Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Status
Not open for further replies.
Dada Salma habari yako, umesema kwamba wazazi wako ni waislam kwa hiyo na wewe ukajikuta unaangukia huko, naomba nikuulize hivi je huo uislam wako wewe ni wa kurithi tu kwa kuwa baba na mama ni waislam au uliusoma uislam na ukajua taratibu zake?.
Maana unaweza ukajifariji kuwa umetetea upendo wako lakini hukujua kile ulichokiacha kwa sababu ya upendo kina thamani gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kinachozidi Upendo

Hayo mengine ni chochovyo mfu.
 
Wasalaam wana MMU!

Najisikia kushare nanyi story ya mahusiano yangu maana ina mafunzo mengi ndani yake.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwanamke niliyelelewa kwenye familia ya watu wa imani na msimamo thabiti wa dini ya kiislam.

Baba na mama yangu ni swala tano hivyo hata sisi watoto tulijikuta tuna angukia huko huko!

Siku moja nikiwa natoka dar kwenda kuanza kazi mwanza nilibahati kukaa jirani na mkaka mmoja. Nikiwa nimevalia waswahili wanasema kininja.

Baada ya kuingia kwenye basi nilifika ktk siti yangu na kumsalimia jirani yangu ambaye siku hiyo nilikaaa naye siku nzima.

Yule kaka alikuwa mkristo lakin alikuwa ni mtu mstaarabu sana. Safari ilianza tukawa tunazungumza hili na lile ilimradi midomo isichache.

Tulipofika mwanza tulibadirishana namba za simu kisha kila mmoja akaelekea kwenye uelekeo wake.

Nilipenda utulivu wake na maongezi yake kwani yalikuwa ya staha na yaliyojaa hekima , pamoja na hilo ukarimu wake ulikuwa kivutio kikubwa kwangu kwani kila alichonunua njiani alininunulia nami pia.

Baada ya kuacha zilipita siku tatu ndipo akanitumia meseji ya kunisalimu Tuliendelea na mawasiliano kwa muda wa mwezi mmoja tukajikuta tume fall in love...

Kipindi nimekubali kuanza nae mahusiano sikujali habari ya tofauti za dini kwakuwa nilijua ilikuwa kwa muda tu., kumbe sikujua kuwa muonja asali huwa haonji Mara moja.

Tulianza mahusiano , nikajikuta nimezama mzima mzima, tukadumu miezi sita tukiwa kwenye penzi moto moto,, hakuna akiyetamani kuona mwenzie anakwenda mbali.

Ikafika kipindi tukakubaliana kufunga ndoa, yaani alinifanya niwe kipofu maana sikutaka kuona namkosa , na yeye hivyo hivyo,ingawa kila nilipokumbuka namna ya kuwaeleza wazazi nilihisi wangekuwa kikwazo.

Nikajitutumua na kuwaeleza , kwakweli haikuwa rahisi,nilipingwa na kila mtu nyumbani. Nilimpigia simu mpenzi wangu na kumueleza msimamo wa wazazi, nakumbuka aliniuliza swali moja tu..unanipenda kwa dhati nikajibu ndiyo ..akajibu nisiwe na hofu tutavuka pamoja.

Nyumbani wakanipa mashart kama nataka kuolewa na Alex (siyo jina halisi) basi nimwambie akubali kubadili dini.

Binafsi niliona isingekuwa rahisi mwanaume kubadiri dini kumfuata mwanamke hata hivyo pia sikuona vyema kuona my man anabadiri dini kwasababu yangu maana niliamini mm ndiye wa kumfuata.

Nikamwambia vile wazazi walivyosema..Alex alinijibu for the sake of our love nipo tayari kubadiri lkn mm sikuona vyema mwanaume kumfuata mwanamke hivyo nilimzuia asifanye hivyo aniache nipambane.

Nilitafuta muda nikaongea na baba kwa undani akanielewa na kumshawishi mama hatimaye tukaruhusiwa kufungua ndoa...

Nilikubali kubadiri dini kwaajili ya upendo nimkamfuata Alex ...tukafunga ndoa mwaka 2008 , maisha yakaendelea, sikuwa na shaka na upendo wa Alex kwangu.

Nakumbuka tulianza maisha tukiwa masikini sana Alex akiwa Mwalimu wa sekondari nami nikiwa mwalimu wa shule ya msingi.

Baada ya miaka mitatu Alex aliniomba aache kazi aingie kwenye biashara, nilipinga lkn baadae nikakubali.

Nakumbuka alianza na biashara ya Mbao toka mafinga , biashara ikakuwa akafungua duka kubwa la vifaaa vya ujenzi. Biashara ikawa kubwa sana kiasi cha kunilazimisha namimi kuacha kazi ili tusaidiene kusimamia.

Nashukuru Mungu tulikuza mtaji tukajikutana tunaingia kwenye biashara ya mabasi.

Wakati yote haya yanaendelea Alex alizidisha upendo kwangu , nilichofanya nikumtii na kumpenda zaidi, tulipendana na kudumu ktk upendo.

Mungu ametujalia watoto watatu sasa na tukiwa na biashara nyingi huku tumeajili zaidi ya watu 300.

Mpaka hivi naandika Upendo wangu na Alex unaongezeka kila kukicha

Nihitimishe kwa kusema Upendo wa kweli hauzuiliwi na chchte.

Wasalaam.
Dini kwako haikuwa na maana na hukuwahi kusoma au kuijua dini yako. Thats make nosense in your story !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wavaa ninja, masuruale mafupi na wafuga ndevu hawatapenda hii stori.. Lakini ingekua mwanaume ndio kakufuata ungeona jinsi wangekupongeza..

Hongera kwa kutetea penzi lako, dini haimpeleki mtu mbinguni..
NI KWELI KABISA
 
Mmebanwa pabaya,bakini kudanganyana makanisani,mkija kwa wanaume,mjipange.Kwa vile wewe ni jike,ndio wajuwa wivu wa kike.
Hawa pia ni Waislam maninja

Hawana tofauti na Aisha mapaja nje wa Tandale....ajinasibuye kuwa mwenye udhu wakati dhakali za wanaume kwake aita Sunnah

2017-03-26-09-25-11--1186129004.jpeg

kila mtu atabeba kadhia yake ila wewe majanaba lazima yawe accumulated hadi ufe nayo
 
Hawa pia ni Waislam maninja

Hawana tofauti na Aisha mapaja nje wa Tandale....ajinasibuye kuwa mwenye udhu wakati dhakali za wanaume kwake aita Sunnah

View attachment 568918
Ninja yuko wapi hapo.Kila kona mmebanwa,uongo wa vilema,misukule,kufufua waliokufa,mumeona mmeshtukiwa,sasa mmehamia kwenye story za uongo.Hapo pia mmeshtukiwa,tafuteni gia nyingine sasa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninja yuko wapi hapo.Kila kona mmebanwa,uongo wa vilema,misukule,kufufua waliokufa,mumeona mmeshtukiwa,sasa mmehamia kwenye story za uongo.Hapo pia mmeshtukiwa,tafuteni gia nyingine sasa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Dada yako Aisha wa Tandale Alhamis alikeshea dushe ijumaa akaamkia Masjid na janaba lake

Ila akienda masjid kuutwa kutuvalia kama maninja

Yule jini lake ni zaidi ya jini la mahaba.
 
Napenda kweli member wenye. kuinogesha JF kama wewe umejiunga tarehe 5 august tarehe 10 ukatupia thread ikapata 11 reply Leo tarehe 16 august umetupia tena nyingine
Nakutakia membership njema hapa JF karibu sana
Dah mkuu tutapaisha chopa ngani kweli???
 
Anayefanikiwa Duniani ni kwa neema za kumcha Mola wake na kujituma kadiri ya uwezo wake kufikia mafanikio....mtu wa kwanza kuingia motoni ni masikini anayepoteza muda wake kumfikiria tajiri kaupataje utajiri wake.

Kujituma hata kubadili dini ili umpate tajiri?? Sidhani
 
ikiwa kama mume/mke bora hutoka kwa mola je huyu mume aliempata atakua katoka kwa shetani?

Kuna jamaa alisema kuwa duniani ili ufanikiwe lazima ujitume. Nadhani amempata huyu mume kwa kujituma saana
 
ikiwa kama mume/mke bora hutoka kwa mola je huyu mume aliempata atakua katoka kwa shetani?

Kuna jamaa alisema kuwa duniani ili ufanikiwe lazima ujitume. Nadhani amempata huyu mume kwa kujituma saana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom