MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,221
22,295
Nimefikiria kwa makini sana nimeona ni jambo sahihi kuoa binti wa kisabato, sababu ni zifuatazo;

1. Nitaokoa zaidi ya milioni 2 kwa mwaka kutoka kwenye hela za kuhudumia nywele. Milioni 2 ni kama matofali 2000.

2. Kwenye msosi nitaokoa hela nyingi sana kwa mwaka zaidi ya milioni 3 kwasababu mama wenye nyumba hatataka kula kitimoto, rost nyama, mayai, biriani, pilau, cocacola, majani ya chai, maini, na vitu vingine vitamu yaani rojorojo.

Badala yake mboga za majani, juice ya mwarobaini, maharage, na matunda vitashika hatamu. NB: Kitimoto nitakula kwa siri bila mke kujua.

3. Nitakuwa na utulivu wa nafsi kwasababu wife sharti lake kuu ni kumwacha awe huru na sabato yake.

Isitoshe wachungaji wa kisabato sio kama kina Mwamposa ambao huwafanya mateka wa kiimani wake za watu.

4. Nina uhakika wa watoto wangu kuwa katika maadili mazuri kwasababu kanisa lina mambo mengi kwenye makuzi ya watoto. Kitu kama PF naunga mkono sana.

Ila watoto wakiwa wakubwa nitapiga marufuku kuhudhuria camps za vijana kwasababu ya kashfa ya ngono iliyopo.

5. Nitaimarika sana kiafya kwasababu SDA wako vizuri sana kwenye miongozo kuhusu afya kwa waumini wao. Ikumbukwe vitu vyote wasabato wanavyosema tusitumie vina madhara ambayo yamethibitishwa kisayansi sema ni ubishi wetu.

Kwa mfano kitimoto ni kitu hatari.

Kiukweli nataka nioe binti wakisabato ila kabla ya kuoa lazima nikague vyeti vyake. Kigezo cha ufaulu ni muhimu sana.

Lazima mke wangu kwa O-Level awe na C ya hesabu au zaidi, English kuanzia D.
 
๐™ฝ๐š’๐š”๐šž๐š๐šŠ๐š”๐š’๐šŽ ๐š”๐š’๐š•๐šŠ ๐š•๐šŠ ๐š”๐š‘๐šŽ๐š›๐š’.
 
Watoto wa kisabato kiukweli wametulia saaaaana pamoja na mapungufu ya kibinadamu,mi nimeoa msabato aiseeh burudani mno havina hasira za kijinga ni waaminifu Sana ila tatizo lao Ni sabato yao tu daaah fanya yote ila sabato yao usiibughudhi, kiukweli need nimeridhika hata jamaa yng nilimshauri leo hajutiiii
 
Back
Top Bottom