Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Status
Not open for further replies.
Nani kakwambia Mungu wa wakristo ni Bwana Yesu..!?
Mkuu heshima kwako, kwa mtazamo wangu na baadhi ya wale niwasikiao miongoni mwa wakristo nimewasikia wakimwita yesu mwana wa mariam kuwa ni mungu, nami nikashawishika kutambua kuwa mungu wa wakristu ni Yesu.
Kumbe nimekosea, basi tafadhali kupitia jukwaa hili nifahamishe mimi na wale waliokuwa na mtizamo wa kimakosa kuhusu mungu halisi wa wakristu ni nani?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam wana MMU!

Najisikia kushare nanyi story ya mahusiano yangu maana ina mafunzo mengi ndani yake.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwanamke niliyelelewa kwenye familia ya watu wa imani na msimamo thabiti wa dini ya kiislam.

Baba na mama yangu ni swala tano hivyo hata sisi watoto tulijikuta tuna angukia huko huko!

Siku moja nikiwa natoka dar kwenda kuanza kazi mwanza nilibahati kukaa jirani na mkaka mmoja. Nikiwa nimevalia waswahili wanasema kininja.

Baada ya kuingia kwenye basi nilifika ktk siti yangu na kumsalimia jirani yangu ambaye siku hiyo nilikaaa naye siku nzima.

Yule kaka alikuwa mkristo lakin alikuwa ni mtu mstaarabu sana. Safari ilianza tukawa tunazungumza hili na lile ilimradi midomo isichache.

Tulipofika mwanza tulibadirishana namba za simu kisha kila mmoja akaelekea kwenye uelekeo wake.

Nilipenda utulivu wake na maongezi yake kwani yalikuwa ya staha na yaliyojaa hekima , pamoja na hilo ukarimu wake ulikuwa kivutio kikubwa kwangu kwani kila alichonunua njiani alininunulia nami pia.

Baada ya kuacha zilipita siku tatu ndipo akanitumia meseji ya kunisalimu Tuliendelea na mawasiliano kwa muda wa mwezi mmoja tukajikuta tume fall in love...

Kipindi nimekubali kuanza nae mahusiano sikujali habari ya tofauti za dini kwakuwa nilijua ilikuwa kwa muda tu., kumbe sikujua kuwa muonja asali huwa haonji Mara moja.

Tulianza mahusiano , nikajikuta nimezama mzima mzima, tukadumu miezi sita tukiwa kwenye penzi moto moto,, hakuna akiyetamani kuona mwenzie anakwenda mbali.

Ikafika kipindi tukakubaliana kufunga ndoa, yaani alinifanya niwe kipofu maana sikutaka kuona namkosa , na yeye hivyo hivyo,ingawa kila nilipokumbuka namna ya kuwaeleza wazazi nilihisi wangekuwa kikwazo.

Nikajitutumua na kuwaeleza , kwakweli haikuwa rahisi,nilipingwa na kila mtu nyumbani. Nilimpigia simu mpenzi wangu na kumueleza msimamo wa wazazi, nakumbuka aliniuliza swali moja tu..unanipenda kwa dhati nikajibu ndiyo ..akajibu nisiwe na hofu tutavuka pamoja.

Nyumbani wakanipa mashart kama nataka kuolewa na Alex (siyo jina halisi) basi nimwambie akubali kubadili dini.

Binafsi niliona isingekuwa rahisi mwanaume kubadiri dini kumfuata mwanamke hata hivyo pia sikuona vyema kuona my man anabadiri dini kwasababu yangu maana niliamini mm ndiye wa kumfuata.

Nikamwambia vile wazazi walivyosema..Alex alinijibu for the sake of our love nipo tayari kubadiri lkn mm sikuona vyema mwanaume kumfuata mwanamke hivyo nilimzuia asifanye hivyo aniache nipambane.

Nilitafuta muda nikaongea na baba kwa undani akanielewa na kumshawishi mama hatimaye tukaruhusiwa kufungua ndoa...

Nilikubali kubadiri dini kwaajili ya upendo nimkamfuata Alex ...tukafunga ndoa mwaka 2008 , maisha yakaendelea, sikuwa na shaka na upendo wa Alex kwangu.

Nakumbuka tulianza maisha tukiwa masikini sana Alex akiwa Mwalimu wa sekondari nami nikiwa mwalimu wa shule ya msingi.

Baada ya miaka mitatu Alex aliniomba aache kazi aingie kwenye biashara, nilipinga lkn baadae nikakubali.

Nakumbuka alianza na biashara ya Mbao toka mafinga , biashara ikakuwa akafungua duka kubwa la vifaaa vya ujenzi. Biashara ikawa kubwa sana kiasi cha kunilazimisha namimi kuacha kazi ili tusaidiene kusimamia.

Nashukuru Mungu tulikuza mtaji tukajikutana tunaingia kwenye biashara ya mabasi.

Wakati yote haya yanaendelea Alex alizidisha upendo kwangu , nilichofanya nikumtii na kumpenda zaidi, tulipendana na kudumu ktk upendo.

Mungu ametujalia watoto watatu sasa na tukiwa na biashara nyingi huku tumeajili zaidi ya watu 300.

Mpaka hivi naandika Upendo wangu na Alex unaongezeka kila kukicha

Nihitimishe kwa kusema Upendo wa kweli hauzuiliwi na chchte.

Wasalaam.
Amen. Nimepata mwanga

Ujana haubagui.[emoji53][emoji53]
 
Mungu ametujalia watoto watatu sasa na tukiwa na biashara nyingi huku tumeajili zaidi ya watu 300.

Mpaka hivi naandika Upendo wangu na Alex unaongezeka kila kukicha

Nihitimishe kwa kusema Upendo wa kweli hauzuiliwi na chchte.

Wasalaam.

So inspirational, All the blesses from The Almighty.
 
Ukristo sio dini ya kweli. Uislam sio dini ya kweli!

- wajali yatima na wajane.

- saidia wenye shida

- mpende jirani yako

Hakika, utakua umejiwekea nafasi mbinguni.

Lakini pia, hakuna haja ya kulazimishana kwenda peponi. Hakuna sababu ya Salma kufata yale unayoamini wewe!

Ninachofahamu mimi, kuna wakristo wataenda peponi na kuna wakristo watachomwa moto.

Kuna waislam wataenda peponi, na kuna waislamu watachomwa moto!

Love is meant to unite, religion is meant to devide!

With love, you can conquer the world!

Hongera dada Salma!
- KANA -
 
Unajuwa katika huu uzi wengi wenu mmeupeleka kiudini zaidi na hamjaelewa content nzima ya ujumbe uliopo kwenye huo ujumbe.

Mimi binafsi nimejifunza sana tena sana upendo ni wawatu wawili na pia kilichopangwa na mungu binadamu hawezi kukitenganisha ndio maana katika umbaji wake aliumba ME na KE kwa kumanisha hizi dini zimeletwa tu lakini tunavyozichukulia ndio zimesababisha ubaguzi mkubwa sana kwetu sisi binadamu na kijifanya kuzijuwa zaidi. Hivi ulishawai kujiuliza kipindi mungu anaumba binadamu aliumba huyu atakuwa muislamu na huyu mkristu?

Niwangapi wameolewa na waislamu dini 1 wananyanyasika kwenye ndoa tuache ubaguzi usio na maana na swala la kipato uwa gumu kwetu sisi kutokana na sisi wenyewe kuwa na mioyo migumu na uchoyo wetu wa kumludishia mungu sehemu yake mfano mkubwa historia ya kaini na abel ndio kisa ukifuatilia utajuwa ukimludishia mungu utapata zaidi hicho ulichokiludisha. Ombi langu dada salma mungu hazidi kuwabariki mala dufu na mwendelele na upendo huo huo kwani kwenye upendo amani na furaha ndipo baba wa mbinguni hufanya makao katika hiyo familia.
 
Napenda kweli member wenye. kuinogesha JF kama wewe umejiunga tarehe 5 august tarehe 10 ukatupia thread ikapata 11 reply Leo tarehe 16 august umetupia tena nyingine
Nakutakia membership njema hapa JF karibu sana
Wewe umekata tamaa nini Ahahahahha maana ni member toka 2015 Ahahahahh😀
 
Wengi humu ni wivu tuu umewajaa. Hongera sana napenda sana watu walio na positive attitude kama yako. Ndoa ni jinsi mnavyotaka iwe ww na mwenzio. Suala la dini nadhani ni complications tuu zisizo na msingi
 
Allah anasema atasamehe dhambi zote ila shirki(Yaani kumshirikisha mwenyezimungu kamwe hato samehe endapo mja atakufa nayo)..........
 
ngoja na mimi nikaze na mlutherani wangu.kumbe inawezekana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom