Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Status
Not open for further replies.
Huyo alex anabahati sana, kwani kwa hekima nyingi ulizonazo zinamtia nguvu na baraka. Nashangaa mwanaume kubadiri dini, why?!! Ni mwanamke anaetakiwa kufanya hivo, kama ikitokea. Kweli mke mwenye hekima humfurahisha mmewe.
 
Mmmh hii story naisikia inasomwa now clouds ala za roho.mwandishi umemwandikia na Diva PIA? Au .....
 
story yako ina mvuto wa drama flani hivi za mapenzi ya kihindi,inanikumbusha movie moja ya Shah Rukh Khan inaitwa DARR,ina mapenzi flani hivi extreme.Hii inaitwa devils love,mtu anaweza sacrifice chochote for love.

katika story yako theme ni "character".ni kweli pande za imani zote kuna watu wana 'outstanding character'

tatizo sio mapenzi tatizo ni shirk.

kama ni ushauri ,penda utakavyopenda,fanya juu chini usife mshirikina na usiache kizazi cha washirikina
 
Mm na ww nani amekaririshwa?, mnaamini kiwanda tu ndio kinaweza kutoa ajira kwa raia 300

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe katika akili yako,hata uwe na akili ya kitoto,unafikiria kuajiri watu 300,ni kazi ndogo,kuna kampuni kubwa za magari,zimeanza siku nyingi,na utakuta wameajiri watu hawazidi 50,itakuwa mtu aliyeanza biashara kwa miaka 6,awe ameajiri watu 300.
 
Wewe katika akili yako,hata uwe na akili ya kitoto,unafikiria kuajiri watu 300,ni kazi ndogo,kuna kampuni kubwa za magari,zimeanza siku nyingi,na utakuta wameajiri watu hawazidi 50,itakuwa mtu aliyeanza biashara kwa miaka 6,awe ameajiri watu 300.
Povu la sabuni gani mkuu kwani kuajili watu 300 kuna shughuli gani? watu wana viwanda vidogo vidogo wameajili watu karibia 80 ndani ya miaka 2 je hao wa miaka sita wanashindwa nininkuajili watu 300

na kashakwambia wanamiliki biashara mbali mbali

tuchukulia mfano wa shule unadhani huwa inawaajiliwa wangapi? kuanzia walimu wafanya usafi wapishi etc?

Msiwe na mawazo mgando kuna biashara nyingi tu ambayo unaweza ajili watu wengi hata kama ni vibarua as long as umewaajili
 
Hongera salma star hizi dini zimekuja na mashua tu as long as unamwamini Mungu aliye hai hata mwislam mkristo mbudha au dini yoyote we fata moyo wako mwisho wa siku wote tutakutana peponi....
 
mungu hayupo kwenye Dini na ukiona watu wanazungumzia dini jua hawaelewi wanachokiabudu, mungu anakuhitaji wewe na sio hiyo miungu ya kiarabu
 
Hujanishawishi bado
Aisee

Ila hongera mwaya

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa Pole inaonyesha unaumwa. Pili swali tu. Ulitaka akushawishi vipi sasa .afu iweje. Information could only be for encouraging people facing challenges in life. It could be applied in business,in studies even in love. Kama shule za msingi hawajafungua basi we mtoro. Huko ndo kuna 1+1 =2.
 
Povu la sabuni gani mkuu kwani kuajili watu 300 kuna shughuli gani? watu wana viwanda vidogo vidogo wameajili watu karibia 80 ndani ya miaka 2 je hao wa miaka sita wanashindwa nininkuajili watu 300

na kashakwambia wanamiliki biashara mbali mbali

tuchukulia mfano wa shule unadhani huwa inawaajiliwa wangapi? kuanzia walimu wafanya usafi wapishi etc?

Msiwe na mawazo mgando kuna biashara nyingi tu ambayo unaweza ajili watu wengi hata kama ni vibarua as long as umewaajili
Mkuu kuna watu wana mawazo ya kimasikini sana binafsi watu kama hao huwa sitaki kuwaamsha wache waendelee kutokuamini
 
Yaan wewe dada umenisikitisha vbaya mnoooo...
Kwanza,usitudanganye wazazi wako walikua na dini...NOoooo...mwenye dini hamruhusu bintiye aingie kwenye ukafiri afu bado mahusiano yawepo..

Ni kweli dunia imeachwa na fitna ya watoto,wanawake na mali.
Mzazi aliye na dini akubali mwanae aritadi?!!!..kuna walakin hapo!

Yaan tumbo la chango la uzazi limeniuma...Wallwahi kuna siku utajutia hii thread yako,,,roho inaniuma utadhni ni mdgo wangu au mwanangu anaeelezea huu upuuzi!

Na hvi upo kwenye mali sa hvi,ndo utazidi kuhadaika...Namuomba Allah akufungue milango ya faham ujione ulivyopotea!!!..

Yaa RABBI BARIKI UZAO WA TUMBO LANGU...



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiumize kichwa,huyu mwandishi ni mwanamme,na ni story za kutungwa.Hawa wagalatia,wako tayari,wawalipe watu,halafu wawalete kwenye mkutano wa kuombewa,wakidanganya kama walikuwa vilema,au wamechukuliwa msekule,au alikuwa hapati uzazi.Au wanachukuwa watu kuwapaka usoni masinzi,na nguo za kiganga,na vibuyu,na vitambaa vya kushona kama hirizi,halafu wanasema wamekamata wachawi.Watu siku hizi,wameshawashtukia.Walipoona huko wameshtukiwa,siku wanaanzisha gia mpya,ya uandishi huu na kujiita mtume,au alikuwa muislamu,akaenda somea majini Saudia Arabia,wakati huko Saudi Arabia,ukikamatwa na kitabu cha uchawi,unafunguliwa mashtaka.
Me mwenyewe nahisi ni propaganda ya Makafiri Mola awalaani..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
story yako ina mvuto wa drama flani hivi za mapenzi ya kihindi,inanikumbusha movie moja ya Shah Rukh Khan inaitwa DARR,ina mapenzi flani hivi extreme.Hii inaitwa devils love,mtu anaweza sacrifice chochote for love.

katika story yako theme ni "character".ni kweli pande za imani zote kuna watu wana 'outstanding character'

tatizo sio mapenzi tatizo ni shirk.

kama ni ushauri ,penda utakavyopenda,fanya juu chini usife mshirikina na usiache kizazi cha washirikina
Na washirikina wote wataingia katika moto wa Jahannam...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nashukuru sana kwa kunitia moyo haikuwa rahisi lkn Upendo ulisimama kati yetu hatimaye tukaungana, tumekuwa msaada hata kwa wale waliotusema vbya
Huo upendo ndo utakuingiza katika moto wa Jahannam...

Natamn kwenye watoto wako mmoja asilim awe anakupa neema zilizojaa katika uislam...!

Yaan wewe ni fungu la kukosa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wana MMU!

Najisikia kushare nanyi story ya mahusiano yangu maana ina mafunzo mengi ndani yake.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwanamke niliyelelewa kwenye familia ya watu wa imani na msimamo thabiti wa dini ya kiislam.

Baba na mama yangu ni swala tano hivyo hata sisi watoto tulijikuta tuna angukia huko huko!

Siku moja nikiwa natoka dar kwenda kuanza kazi mwanza nilibahati kukaa jirani na mkaka mmoja. Nikiwa nimevalia waswahili wanasema kininja.

Baada ya kuingia kwenye basi nilifika ktk siti yangu na kumsalimia jirani yangu ambaye siku hiyo nilikaaa naye siku nzima.

Yule kaka alikuwa mkristo lakin alikuwa ni mtu mstaarabu sana. Safari ilianza tukawa tunazungumza hili na lile ilimradi midomo isichache.

Tulipofika mwanza tulibadirishana namba za simu kisha kila mmoja akaelekea kwenye uelekeo wake.

Nilipenda utulivu wake na maongezi yake kwani yalikuwa ya staha na yaliyojaa hekima , pamoja na hilo ukarimu wake ulikuwa kivutio kikubwa kwangu kwani kila alichonunua njiani alininunulia nami pia.

Baada ya kuacha zilipita siku tatu ndipo akanitumia meseji ya kunisalimu Tuliendelea na mawasiliano kwa muda wa mwezi mmoja tukajikuta tume fall in love...

Kipindi nimekubali kuanza nae mahusiano sikujali habari ya tofauti za dini kwakuwa nilijua ilikuwa kwa muda tu., kumbe sikujua kuwa muonja asali huwa haonji Mara moja.

Tulianza mahusiano , nikajikuta nimezama mzima mzima, tukadumu miezi sita tukiwa kwenye penzi moto moto,, hakuna akiyetamani kuona mwenzie anakwenda mbali.

Ikafika kipindi tukakubaliana kufunga ndoa, yaani alinifanya niwe kipofu maana sikutaka kuona namkosa , na yeye hivyo hivyo,ingawa kila nilipokumbuka namna ya kuwaeleza wazazi nilihisi wangekuwa kikwazo.

Nikajitutumua na kuwaeleza , kwakweli haikuwa rahisi,nilipingwa na kila mtu nyumbani. Nilimpigia simu mpenzi wangu na kumueleza msimamo wa wazazi, nakumbuka aliniuliza swali moja tu..unanipenda kwa dhati nikajibu ndiyo ..akajibu nisiwe na hofu tutavuka pamoja.

Nyumbani wakanipa mashart kama nataka kuolewa na Alex (siyo jina halisi) basi nimwambie akubali kubadili dini.

Binafsi niliona isingekuwa rahisi mwanaume kubadiri dini kumfuata mwanamke hata hivyo pia sikuona vyema kuona my man anabadiri dini kwasababu yangu maana niliamini mm ndiye wa kumfuata.

Nikamwambia vile wazazi walivyosema..Alex alinijibu for the sake of our love nipo tayari kubadiri lkn mm sikuona vyema mwanaume kumfuata mwanamke hivyo nilimzuia asifanye hivyo aniache nipambane.

Nilitafuta muda nikaongea na baba kwa undani akanielewa na kumshawishi mama hatimaye tukaruhusiwa kufungua ndoa...

Nilikubali kubadiri dini kwaajili ya upendo nimkamfuata Alex ...tukafunga ndoa mwaka 2008 , maisha yakaendelea, sikuwa na shaka na upendo wa Alex kwangu.

Nakumbuka tulianza maisha tukiwa masikini sana Alex akiwa Mwalimu wa sekondari nami nikiwa mwalimu wa shule ya msingi.

Baada ya miaka mitatu Alex aliniomba aache kazi aingie kwenye biashara, nilipinga lkn baadae nikakubali.

Nakumbuka alianza na biashara ya Mbao toka mafinga , biashara ikakuwa akafungua duka kubwa la vifaaa vya ujenzi. Biashara ikawa kubwa sana kiasi cha kunilazimisha namimi kuacha kazi ili tusaidiene kusimamia.

Nashukuru Mungu tulikuza mtaji tukajikutana tunaingia kwenye biashara ya mabasi.

Wakati yote haya yanaendelea Alex alizidisha upendo kwangu , nilichofanya nikumtii na kumpenda zaidi, tulipendana na kudumu ktk upendo.

Mungu ametujalia watoto watatu sasa na tukiwa na biashara nyingi huku tumeajili zaidi ya watu 300.

Mpaka hivi naandika Upendo wangu na Alex unaongezeka kila kukicha

Nihitimishe kwa kusema Upendo wa kweli hauzuiliwi na chchte.

Wasalaam.
kila mtu atabeba kadhia zake siku hiyo!hongera kwa kuretardi kwa sababu ya ngono
 
Hongera Salma...tena ungebadili na jina kabisa uitwe Magdalena... achana na hawa wafuasi wa uncle Muddy, hawajielewi!! wanaona kama vile wamepoteza muislamu mmoja,shubhaakhamiiit
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom