua?

Sasa kama nipo sawa kwanini bado mnataka uthibitisho wa imani? Hao wanasema wanaweza kwa sababu nyie mnasema hakuna Mungu kwa sababu hakuna uthibitisho, mnatumie kutokuwepo huo uthibitisho wa imani kuhitimisha madai yenu kuwa ndio hakuna Mungu.

Atheists humu hawana hoja nyengine kujadili kuhusu Mungu zaidi ya kudai uthibitisho.
 
sawa mkuu,

watu wameshika vitabu wamesoma na wameangukia pande tofauti na wote walikua na nia moja ya kuutafuta ukweli --- unalizungumziaje suala hilo
Inategemea wameshika vitabu gani?
Jaribu kusoma vitabu vya dini tofauti siyo dini moja tu, ili upate kujua nini kusudio la dini hizo.
 
Huyo Mungu yupo so insecure hadi anahitaji kuaminiwa?

Huyo Mungu akiaminiwa yupo, anafaidika nini?

Huyo Mungu asipoaminiwa, anapungukiwa nini?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
Yeye hana hitaji lolote kutoka kwa viumbe, bali sisi viumbe ndiyo wenye kumuhitajia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…