Arsis nimeguswa na swala au changamoto ya madam
Farijala wa Farijala kuhusu mumewe,hakika huyo mwanaume mwenzetu anaumia sana lkn na dada yetu anaumia pia,kwasababu si nature ya mwanamke kulea familia,yaan analea lkn ni mzigo mzito kwake sana
Sasa kuna ushauri ulimpa wa ibada na kuacha maasi kitu ambacho ni sahihi kabisa,lkn inajulikana Mwenyezi Mungu ndio suluhisho la kila kitu sisi wengine ni sababu tu,kwahiyo kama kuna sababu ya kumpa kama ni dawa au namna nyingine yoyote basi msaidie ila mponyaji ni Allah
Kwangu mimi nashauri huyo mumeo wakati wa kuoga aweke chumvi ya mawe katika maji yake na iwe sehemu ya zoezi lake la kila siku,hiyo ni dawa ya asili ya kuondoa uchafu mwilini ya kichawi na kishirikina
Ila asiweke imani juu ya hiyo chumvi kwamba itamsaidia ila anapoweka chumvi katika maji anuie mfano wa hivi EWE MWENYEZI MUNGU HAKIKA WEWE NDIO ULIYO UMBA HII CHUMVI NA KUIPA NGUVU YA KUONDOA UCHAFU NA.MIKOSI NA MABALAA,NAOMBA KUPITIA HII CHUMVI IWE NI SABABU KUNITAKASA NA MABALAA YOTE YA KICHAWI,NUKSI NA UBAYA WOWOTE ULIO KATIKA MWILI WANGU
Kwa nia hii utakuwa umemtegemea Mwenyezi Mungu na si chumvi kama chumvi
Nakumbuka kipindi fulani pamoja na kufanya ibada nilitumia chumvi kuogea mara kadhaa,kuna matokeo yalionekana ikiwemo kuota usiku kitu kama majini yametoka nyuma ya mgongo wangu na.kusema huku yanapaa kutoka ndani kwenda nje ya nyumba "wewe si unajifanya mjanja sawa " baada ya kuamka niliwaza sana juu ya ile ndoto
Kwa kifupi habar za chumvi kuwa sehemu moja wapo ya tiba ya asili inakubalika sana na si uchawi,ila nasisitiza usiegemeze kuwa chumvi ndio suluhisho la shida zako ila Mungu kwanza na chumvi ni kama sababu tu
Kama vile tunavyokunywa dawa za hospitalini,anayetuponya ni Allah na dawa ni sababu tu