- Thread starter
- #61
Asante kwa ushauri!Ni hivi
Tanesco wana wateja wa aina mbili
1. Wateja wadogo
2. Wateja wakubwa.
Sikumbuki wateja wadogo likit yao ni kiasi gani ila ni kidogo sana
Wewe hapo sio kwamba unaibiwa ila kwa sababu mnatumia meter moja tanesco wanahesabu mteja mmoja na kwa kuwa mnatumia unit nyingi basi mnakuwa kwenye category ya wateja wakubwa.
Utofauti wa wateja wadogo na wakubwa ni price/unit.
Kuna nyumba nilipanga hapa bukoba, wapangaji tulikua watatu, nilikua nalipa sometimes hadi 40,000.
Baada ya kuhama, nikahamia nyumba ambayo ni stand alone, nikawa natumia 30,000 kwa miezi 3.
Ushauri, unapo tafuta nyumba ya kupanga hakikikisha hakuna swala la kushare meter, afadhali hiyo pesa upngeze kwenye pango la nyumba upate nyumba nzuri zaidi.