Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

kwanza anza kusali, usiache kusali na usiache kukaa na udhu. Bila kua kwenye mwili msafi , uache uradi wa kumtaja mwenyezi Mungu kunshukuru na Takbor.

Unategemea machafu yataondoka vipi ukiwa wewe mwenyewe mchafu?
Simba.
Hilo mimi nasisitizia kwa video clip...
Your browser is not able to display this video.


cc: KMkhalid
 
Naomba uzingatie hili swali

Yule farao pale misri ni mwenyew au wa kuchongwa maana kwa miaka uliyoishi hapa duniani naamini zama zake ulikuwepo
 
Kwa lugha hiyo si wepesi hata ingekuwa mimi kukuelewa.
Nimemuelewa, nafahamu mijadala imemuingia na ile bisha bisha yake anashindwa kuitetea kwa ushahidi sasa hizo ni hasira zake, kaona azipumulie kwangu.

Usijali FF, mimi nimemuelewa sana, wala lisan yake hainipi shida, Arsis ndio kabisa, anasema hao ndio wanafunzi wazuri, wana hasira na elimu.
Simba.
 
Duu, zagalo huyo si kocha wa Brazil wa zamani?
Jina tuu. Ila hiko kitabu ni kitabu Kitakatifu cha kiimani cha Wabantu.

Kwenye kdahalo wa Adam na Hawa ndio nikakikumbuka maana na chenyewe kina habari za Mungu na Uumbaji wa ardhi na Mbingu mpaka Binadamu wa kwanza.

Humo Adamu kaandikwa si kama Binadamu wa kwanza kuumbwa ila kama binadamu wa kwanza kumuasi Mungu. Binadamu wa kwanza kuumbwa kaelezewa huko hadi namna alivyoumbika kupitia vumbi la Mabara Saba.

Mi sio mwandish mzuri saana, jaribuni kukisaka maana ni kizuri sana na kina Miongozo mbalimbali ya namna yakuishi kiasili ya Ulimwengu huu. Na kina elimu nyingi zakutafakari.

Arsis Kuna mdau alikuuliza kutokana na maelezo yako ya namna hii dunia ilivyo kishape, Je wanaodanganya umbo lake wanataka kufaidika nini?
 
Sqali zuri sananhili
Naomba uzingatie hili swali

Yule farao pale misri ni mwenyew au wa kuchongwa maana kwa miaka uliyoishi hapa duniani naamini zama zake ulikuwepo
Naona kama alijielezea huko nyuma. tumwachie mwenyewe aje.
 

ionjo vya Arsis 5 -4

nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.


maji yakunywa yakaletwa, bahati yule alietumwa ka;eta chupa sita kwenye plasiti zake.

Mzee; Fungua basi hilo fungashio, wape watu maji na mie nipe chupa moja.

Tukapewa maji wote akasema.

Mzee Ali; Dokta kunywa basi nusu hio moja nataka hayo yako ya kunywa niyatie dawa, tumaliza kazi ya leo.
Dokta: hata siwezi kuyanwa haraka haraka.

Mzee Ali; yapunguze humo kwenye ndoo ya maji.

Mke wa Mzee; Ngoja, nyie watoto leteni gilasi safi, usiyamwage bure Dokta.

Mara yule binti walikua wamekaa nje ya mlango kwa uani, akaleta gilasi.

Mzee Ali akasema hayq lete hio gilasi hapa akaiweka mbele wake akatoa kama unga unga una vijani vijani hivi vimekauka akatia kwenye gilasi kama robo gilasi akmwambia haya lete hio chupa yako uliokwisha fungua. Akaichukua akaijaza yale maji, lile vumbi la maji na vile vijani kama vingine vikapanda juu vingine vikaenea kwenye gilasi.


Mzee Ali; Dokta kunywa kidogo kidogo kwa spidi yako, ukinywa kidogo ongeza maji, hii noiliokutilia kipimo chake maji chupa moja utaiona nzito lakini usiiogope haina ladha yoyote utaona harufu ya majani tu. Dokta akaanza kuinywa kidogo anaongeza maji aksma..

Haya maji si tunaweza kuchanganya kwenye hii chupa maana naona nzito sana.
Mzee Ali: unaweza Dokta, tia humo ongeza maji mengine kwenye gilasi mpka aitapofikia, kunywa kwa raha zako, nradi umalize hayo maji ya lita moja.

Dokta akawa anakunywa taratibu sana, mimi naona Dah hii lita moja huyu Dokta itamchukua saa nzima kuimaliza.

Mimi: Naomba nikasikilize simu kidogo nje, Mzee naomba funguo za gari.
Mzee Ali, anamaliza sasa hivi huyu.
Mimi; Sikawii kabisa.

Nikachukua funguo za gari nikaenda kwenye gari kutazama kweli kuna simu zilipigwa. Nikapiga nisioijua namba. Kupokelewa kwanza ile sauti naijua, lakini kichwa kinanambia haiwezekani.
Mimi: Nani mwenzangu?
Jini1: Wewe kila siku tunaongea leo umesahau sauti yangu?
Mimi: Huu utani au vipi, toka lini tukaongea na simu?
Jini1; Sasa si nimekuhitaji mkuu na wewe uko kwenye vilinge vya uganga, ningekujaje hapo bila idhini yako?
Mimi: Hii kali hii?
Jini 1: Sasa mkuu, ikiw naweza kuja tunakua pamoja, nishindwe kuongea na simu. Tena na simu mpya hata wewe hauna hio. Nimeletewa zawadi na rafiki yako wa Kiarabu tuliekea nae Unguja.
Mimi; Acha utani, sema unataka nini ntaka kurudi ndani.
Jini 1; Arsis anakwambia hata saa ngapi ukirudi uende kule mnakokutana, anataka kuongea na wewe kule.
Mimi; Poa.
Jini 1: Na mimi nitakuja ofiusini kwako kabla hujaenda kwa Arsis, kuna vitu kanambia nimalize mimi tu kukuelezea.
Mimi; Poa, huku nikawa narudi ndani, kweli nikakuta Dokta ndio anamalizia malizia maji yake ya dawa Sijakaa sana akayamaliza.

Mzee Ali; Sasa nenda na huyo mwenzaki uani huko, ukisikia kutapika utatapika kwenye hio ndoo tupu, huyo anajua cha kufanya atakuelekeza.

Wakatoka Dokta na mkewe.

Mzee Ali; Mmeona jamani kazi zetu, hizi ndio zimenitoa kwetu Kojani kunileta mjini huku, matatizo ya majini ni mengi sana.

baba yeye kakaa kimya tu, hua hapoendi kuongelea vitu asivyoivijua au akiwa na mtazamao tofauti, yaani kwa ufupi haendi kubishana kabisa. Mimi nikawa naguna kuashiria kumsikiliza.

Mzee Ali; Sasa hiviu yyule ataanza kutapika uchawi aliomezeshwa. mimi sifahamu kitatoka nini, watu wengine wanatoka mpoka vyura tumboni.

Mimi: dah, hatari.

Mzee Ali: Si ndogo, si umeina mijini ilivyokua inakuja ile, kama sina kinga za kikwetu saa hizi patashika nguo kuchanika, ndio maana siku hizi tunawalisha zile skin taiti wakija kina mama. Bila vile kuna sinema hapa si mchezo. Nyie mmekuta huyu Dokta hivyo vojini vyake vya siku nyingi ndio maana hakua na piroka ypoypote, lakini kuna wale wa kusukumiwa halafu wanajua wanataka kutolewa, inakua earangati humu si la kawaida, wengi tunaita vijana wenye nguvu zao wawafunge kamba.

Mimi; Sasa mnajuaje kama huyo atakua na fujo na huyu hana?
Mzee Ali; uzoefu wa kazi kijana, mimi hii kazi ya ukoo na nimefundishwa na wazee wangu na majini wenyewe wanaonisaidia hizi kazi. Mika mingi sasa, toka mimi mdogo ndio mambo nayoyaona haya.

Haijapita muda yule mkewe wakarudi na ndoo zote mbili ile yenye maji kwanza ilikua imebaki kama nusu na ile tupiu ikawa na maji kiasi hivi.

Mkewe: Nimemwabia Dokta akakoge atulizane, maana anaonesha kachoka sana.
Mzee Ali; haya akimaliza aje kuona mwenyewe kinachoendelea, kazi iliobaki ndogo, huvixhma tu hayo mauchawi aliyatoa. Umelete basi.
Mkewe akatoka kaacha zile ndoo hapo pembeni.
Mzee Ali tazameni tu muone kuna nini?

Mie nikanyuka nikatazama mzee akasema inatosha nikiona mimi tu, yeye hakunyanyuka.
Mimi: naona kama kuna megu mbegu sijui za nini hizi? Na naona kama kiuna hirizi tatu, mboili nyeusi moja nyekundu.

Mzee Ali: hakuna vichupa humo? Au karatasi za tarasimu?
Mimi hakuna ziko hizo tena sijui kama ni herizi hizi au nini?

mzee akanyanyuka akatazama ndani ya ndoo.

Mzee Ali ; hizi sio herizi za kibinadamu, hizi herizi za kijini, itambaa tu hivi vimepigwa fundo, kila tangi hapo na jini wake, itakua majini yanamgoimbani ahuyu, kila mmoja awe ndio kiti chake yeye hapo.
Mara wakarudi, hapoi ndio nikamuona Dokta vizuri, maana alikua amevua lile dira na skin taiti, alikua amevaa abaya zile za ghali inaonesha, na kishakoga yupo fresh. Uong mbaya alikua bomba haswa na ana mzuto fulani na ile rangi yake, Mie moyo paa. Nikamlaani shetani pale.

Mzee Ali; Dokta tazama madude yaliotoka hayo ywambiw unaytajua?
Dokta; siiyajui.
Mzee Ali: sasa hapo tumetoa vifungo vua kijini, bila hivyo kutoka jini haondoki. haimaanishi kama majini wametoka , hawapo kwa saas lakini wanaweza kuingi an kutoka musa wowote mpaka tuwatoe kabisa. Hao kazi ya kuwatoa atakwambia Sheikh... ka leo tumemaliza iliobaki kazi yangu nitaifanyia mwenyewe hapo uani ya kutekeza hivi vifungo.
Dokta; Na hizi mbegu za nini? nazi nimeitapika mimi?
Mzee Ali; Vyote hivyo ndio vifungo vyenyewe, unaweza kukta jiniwa mbegu mwingine, jini wa hizo mwingine, lakini mimi najua hivyo vifundo vyeusi na vyekundu majini ya Kingazja hayo ya koo tpofauti, hayao yanashindana. Yalikua yanakiushndania, sasa inawezekana hizo mbegu vimbomu vyao wanavyopigania au vofungo, lakini nitapata habari zake nitakujulisha kesho kwa simu. Haya Dokta tumealiza kwa leo. Jamani tumemaliza, hio kazi ya leo imeishia hapo, kama mna swali lolote naagana na Dokta nje hapo.

Na mimi na mzee tukatoka, tukakawacha wenyewe waongee kwa mbali huko walipomaliza tukaagana na Mzee Ali tukabadilishan namba. Tukaelekea kwenye gari yetu, tukakutana na dokta na yeye kile kigari kweli kilikua chake.

Mimi: Dokta nimefurahi kukujua.
Dokta: Jinsi nilivyokua taabani hata hii gari naona tabu kuendesha. Nyie mnaendea wapi?
Mimi: Sisi sipo mbali hapa Ilala tu.
Dokta: Mimi nakaa Upanga, hivi hapo Ilala siwezi kupata chakula maana sijala kiti kabisa leo, aliponambia kuna kutapishana sikula kuanzia asubuhi.
Baba: Yupo Barafaa Ilala, chpsi kuku, pzuri kama huwezi kuendesha wacha Simba aendeshe mpaka hapo mimi tutakutana hapo, hata mimi mmenitamanisha kuku wa barafaa. Haya nneda simba kamuwndeshe Dokta. Nikacheka.

Nikashuka Dokta akshuka akakaa kwa abiria, nikaanz akundesha, mimi kimya.
Dokta; Nyinyi mnakaa Ilala na nyinyi mmekuja kwa shida zenu kw Mzzee Ali?
Mimi: Hapana, mimi najuana na Sheikh...wa Unguja ndio kanambia nije kumjua Mzee Ali na nione kazi anazofanya, imekua na wewe ndio upo hapo.


Tukafika kwa Barafaa, ile kuweka gari, barafaa kuniona.
Barfaa; Simba kama kawaida yako, nikamwabia hapan aleo nimekuletea mgeni, Dokta unachukua au unakula hapahapa?
Dokta: Bora nile hapahapa kama utanisubiria nile.
Mimi;l Poa haya twende tukakae palee, naona Mzee kishaingia itabidi anisubiri.


Nikaenda kwenye gari ya mzee nikamwambia akasema sisi tuchukulie nyumbani huyo Dokta akikataa kuendesha mxhukulie teksi wewe noo na gari yake nyumbani titampa mtu ampelekee. Mimi ukija nyumnai nichukulie iule order yetu ya kawaida. Akamuaga Dokta kwa mabli, akaondoka zake.

Mimi: Barafaa ile kawaida yangu ya kuchukua nifungie na pale tupe nusu mbili na chpsi na juisi kwa wingi, jagi moja na glasi.

Barafaa: Poa Simba, umeongeza mke? Au uko njiani?
Mimi; IshaaAllah iwe dua ya heri.

Tukala pale na dokta nikam zee alivyosema, dokta akasema hajisikii vizuri, labda kwa yale maji madawa aliopewa, lakini amaekula vizuri atapata nguvu na juisi ile akaipenda ya Barafaa, akatiliwa kwenye chupoa za takeaway, nikamchukulia taxi tukabadilishana namba nikamwabia sasa hivi kuna kijana atamepelekea gari yake, atampigia amuelkeze wapi. Dokta akasema hakuna shida akaondoka na mimi nikaondoka nazigo nikulitegemea. Nikakuta mzee kishawambia kuna kuku chipsi nakuja nazo, nikakuta nyumbani wanazingoja kwa hamu. Nikawawachia pale nikaenda na mimi kukoga kubadili kujipumzisha kidogo niende kwa arsis. Nikakumbiuka Jini1 alisema anata aongee na mimi.

Nikaingia ofisini kwangu ili niongee nae.
Simba.

...5.5
 
Hapo sasa si unatoboa siri za mwenye matatizo, watu si washajua Dokta gani huyo nwenye kigari hicho na aliolewa na madokta wawili?
. Huyo Mzee Ali si unampaisha kwa makusudi?
 
hakuna anefaidika na chohocte zaidi ya elimu kihitilafiana. Labda Arsis akija atueleze fikra zake, siwahi kumuuliza hilo.
Simba.
 
Naomba uzingatie hili swali

Yule farao pale misri ni mwenyew au wa kuchongwa maana kwa miaka uliyoishi hapa duniani naamini zama zake ulikuwepo
Arsis alishawahi kuandika humu kaihshi na Ramses na Barsis, katika Mafarao. Pia aliwahi kusema mafarao wapo wengi soio mmoja na wapo kwa miaka mingi sana sio kama tunavyoambia sasa mia elfu 3 au nne au tano.

Arsis alienda mbali na kusema hata wanaedai ni Mariam mwana Yesu na kikagtika koo za Kifarao, jina lake ni ni Meritaton kwa kifarao.
Simba.
 
Hapo sasa si unatoboa siri za mwenye matatizo, watu si washajua Dokta gani huyo nwenye kigari hicho na aliolewa na madokta wawili?
. Huyo Mzee Ali si unampaisha kwa makusudi?


Ni moiaka mingi sana nyuma, "mficha maradhi kifo humuumbua".

Mzee Ali hata sifahamu kama bado mpaka sasa yupo Buguruni, sina sababu ya kumpigia debe. Wajinga ndio waliwao.
Simba.
 

Mkuu swali jepesi sana hilo acha kupoteza muda ! Lina majibu mawili tu kabla ya ufafanuzi wowote! Ni aidha ndiyo imeruhusiwa ama hapana haijaruhusiwa . Muuliza swali hakuhitaji tafsiri ya kilugha na hii ni kulingana na jukwaa! Hatuko hapa kujifunza isimu. Muulizaji alitaka tafsiri ya kimaana.
 
Ngoja nilete fujo kidogo ! sisi tusiokuwa na elimu ya dini ya kiislamu tunaielewa dini yetu kupitia fahamu za wema waliotangulia ie maswahaba, tabi, tabitabiin nk, kuhusu itikadi nyingi zilizopo hilo sio mada yetu kwa vile mtume aliliweka wazi. Abuu Dawud anasimulia kuwa alimsikia mtume akisema; 'wasomi aka wanazuoni ndio warithi wa mtume', hii inatupa nguvu sisi ya kuielewa dini kupitia fahamu za hawa wanazuoni.

Binafsi nataka kufahamu ndugu yetu Arsis yeye anataka kutufundisha kuielewa qur an hususan kwenye kisa cha mzee Adam kupitia ufahamu wa nani? au anataka tumuongeze kwenye kundi la hawa wema waliotangulia ingawaje yeye bado yupo hai? nataka Arsis atuambie amejifunza dini ya kiislamu kwa nani ili awaondolee mashaka wote wanaohisi ubatili wa mafundisho yake.

Mwambie Arsis hapa watu wanahitaji literal meaning pekee, tafsiri za kilugha haziwezi kuwa changamoto kwahio awache kupoteza muda.
 
Ujumbe niliupata hujanikosea,wala sijakasirika kisa kumwambia kaka yangu hana elimu sababu iko hivyo hao ma Sheikh na wanasengenyana wanakashfiana kila mmoja anajiona bora hivyo sijakasirika sababu hio,nilikwazikasikupenda wewe kuanza kashfa sijui sauti yake kama ina mafua na nilikuambia ana sinusitis alisha fanyiwa oparesheni,hata hivyo mie sio mtu wa kukasirika kununa haswa muda mrefu ndo maana mume wangu anipenda 😁hunisifia sijui kununa dakika 5 nishasahau hivyo usijali sina kifundo niko poa nilikuamua tu kuendelea na nyuzi zingine ili tusije kugombana kukashfiana sababu niliupenda huu uzi kwenye visa vyako toka kwa babu Kamba🍤 ilipo ingizwa maswali na majibu kadri siku zilivyo enda hamu ya uzi huu ikapotea na kuja kusoma visa vya koo za Simba nikachoka kabisa 🙉ila pamoja sana.
 
Sawa ila nataka kujua sasa yule farao wa pale makumbusho misri ni mwenyew au wakuchongwa?????
 
Mi namuuliza Arsis. Anakijua Kitabu cha ZUGRIL ZAGALO (Nguvu iliyodumu katika Jadi) ?
Sikijui, mimi naona hio ni habari mpya sana sana sio ya zamani kabisa.

Vitabu vya zamani vya Africa ni pamoja na cha Yahya, kaka yake Yesu na mtoto wa Mariam au wanakiita Sabai kedush. Wamebadili sasa wanaita Meshafa Kedush.

maandiko yote ya zamani sana ya Misri ni ya Afrika.

Zagalo Kiarabu ni Zaghloul, huyu unampata katika hadithi za kutunga za zamani za mesopotamia za Harun Rashid. Wuyo Zaghloiul nfio huyo Kiswahili wametfasiri Abunuwas.

Soma kuhusu maktaba ya zamani ya Timbuktu, utapata vitabu vingi sana. Halafu Waafrika wajinga sana, wanawawachia wazungu eti ndio wafanye tafiti na uhifadhi wa hio maktaba ya zamani sana. Wanafikiri kitabaki kitabu cha maana? Hali kadhalika kwa Maktaba ya Fatma AlFikhri.

Sina elimu na hio kitabu.
Arsis.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…