Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Kwa Kiarabu ni; Bidaa
Kwa Kingereza ni; heresy.

Umeridhika au bado?

Sasa na wewe rudia post zangu unapokuta alama ya kuuliza jibu ukweli wako. NBona unakwepa maswali yangu? Yamelenga kutoa elimu.
Simba.
Sijakuambia unitafsirie uzushi kwa kingereza ni nini au kiarabu nataka maana yake.
Narudia uzushi ni nini?
 
Vitu vingi sana kwenye dini uzushi, hilo nalijua, nimeanza kuchambua uzushi wa Adam kua ni mtu wa kwanza, kabla sijamaliza, umeleta "tawheed" halafu unasingizia mambo chungu nzima, maana yake ulioitoa ni potofu kama somo lenyewe.

Inaweza kua wewe unajifunza kwa nia njema kabisa, lakini sababu ni ipi? Kupoteza muda? Wakati Qur'an ipo wazi kabisa, inasema Sema, Allahu ni "Ahad" katika Surat Ikhlas. Sasa hio tawheed inahusu nini zaidi ya kupotosha watu tu?

Mtume Muhammad alisomesha somo linaloitwa "Tawheed"?
Simba.
Basi ndio maana nilikuuliza shida yako ni neno TAWHEED au yanayofundishwa ndani ya TAWHEED?
Japo unakwepa kunijibu ila maelezo yako yanaonyesha shida yako ni neno TAWHEED.
Maana TAWHEED inafundisha juu ya Mungu mmoja ambaye ni ALLAH na wanarejea quran na mtume kafundisha Mungu ni ALLAH sasa shida ni nini hapo?
 
Vitu vingi sana kwenye dini uzushi, hilo nalijua, nimeanza kuchambua uzushi wa Adam kua ni mtu wa kwanza, kabla sijamaliza, umeleta "tawheed" halafu unasingizia mambo chungu nzima, maana yake ulioitoa ni potofu kama somo lenyewe.

Inaweza kua wewe unajifunza kwa nia njema kabisa, lakini sababu ni ipi? Kupoteza muda? Wakati Qur'an ipo wazi kabisa, inasema Sema, Allahu ni "Ahad" katika Surat Ikhlas. Sasa hio tawheed inahusu nini zaidi ya kupotosha watu tu?

Mtume Muhammad alisomesha somo linaloitwa "Tawheed"?
Simba.
Alafu unaposema Quran inasema mwenyezi Mungu ni mmoja si ndio Kwenye somo la TAWHEED wanafundisha ALLAH ni mmoja na rejea yao ni quran mbona kama unapinga kitu usicho na elimu nacho?
Ukisema TAWHEED ni uzushi na TAWHEED inafundisha juu Mungu mmoja kwahiyo kusema Mungu ni mmoja ni uzushi si ndio?
 
Nikaingia chumbani kwangu nikakoga koga nikavaa kashual tu ile sijatoka Simu ikaita, kupokea Jini 1. Tukasalimiana pale.
Jini1; Simba leo umekua mtu mkubwa sana Unguja.
Mimi; Kivipi tena?
Jini 1; Utaogopewa Unguja nzima, wewe utanambia. Ngoja kesho kutwa, utanambia.
Mimi; Kwanini?
Jini 1; Wewe huoni jinsi mkubwa wa vibuki vya Ndama Mulaki alivyokunyenyekwea?
Mimi; Akiona kuna simba, nilikua nataka kumuuliza Arsis hilo.
Jini1; Wala haina haja ya kumuuliza Arsis, yeye anasikia maonhgezi yetu. Kwanza mimi sikukupigia kwa hilo. Lakini kwa kua tumeshalianza nakuja kwako, nije?
mimi; Njoo.

Hata sekunde haijachukua mlango ukagongwa, kufungua Jini 1 kafungua ananukia udi halafu kapendeza huyo kavaa na abaya.
Mimi; kwema?
Jini 1; Kwema, mambi ya Unguja haya, ukiwa Unguja lazima uwe Muunguja, kwani nimechukiza?
Mimi; umependeza lakini wewe sura yako hutaki niione mika yote, kwanini?
Jini1; Wewe nae huchoki kuniuliza hilo, achana na hilo, mie ukiniona utakua hunikaribushi kwako au utakua hutaki nindoke.
Mimi: haya nambie kilichokuleta.
Jini 1: Kwanza ngoja tumalize swala la leo kwa Bi S. Bi S, kulikua hakuna simba wala jinni la Simba. Bi S. kawekewa picha tu kwa teknolijia ya kisasa, ile niliwahi kukwambia sijui Arsis anitaje na kizungu chenu. Hio hata wewe Simba huipati hio, sisemi mengi.


Sasa ile picha ya Simba aliwekewa na wewe ulipokua unaongea alipopandisha yeye, na jini lake likaogopa sana, wanamjua Simba, tena huyo aliewekwa picha kwako ndio baba lao. Ndama akaogopa akawa na anamwalaumu sana Bi S, kafikia mpaka kumwambia siku nyingine ukimakribiusha mtu mkubwa namna hii lazima tujue iki tumkaribishe kwa hadhi yake. Usirudie tena, lazima apewe heshima zote Simba. Huyo ni mkubwa sana kwetu sote sisi. Kwanza kakaufanyia heshima kubwa sana kuja, huyo haji bure bure tu. Kwa hio jichunge sana na kauli zako na mambo yako kwake. Muhheshimu huo kuliko mimi.

Jini 1: hayo ndio aliambiwa Bi S. Sasa mimi hayakunileta hayo, yamenileta nikupe umbea. Wageni walikuja leo hapa Hoteli, wameshafika huko. Wanajuana na Dokta, si unajua Wangazija wote wanajuana, wao walikua hawajui kama kaja hapa, Bi S ndio aliwaambia wana shughuli ya mtu wa hukohuko kwao Dar, wakauliza nani alipowaelekeza, wakamwambia gtunamjua sana, mtoto wa fulani yule. Akawajulisha kua mwenzao ndio shughuli yake ya kwanza. Waksema hii sio ya kuikosa, huyo tuwe nae, maana hapa Dar hapatikani sana, lakini tukijuana nae huko huku sasa itkua wepesi kuwa nae karibu.

Jini 1; hayo ndio yalioongelewa, mengine umbea wa kike tu sina haja ya kukwambia.
Mimi; Sasa inanihusu nini?
Jini1: Na wewe si umbea tu, unakua unajua kinachoendelea.
Mimi; haya Ahsante kwaheri.
Jini 1; Unaona upuuzi nilichokwambia, utakuja kukifurahia siku moja. kwaheri, akafungua mlango akaondoka zake.

Sijakaa sana, simu ya hoiteli ikaita, nikaipokea.

Meneja: Njoo bwana, umeshakula?
Mimi; bado ndio nilikua nafikiri maana leo nilialikwa biriani la nguvu njimini huko.
Meneja; basi vizuri kama haujala, niliwaalika hawa kina mama waliokuja chakula cha usiku, nikaona na wewe uje mpate kujuana. Watyu wa Dar hawa, labda mnajuana. Njoo bwana ni watu muhimu sana kujuana nao, utawapenda, wachesi sana.
Mimi; basi nakuja.
Meneja; kama nusuu saa watakua washakuja, unaweza kuja mapema tukapiga stroty, watatukuta.
Mimi; Poa.

Nikaona wacha nipige simu kwa wanangu Dar maana inaweza kua usiku nikakosa kuongea nao, nikawapigia nikaongea na wofe nikaongea na wanangu. Nikampigia mother na Mzee. Nikafikiria nikampigia na mshikaji. Ile kupokea tu.
Mshikaji: Ilikua nikupigie leo hata saa kumi usiku? Nambie dokta uko poa huko?
mimi: Sijamuona lakini nategemea kumuona kesho.
Mahikji; nambie kweli, unakwenda Unguja kitu kama kile huna habari nacho?
Mimi; Sasa yule si umesema demu wako? Nikuvunjie heshgima Mshikaji wangu?
Mshikjai: Wewe mwana nakujua, huna mazzagazaga siku hizi. Ingekua enzi zako, kwani anagefika hata Unguja yule, wadamganye wengine. Ingekua sijamuona kupanda boti na wewe inhgekua sijaenda kukupeleka bandarini, ningejua saa hizi umemficha sehemu, ile hoteli yenu ya kisenge mliokwenda kukaa sabam halafu sisi washikaji wako hatukupewa kadi.
Mimi; Nimekupigia kukusalimia na kukuuliza gari yake vipi.
Msshikaji: Mwanangu, dingi wako mchaawi wa magari hakuna siju cha kkompyuta zako wala nini, tumnehangaika sisi tumesagfisha tanki la mafuta, tamki lilikua safi kama jipya, mafut asafi, filter zote mpya, tukiitest gari iko vile vile.

Mwanangu dingi wako akasema fungueni boneti, tukafungua, dah, yule mzee sijui ananusa ugonjwa ulipo? Akatazama pale akasema washa gari ile kuwashwa, akaipiga resi kwa mbele, akasema zima gari. Mwanagu yule mzee noma. Kuna kidude hichoi kina paipu ndogoi ndogo na miwaya waya, akakichomoa mwenyewe dakika sifuri tu, akkaikupiza upoanda mmoja kisha akakipyuliza upande mwingine, akasema hii mixer sensor sijui kaita jina gani pale, ndio tatizo, akanambia mimi nkamletee ile sporay haitoki juu ya meza yake,kuoleta, akakipachua akakaippulizia akasafisha vizuri, akakirudishia akaki[puliza tena, akakpachika kwenye gari, cha kupachika pahika tu, hakihitaji hata spana. Ingekua wewe pale ungeitish spana za gereji nzima. Akacheka. Basi mwanagu kupiga stati, steringi mimi hapo, gari kam mpya, unaihisi gonjwa limekwisha, Dingi akasema haya kapige raundi uje usseme kama imebadilika au bado.

Mshikaji; Mwanagu, yule dingi wacha mikampuni imeletee migari yao, wanajua yule mchawi wa magari, yule ukisafiri hulali porini.

Nkaona huyu hanyamazi leo.

Mimi; Hoyaa, kwa hio gari iko poa.
Mshikaji: tena kutoka hapo nimeifanyia mwenyewqe usafi mwanzo mpaka mwisho. Yule Dokta mwenyewe akiiona ataisahau. Halafu mwanagu si nilikwambia yule mtu wa ndumu? Kaacha vizibiti kibao kwenye eshtrei, nimekuta vipisi vitatu, vile bvua mwisho kabisa, halafu yule anaonesha anapiga kavu kavu bila miksi bila nini, vipisi vimejaa asali.

Mimi: Hoyaa, poa bas nyamaza, nilitaka kujua hilo tu. Mie kabla ya kuja nitakupigia unifate.

Mshikaji; Lini mwananhgu, unajiua Unguja vifaa vinauzwa rahisi, mwananhgu nichukulie mziki mmoja mnene, wale nyokjko pale nyumbani wananiringishiavimziki vyao, nataka wakiwasha nikiwasha wangu wote wanazima.

Mimi; Nakuahidi mioana na Dokta nakuletea mimi zawadi ya mziki, lakini wewe si Sheikh siku hizi mziki mnene wa nini?
Mshikaji: Ule niwazime wale tu kelele zao, tutasikiliza Qur'an mule saa zote.

Mimi; Kwa heri. Nikajiweekaaweka swa nikatoka kwenda kwenye msosi.

Nikamkuta meneja, yupo nje ya chumba cha msosi, boitra umeytokea wewe kwanza, hawajafika bado, lakini hawachelewei, ilikua waje dakika 15 nyuma, mara ananamibia hao.
Meneje; Karibuni, karoibuni utafikiri mmeambizana na Simba hapa. Huyu ndie niliwaambia na yeye katokea Dar. Anaitwa Simba, Simba huyiu Bi H na huyu Bi H, wote majina yao yanaanzia na H lakini ni majina tofauti, nitawaita Hw na H2.
H 1: Jina lako linatisha, Simba wapo ngorongoro huko.
Mimi: usiotishike ni jina la ukoo tu, jina langu noi...
H2: hilo Simba ndio zuri zaidi, nimelipenda.
Meneja; Mimi nilichagua tukae pale te)wendeni, najua myatapapenda, alichagua meza amabyo unakiona chumba kizima cha chala.

Tukaenda kukaa pale akaja mhudumu akaleta menu.
H1; Weewe ndio umetualika chakula sasa tuchague tena, wewe tuagizie, wewe ndio unavijua zaidi.

Meneja: Pengine mna miiko ya chakula.
H2: Mimi sina mwiko kwenye kula kasoro kiwe cha halali tu.
H1; hata mimi, labda mwenzetu DSimba hapa.
;Mimi; Meneja mimi sina mwiko kama hawa mabibie hapa. Watachukula nwao na mimi nakula.

Meneja, basi poa, tutaanza na light salad ya kaa, pamoja soup ya Kithailanda inaitwa TomTun Gong, hiyo wenyewe wa Thai wanasema Ni Mfalme wa supu zote duniniani. mtaiependa sana, halafu tutaleta chakula mchanganyiko kidogo kidogo, kila mtu aatakula apendacho na njaa yake. Akacheka.
H1; Njaa nilonayo si ndogo.
Mimi nikakumbuka code yangu na wife nikataka kucheka nikajizuia, lakini H1 alishaniona nikitabasamu.
H1; mbona umefurahi Simba na wewe una njaa?

Meneja huku ananyanyuka, msiwe nashaka kuleni muwezvyo kama hamjatosheka semeni tu kinakuaja, mimi dakika tatu narudi.

H1; Simba umesikia, kula tani yuako kama hujatosheka ongeza tu.
Nikajua huyu bibie kishaipata code.
H2; Mimi ninhgepayta na wine ingekua traha kweli, wine inazisidisaha njaa.
H1; Una yako tu wewe, akanyoosha mkono.
Mhudumu kuona mkono akaja mbio mbio.
H1; Mna red wine zzuri kwa chakula? Zipo aina nyingi lkakini mimi na recommned, akataja jina gani sijui, kwa sababu naoana hio ndio wageni wengi wanaipenda.
H1: Wanaipenda pengine kwa bei rahisi.
Mhudumu; Mama hapa wine zote bei moja tu, niz zuri.
H1p haya tuletee.

Ikaletwa wine kwanza )tukaoneshwa, ikafunguiwa mbele yetu, akatia kwenye glass moja kidogo tuonje, H1 akasema mpe DSimba atuonjee. Mimi nikawaambia pass.
H1: Mpe huyo cha pombe alietaka wine.

Akapewa H2 akaionja kimadaha, akasema iko fresh sana, nitilie akatiliwa, akawa anakunywa peke yake.
Mhudumu; Kama nyinyi mtapenda niwaletee sparkling water ni nzuri kwa chakula.
H1; Wewe unajua mambo, leta hio.

Mhudumu alivyoondoka kuleta.

H2: hajui, sema kweli, angekuletea mambo yako yale, saa hizi ungem hug.
H1; Bado muda wake, subiri nione mazingira hyamekaaje kwanza.

Meneja akarudi na muhudumu akaja kaleta maji mara ikaletwa bakuli kubwa la salad ndogo ndogo nikaona imechangwa na nyama ya kaa. Meneje akaanza kutaka kuwapakulia, kina mama. Wakasema wewe tia chako, sisi tutati wenyewe, ahsante mwanangu. We simba huyu mamake na mimi babu yetu mmoja. kwa hio mimi mwanangu huyu.
Simba.
...113
Dah, tukapiga salad na supu, kweli ile ni Mfalme wa supu, mule ndani kuna kibaridi cha kiyoyozi lakini kijasho chembamba kikaanza kunitoka.
H2; Siku zote tukija hapa tunakunywa supu, llakini hii hya leo kiboko, nasikia joto.
H1: joto au nanihii hizo, hakuna mtoto mdogo haoa sema kweli tu.
H2; Wewe umesema huyu mwanao halafu unaongea upuuzi mbele yake?
H1; Mwanangu tukiwa na mamake huko kwao, huku sisi wote watu wazima, nipishe huko. Kuchangia mababu huko, mimi huyu halali yangu kunioa. Na bahati yake nimeolewa, jinhadsome hili bado bachela, hatukubali. Safari hii hatuondoki Unguja bila kukupa mke. Tena muulize huyu H2, niliposikia nikamwambia huyu tumjulishe nannihii niliokwambisa H2, sitaki kutaja majina. Tena leo anakuja kwa ajili yetu disko na ndugu yake mashoga zake wakiunguja. Meneja leo usikose Disko, nikujulishe na vifaa vilivhyoenda shule kama wewe.
Meneja; Hao si ndio hatari, mimi nataka kuku wa kienyeji, sigtaki vita vyua kila siku nyumbani.
H 1; Vita vya nini mkiwa wote wasomi mnaelewana liugha, huyu I love you, yule I love you more.

Tukacheka,

H1: Simba na wewe ushaoa au bado nikupe mke hukohuko Dar?
Mimi; Tayari nimeoa na watotowawili sasa.
H2; Umewahi sana kuoa wewe?
Mimi; Nimeoa exactly siku ya birthday yangu ya miaka 18.
H1; Sasa kilichokuwahisha nini? Kwanza ungeisoma dunia.
Wazazi walishafanya mipango yao, mimi nikaona poa tu.
H2; Huyu sio mngazija? Tabia za wazee wa kingazija hizo.
Mimi; Hapana sio Mngazija.
H2: basi wazee wa kingazija hata hio kumi na nane hufikishi, ukishabalehe tu unaozwa mbio mbio.
Mimi; Hata sisi kwetu hivyhivyo sema sheria za nchi siku hizi zinabana,
Hq: hamjui sheroa nyinyi, sheria miaka 14 tu unaruhusiwa kuoa na kuolea.
Mimi: Yeah, sheria za kiusoma, tulingojwa tumalize form IV gtu ili tuozwe nadi ikawa coincidence na boirthday yangu.
H1: hapo sawa. Asikudanganye mtu, sheria ya Tanzania ndo ani miaka 14 tu. Huyo H2 najidai, muulize aliolewa wazee wakingazija wamemuoza ana mika mingapi?
H2; Mie nilikua 15 nilipoolewa, 16 mtoto wa kwanza.

H1; Meneja, hii supu, kwanza msilete chakula, wacha niende nje huko garden au beach nikanyoshe migiuu kidogo anipigwe na fresh air.
Maneja: kuna sehemu nje mnaweza kuletewa chakula huko.
H2: napajua, basi vinngiune tutamalizia huko lakini tupeni kama nusu saa ndio mlete. Wacha huyu bibi akanyooshe miguu.

Meneja akasema vizuri huku ananhyanyuka, akasema tutakutana huko. Ile kuondoka tu.
H2: Husewmi una yako tu, unasingizia kunyoosha miguu.

H1 hakujibu akanyanyuka, twendeni simba achana na huyo, kazowe kukaa ndani kama yai, akitoka yeye analiwa tu, ndio anachokijua hicho. Tukanyuka, akatuacha mimi na He, nyinyi ytangulieni mimi nakuja, nikaona kaelekea resepshen, tukaenda beach na H2, kweli kuna sehemu nzuri saja ya kukaa na kula, yaani kuzuri pametulia, mimi ningejua toka jana ningekua nakula huku nje.

H2: Wewe; utamzowea huyo, ana hyake utayaona sasa hivi, anajidai hanywi wine, bado muda wake huyo, wine anapiga vizuri na ma wiski anapiga, muone hivyp hivyo huyo, anajida mwanangu sijui nini, kiroho chote kipo kwa manager.

Mara akaja H1;

H1; Usimsikilize huyo kiini cha yai, kishatoka nje lazima aliwe. Na wine zile na supu ile. Kwanza huyu meneja kwanini siku zote anatuficha hii supu?
H2; Na wewe nae huelewi? kasema ni mfame wa supu, sio malkia wa supu. Hipo ilikua kwa ajili ya simba hapa, fungua akili zako, hio ni zaidi ya supu ya pweza.
H1: Ndicho unachokijua wewe hicho. Akafungua pochi akatoa hanja akchoma. Hiki ndicho kilichonitoa nje, mie mapombe yenu na chakula bila apitaiza siwezi.
H2; Nilijua tu. Huoni haya?
H1; Wakumuonea haya nani huyo Simba? uso wake tu uanonesha wamo huyo, wewe unamunaje mtoto wa Ilala huyo, si umesema kwenu Ilala?
Mimi: Ndio.
H1: Piga ganja usione haya, hakuna mamako wala babako hapa, chukulia sisi marafiki zako ingawa wakubwa kwako.

Tukakaa kaa nje, kikaletwa chakula tukala pale, hata mimi nili enjoy zaidi kula nje.

Baada ya h1 ndio akasema sasa H2 twende zetu tukapumzike ndani, Dieko tutaenda sita au saba usiku. Simaba uje huko, uje ujionee vitoto vya Kiunguja, na miziugu kibao huko. Usikose kuja Simba wetu, nikawaambia poa. Tukaondoka wote, wao wakaelekea chumbani kwao na chumbani kwangu.

Kufika chumbani ikabidi kwanza nipumzike ile kupumzika kikweli, ile supu na ile chakula si mchezo, baharini na upepo ule kijasho kinanitoka. Niakasema hii nitamuuliza meneja tukiwa pekeetu. Wale ma mama hawajanikuta enzi za Usimba.

Nikakoga fresh nikajituoa kitandani, hata nilipolala sijijui, nastuka naona time kusali alfajiri, nikashukuru, Mwenyezi Mungu kaniepusha na shari za usiku. Nikasali, nikasema wacha niende beach, Aisee nikakuta wazungu kibao tayari wapo beach, wenbye kutembea wenye kuogelea wenye kufanya jogging, na mimi nikaunga mkumbo wa kuogelea baharini noikaogelea sana, mpaka nilipoona hoi, nikajisuuza kwenye shower nikaende akupiga breakfast nikaebda chumbani nipige simu simu zangu za muhimu nikapiga piga simu. Nikampigia na mwenyeji wangu Nikamwabia leo asihangaike chakula mchana kwa ajili yangu, mimi nitakula hoteli, Tukakubaliana nitakwenda nikipata nafasi lakini siendi kwa chakula. Nikatoka noikaenda nje kuzunguka nje ya beach, nikaona wnyeji wenhyeji wenyeji, nikatembea sana kama masaa mawili nikapenda sana mandhari ya kule, ni pazuri sana. Pametulia.

mchana mchana nikarudi chumbni kwangu, ile nafika tu, simu ya hoiteli ikaigta, nikajua meneja. Tukasalimiana ple.
Meneja: Simba jana ukawakaimbia kina mama.
Mimi: Sikuwakimbia, supu yako na msosi ndio umenifanya nikimbie, nimelala sina habari kabisa.
Meneja; Mimi ingejua sio kazi nisingeenda nimeenda saa tisa uiku, nililala pia kustuka nikaone ninde kwa kazi zangu, nikaonana nao, wenyeji walisema watakuja wamme walikua sigta, wanawake wanne na wanaume wawili, wote sijuani nao, tukabadalishana namba tu, lakini wanaonesha watu na heshima zao, ni vijana wotw umri wangu au zaidi kidogo, ni wagtu wema kwa ujumla na wame enjoy sana.

Mimi: Hata leo nilikua sipo nimerudi muda huu, niliamua nikatenbee tembee kwa miguu, ndio niliwaambia rese[shen ukirudi wanijulishe, ndio wamenoijulisha nikakupigia.

Mimi; Poa, baadae nigtaenda mjini kabisa huko lakini nitachelewa sana kurudi, kuna sehemu nimealikwa, pengine kurudoi asubuhi.

Meneja; Ukihitaji gari ya kukupeleka na kukurudisha muda wowote ule, waambie resepshen tu. Tukaagana.

Mimi nikajua hapo hajanambia ukweli wote, kwani najua system za milango ya hoteli kubwa, unajulikana upo au haupo chumbani kwa kadi tu zile za kufungulia milango. Lakini nikajifanya sielewi kitu, nikakaa kimya tu.
Simba
...
 
Upande wa visa alhamdulillah mambo yanaenda

Mada ya adam nayo iendelee tafadhali

Asante
 
Vitu vingi sana kwenye dini uzushi, hilo nalijua, nimeanza kuchambua uzushi wa Adam kua ni mtu wa kwanza, kabla sijamaliza, umeleta "tawheed" halafu unasingizia mambo chungu nzima, maana yake ulioitoa ni potofu kama somo lenyewe.

Inaweza kua wewe unajifunza kwa nia njema kabisa, lakini sababu ni ipi? Kupoteza muda? Wakati Qur'an ipo wazi kabisa, inasema Sema, Allahu ni "Ahad" katika Surat Ikhlas. Sasa hio tawheed inahusu nini zaidi ya kupotosha watu tu?

Mtume Muhammad alisomesha somo linaloitwa "Tawheed"?
Simba.
"Mtume Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake"
 
Arsis tu naomba kujua kuhusu mizimu na matambiko, je ni vitu kweli vipo na vina athari katika maisha ya binadamu na je kama sijawahi kushiriki huko ila labda mababu walikuwa waki Fanya hizo Mila na Mimi sizifanyi inaweza kuniletea athari? Ukijibu hili najua wengi utapata faida(elimu) kubwa
 
Tutapata tu elimu, mimi natoa nivijuavyo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, kuna wajuzi humu zaidi yangu.

Yupo kaka yake Etugrul Bey na Nourhan na wao wana elimu yao, ambayo sio yangu.
Simba.

Wapigaji ni wengi sana kupita kiasi katika haya mambo. Hawana dini wala kabila. Wapo wapigaji wakubwa na wadogo.
Simba.
ndio utujibu ww kwa elimu yako hao wengine watatujibu kwa wakati wao..swali limeelekezwa kwako lakini unakwepa kujibu unawarushia mpira wengine au umeona ukijibu utakuwa umetoa siri ya kambi.!
 
Alafu unaposema Quran inasema mwenyezi Mungu ni mmoja si ndio Kwenye somo la TAWHEED wanafundisha ALLAH ni mmoja na rejea yao ni quran mbona kama unapinga kitu usicho na elimu nacho?
Ukisema TAWHEED ni uzushi na TAWHEED inafundisha juu Mungu mmoja kwahiyo kusema Mungu ni mmoja ni uzushi si ndio?
Qur'an haijatosha kukufundisha kua Mwenyezi Mungu ni mmoja mpaka uzushe somo jipya nje ya Qur'an?

Mwenyewe hapo juu kidogo umekiri kua neno tauheed hata kwenye Qur'an halipo. Mimi sasa nakuongezea, hata kwenye hadithi halipo. Umeshakiri kua hujui lilipotokea, au umesahau? Usichokijua kilipotokea kimezuka tu, kwa Kiswahili uzushi.

Mbona mvivu wa kujibu maswali? Usiogope sikutegi, nakupa elimu kwa faida ya wengi.
Simba.
 
ndio utujibu ww kwa elimu yako hao wengine watatujibu kwa wakati wao..swali limeelekezwa kwako lakini unakwepa kujibu unawarushia mpira wengine au umeona ukijibu utakuwa umetoa siri ya kambi.!
Nikujibu wakati uzi mzima huu ni majibu kwa hayo unayouliza, nini ambacho hujakielewa? Uliza tu.
Simba.
 
Basi ndio maana nilikuuliza shida yako ni neno TAWHEED au yanayofundishwa ndani ya TAWHEED?
Japo unakwepa kunijibu ila maelezo yako yanaonyesha shida yako ni neno TAWHEED.
Maana TAWHEED inafundisha juu ya Mungu mmoja ambaye ni ALLAH na wanarejea quran na mtume kafundisha Mungu ni ALLAH sasa shida ni nini hapo?
Mimi nimekujibiu sina shida, Qur'an inajitosheleza, haihitaji neno au somo jipya la uzushi kuielezea.
Usisahau hilo.
Simba.
 
Sijakuambia unitafsirie uzushi kwa kingereza ni nini au kiarabu nataka maana yake.
Narudia uzushi ni nini?
Kitu kutokea kisipojulikana, kuzuka tu, ndio uzushi. Au hujakiri juu huko kua hujui neno na unaloliita wewe somo la tauheed lilipoanzia au kutokea (kuzukia)?

Halipo hilo kwenye Qur'an wala hadithi.

Hilo ni kama Hawa, mpaka leo mmeshindwa kujibu mmemtolea wapi.
Simba.
 
Amekwambia toa maana yake sio unatutafsiria
Usiwe na shaka kabisa, mimi napenda sana mtu ambae hajakielewa kitu aendelee kuuliza mpaka aelewe. Ndio msoni ambae anaelimika.

Uzushi Kiarabu: (بدعة) Kingereza (heresy) au (innovation) inahusu uvumbuzi au uanzishi katika masuala ya kidini ambayo hayapo kwenye Qur'an. Hilo la "tauhewed" hata kwenye hadithi halipo dio maana nimelikoozesha hapo mwanzo.

Kwa ndimi (lisan) tofauti, neno hilo linamaanisha "uvumbuzi, riwaya", mafundisho yaliozuka au kuzushwa tu ni uzushi. Na anaezusha jambo huitwa mzushi.
Simba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom