Haya mambo ya Co - Parenting, Baby mama, Baby Daddy yanavuruga malezi, badala ya wazazi kulea mtoto, wanashindana kupata attention ya mtoto

Haya mambo ya Co - Parenting, Baby mama, Baby Daddy yanavuruga malezi, badala ya wazazi kulea mtoto, wanashindana kupata attention ya mtoto

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
2,686
Reaction score
8,170
Katika baadhi ya familia, baada ya wazazi kutengana au kutoshirikiana moja kwa moja katika ndoa, huibuka mifumo ya malezi kama co-parenting, au mtoto kubaki na mzazi mmoja huku mwingine akihusika kwa zamu au kwa mipango maalum ya kumlea mtoto.

Kwa mtazamo wa kitaalamu wa malezi, changamoto kubwa inayoweza kujitokeza si mfumo wenyewe wa malezi, bali namna wazazi wanavyousimamia.

Badala ya lengo kuu kuwa ni ustawi wa mtoto, wakati mwingine wazazi hujikuta wakiingia kwenye ushindani wa kihisia, kila mmoja akihangaika kupata upendo au “attention” ya mtoto. Hali hii inaweza kuathiri uthabiti wa malezi na kumuweka mtoto katikati ya mgawanyiko wa hisia.

Mtoto annaza kulelewa katika mazingira ya hofu ya kumkosea au kukwepa kuumiza hisia zake. hapa ndipo nidhamu na mafunzo muhimu ya maisha yanaweza kudhoofika.

Malezi bora yanahitaji uwiano kati ya upendo, mipaka, na maamuzi thabiti yenye lengo la kumjenga mtoto kimaadili na kisaikolojia.

Pia, migogoro kati ya wazazi ikiwemo mawasiliano yasiyo ya moja kwa moja huongeza ushindani zaidi kiasi cha kuanza kutoa taarifa hasi kuhusu mzazi mwingine, mtoto anaanza kudanganywa ili amchukie hasa baba yake, hii huweza kumchanganya mtoto na kuathiri mtazamo wake wa mahusiano na uaminifu.
 
Back
Top Bottom