Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Hajasema anawezza kuwa kitu, amesema anaweza kuwa chochote. Labda mimi ndio sijaeleza vizuri. Yaani yeye anasema anaweza kuwa chochote ukitakacho wewe, sababu kuu, haonekani, mimi sijamuona mpaka leo. Kwa hio hapo ni fikra zako tu, ukifikiria mti unaongea na wewe, kwake sawa, ukifikiria jini anaonea na wewe kwake sawa, ukifikiria mtu anaongea na wewe kwake sawa.

Lakini mbona niliandika mwenyewe anasema yeye ni mtu. Au nimbishie hilo?

Hilo la kila kitu "lina uhalisi": wake sijakuelewa. Huo uhalisi unaupata kwa kuuona, kuusikia, kuusoma au vipi? Uhalisi wako wewe ni upi> Mimi siujui.
Simba.
 
Hilo mbona limejibiwa siku mbili tatu nyuma, au kuna lingine sijaliona. Nifahamishe lipo post namba ngapi au uliza tena.
Simba.
page no 78 nimeuliza maswali mawili ila hujajishughulisha kabisa, nitakumbushia mpaka ujibu maana yamekua maswali yangu 3 sasa ambayo unayapita tu.
Lingine niliuliza juu ya makanisa fake na manabii fake utupe list ila kimya.
 
huyo kaka yako nishjua namuonaga youtube
 
Uzi wako Simba toka day 1 mpaka leo umesema mengi na kiumbe wako.
ENatamani utuelezee amekufanikisha vipi kwenye maswala ya Uchumi mpaka sasa upoje na unamiliki nini?
ndio kwanza nayaona maswali yakobaada ya kunistua. Ngoja nijibu moja moja.

AlhamduliLlah, sijawahi kufikiria kuhusu uchumi binafsi toka zizaliwe, nimekikuta kila kitu kipo kwetu.

Binafsi kwa sasa nina familia ya wake wawili na watoto sita. Kila mmoja anakaa nyumbani kwake.

Nina fanya biashara ya kutengeneza magari, kwa sasa mimi naelekeza tu vijana. Nina duka la spea za magari za vifaa vya umeme tu wa magari (electrical system) vipya na used. Vyote ka gari ndogo na kubwa za aina zote.

kama sina spea, nakuagizia faster kutoka nje ya Tanzania. Uzoefu wa miaka mingi, kuanzia ma control bocx mpaka clips za umeme wa magari. Duka langu limezoeleka sana na wanunuzi wangu wakubwa ni mafundi umeme wa magari, hapo tabata.

Similiki gari, sijawahi kumiliki lakini ni zangu, kwa maana natumia za mama, baba na wake zangu. Sijaona umuhimu wa kumiliki gari langu binafsi.

Sina mali, sina akiba benki, sijawahi kuhitaji. Mali za shamba la babu yangu, zinazomuhusu babangu mimi nnazishughulikia lakini ni zake hazihiusu, isipokua mwenyewe ananipa sadaka yake apendavyo kwa kumfanyia kazi zake.

Huwezi kuamini, sijawahi kununua chakula nyumba zangu zote mbili. Chakula mpaka leo kinatoka kwa wazazi wangu na uzee wangu. Nikinunua kitu labda ni zawadi nikisafiri. Nashukuru Mungu nimepata wazazi wema kabisa. Mwenyezi Mungu awaweke. Mimi na babangu mzazi ukituona utafikiri ni mtu na mdogo wake, mama yangu ndio kabisa, hata enzi za babu nje nje, yeye ndio nilikua naenda nae kama partner wangu. Sasa basi tena mambo hayo. Nimetubu.

Natumai nimekujibu kuhusu uchumi. Kama kuna lingine, uliza tu.
Simba.
 
Safi, basi weka kipind au uanzishe uzi mwingine ili usiingiliane na huu uwe unaelezea Dawa na inatibu nini, ili walau huyo kiumbe wa fimbo watu wa jF wafaidike nae,
unaeza elezea ugonjwa huu na huu Dawa yake ni hii hii, au ukichukua hiki na hiki ukafanya hivi kinatibu hivi hapo kwa week mpaka mwezi utakua umefanya kazi kubwa sana na ndipo tutaona ufanisi na hakika wa habari zako
 
Yani elimu ya Ukristo niichukue kwa muabudu majini!? Hauwezi kuwa serious.
mimi sifugi majini ila naweza kukupa elimu vipi nikupe elimu au unaendelea na majivuno.?
Kwani hujapata kusoma katika wafilipi 2:3 Inasema " Msitende neno lolote kwa majivuno , Bali kwa unyenyekevu, Kila mtu na amuhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake.
 
Tatito lako huelezei mtu akaelewa ni unaelezea unaacha mtu na maswali zaidi hakuna asie jua Umm ni Mama Mwanamke Abu Baba mwanaume ila Umm Subian na Abu Subian au kwa majina mengine Inkubi na Sakubi Arsis hakuelezea mtu akaelewa kaongea kifupi tu Subian ni Sabayin yaani hajaelezea kuhusu majini Subian kwa kina kwa upana.
 
Haijuwi hiyo mistari huyo mjivuni.

Anajuwa mapambio na nyimbo za kwaya tu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…