Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Status
Not open for further replies.
njiwa KWANI WEWE UNA UHAKIKA KUWA UTAIONA PEPO? UMETENDA DHAMBI NGAPI HAPA DUNIANI MPAKA UNAMHUKUMU MTU ALIYEBADILI DINI?

KUBADILI DINI SIYO KUMBADILI MUNGU, MUNGU NI MMOJA TU NA DINI NI NJIA TU YA MAWASILIANO KATI YA BINADAMU NA MUNGU.. HVYO KUITWA MUISLAMU HUKU UKITENDA DHAMBI HAIKUONDOLEI ADHA YA MOTO HUKO JEHANAMU.. KABLA YA KUMHUKUMU MWENZAKO JIHAKIKISHE KUWA WEWE NI MSAFI KWA 100%

ALIYERITHI DINI NI MPUMBAVU KULINGANISHA NA MTU ALIYEINGIA KATKA DINI AKIWA NA AKILI ZAKE TIMAMU.
Mungu ni 1 nani kasema?
Na wale Mungu baba,mwana na roho mtakatifu nao unawapa daraja gani?
 
Wengi humu ni wivu tuu umewajaa. Hongera sana napenda sana watu walio na positive attitude kama yako. Ndoa ni jinsi mnavyotaka iwe ww na mwenzio. Suala la dini nadhani ni complications tuu zisizo na msingi
you are very right dada Cajojo
 
Hongera kwa ilo ila bado hujaniaminisha kama kweli umetoka katika malezi ya kidini.kubadili msimamo wa dini kufuata kitu cha mpito no ngumu sana na sio kwawepesi uliosema eti wazazi wamekuelewa ju ya swala ilo(no story ya kutunga tu iyo)[HASHTAG]#Salma[/HASHTAG] star

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wana MMU!

Najisikia kushare nanyi story ya mahusiano yangu maana ina mafunzo mengi ndani yake.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwanamke niliyelelewa kwenye familia ya watu wa imani na msimamo thabiti wa dini ya kiislam.

Baba na mama yangu ni swala tano hivyo hata sisi watoto tulijikuta tuna angukia huko huko!

Siku moja nikiwa natoka dar kwenda kuanza kazi mwanza nilibahati kukaa jirani na mkaka mmoja. Nikiwa nimevalia waswahili wanasema kininja.

Baada ya kuingia kwenye basi nilifika ktk siti yangu na kumsalimia jirani yangu ambaye siku hiyo nilikaaa naye siku nzima.

Yule kaka alikuwa mkristo lakin alikuwa ni mtu mstaarabu sana. Safari ilianza tukawa tunazungumza hili na lile ilimradi midomo isichache.

Tulipofika mwanza tulibadirishana namba za simu kisha kila mmoja akaelekea kwenye uelekeo wake.

Nilipenda utulivu wake na maongezi yake kwani yalikuwa ya staha na yaliyojaa hekima , pamoja na hilo ukarimu wake ulikuwa kivutio kikubwa kwangu kwani kila alichonunua njiani alininunulia nami pia.

Baada ya kuacha zilipita siku tatu ndipo akanitumia meseji ya kunisalimu Tuliendelea na mawasiliano kwa muda wa mwezi mmoja tukajikuta tume fall in love...

Kipindi nimekubali kuanza nae mahusiano sikujali habari ya tofauti za dini kwakuwa nilijua ilikuwa kwa muda tu., kumbe sikujua kuwa muonja asali huwa haonji Mara moja.

Tulianza mahusiano , nikajikuta nimezama mzima mzima, tukadumu miezi sita tukiwa kwenye penzi moto moto,, hakuna akiyetamani kuona mwenzie anakwenda mbali.

Ikafika kipindi tukakubaliana kufunga ndoa, yaani alinifanya niwe kipofu maana sikutaka kuona namkosa , na yeye hivyo hivyo,ingawa kila nilipokumbuka namna ya kuwaeleza wazazi nilihisi wangekuwa kikwazo.

Nikajitutumua na kuwaeleza , kwakweli haikuwa rahisi,nilipingwa na kila mtu nyumbani. Nilimpigia simu mpenzi wangu na kumueleza msimamo wa wazazi, nakumbuka aliniuliza swali moja tu..unanipenda kwa dhati nikajibu ndiyo ..akajibu nisiwe na hofu tutavuka pamoja.

Nyumbani wakanipa mashart kama nataka kuolewa na Alex (siyo jina halisi) basi nimwambie akubali kubadili dini.

Binafsi niliona isingekuwa rahisi mwanaume kubadiri dini kumfuata mwanamke hata hivyo pia sikuona vyema kuona my man anabadiri dini kwasababu yangu maana niliamini mm ndiye wa kumfuata.

Nikamwambia vile wazazi walivyosema..Alex alinijibu for the sake of our love nipo tayari kubadiri lkn mm sikuona vyema mwanaume kumfuata mwanamke hivyo nilimzuia asifanye hivyo aniache nipambane.

Nilitafuta muda nikaongea na baba kwa undani akanielewa na kumshawishi mama hatimaye tukaruhusiwa kufungua ndoa...

Nilikubali kubadiri dini kwaajili ya upendo nimkamfuata Alex ...tukafunga ndoa mwaka 2008 , maisha yakaendelea, sikuwa na shaka na upendo wa Alex kwangu.

Nakumbuka tulianza maisha tukiwa masikini sana Alex akiwa Mwalimu wa sekondari nami nikiwa mwalimu wa shule ya msingi.

Baada ya miaka mitatu Alex aliniomba aache kazi aingie kwenye biashara, nilipinga lkn baadae nikakubali.

Nakumbuka alianza na biashara ya Mbao toka mafinga , biashara ikakuwa akafungua duka kubwa la vifaaa vya ujenzi. Biashara ikawa kubwa sana kiasi cha kunilazimisha namimi kuacha kazi ili tusaidiene kusimamia.

Nashukuru Mungu tulikuza mtaji tukajikutana tunaingia kwenye biashara ya mabasi.

Wakati yote haya yanaendelea Alex alizidisha upendo kwangu , nilichofanya nikumtii na kumpenda zaidi, tulipendana na kudumu ktk upendo.

Mungu ametujalia watoto watatu sasa na tukiwa na biashara nyingi huku tumeajili zaidi ya watu 300.

Mpaka hivi naandika Upendo wangu na Alex unaongezeka kila kukicha

Nihitimishe kwa kusema Upendo wa kweli hauzuiliwi na chchte.

Wasalaam.
Wasalaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yule mzee wa dini nyingine baada ya kuambiwa mpenzi wa mtoto wake ni dini nyingine alisema

sikuchagulii mtu wa kuoa, ila nachagua dini lazima awe.............kupewa habari nikasema isiwe tabu najua unanipenda nami nakupenda pia tusiwakosee wazazi olewa na wa dini yako.

mwaka wa 2 yupo ndoani maisha msisimko na cocacola hakuna shida. yule mzee udini utamuua nilitaka mpiga mimba mwanae nisepe ila kwa vile nampenda nilimuacha salama
 
Wafikiri hii habari ni ya kweli?Sio habari ya kweli:
1:Angalia mwandishi,anavyoshindwa kutofautisha kati ya 'r' na 'l'.
2.Mwandishi hakutufahamisha toka mwanzo kama ni waajiriwa,hasa yeye kuwa mwalimu,si rahisi kumpata mwalimu wa kike kuvaa ninja,wa shule za serekali.
3:kuajiri watu 300,sio mchezo,hiyo ni ajira ya kiwanda sio bus,mtu mwenye biashara ya kawaida,hawezi kuwa na wafanyakazi 300.Wamezidi ni 10.
4:ndani ya miaka 6,kuwa matajiri wa kuajiri watu 300,huu ni uongo mkubwa.
5.Story ni ya kutungwa,sio ya kweli.
Tatizo lenu mnaishi kwa kukariri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana na pia shukrani kwa kushare nasi habari hii ya kuonyesha mapenzi ya kweli yapo bado Tanzania. Mapenzi ya kuanza kama maskini kabisa lakini mkapambana hadi kuweza kuajiri watu 300.

Warembo wengi siku hizi hupenda ready made njemba mwenye kila kitu, hivyo nawe ungekuwa hivyo penzi lenu lisingetokea maana ungempiga chini baada ya kugundua kwamba hana chochote.

Halafu nimependa pia msimamo wako wa kupambana na wazazi hadi wakakubali kuolewa na pia kubadili dini. Wakati nasoma hii nilidhani itaishia vibaya jamaa kakutelekeza baada ya kuwa tajiri lakini si hivyo bado mnaonyeshana mapenzi ya kweli katika ndoa yenu ya karibu miaka 10 sasa.


Ni adimu sana kusikia mapenzi ya kweli kama haya siku hizi, ni pesa tu yule hana pesa yule ana kibamia, yule ananuka mdomo, yule jamaa ni mshamba sana mimi wa MUJINI wapi na wapi na watu wa kuja. Mwenyezi Mungu awajaalie zaidi.
Mkuu nashukuru sana kwa kunitia moyo haikuwa rahisi lkn Upendo ulisimama kati yetu hatimaye tukaungana, tumekuwa msaada hata kwa wale waliotusema vbya
 
Yote nayajua , huwezi kuwa na ushauri mzuri zaidi niliopewa na wazazi wangu hayo mengine hata wewe utapitia

Sitakaa niyapitie hayo kwani siendi kuoa au kuolewa na mgalatia. Ndo maana hata babako akakuruhusu kwani alijua huna dini. Umeshaenda kwa huyo mgalatia, umeshakaa kwake sasa unamuomba babako ushauri ulitegemea akuambie uondoke huko??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom