Nilivyovuka vikwazo vya kidini kutetea penzi

Status
Not open for further replies.
Wasalaam wana MMU!

Najisikia kushare nanyi story ya mahusiano yangu maana ina mafunzo mengi ndani yake.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwanamke niliyelelewa kwenye familia ya watu wa imani na msimamo thabiti wa dini ya kiislam.

Baba na mama yangu ni swala tano hivyo hata sisi watoto tulijikuta tuna angukia huko huko!

Siku moja nikiwa natoka dar kwenda kuanza kazi mwanza nilibahati kukaa jirani na mkaka mmoja. Nikiwa nimevalia waswahili wanasema kininja.

Baada ya kuingia kwenye basi nilifika ktk siti yangu na kumsalimia jirani yangu ambaye siku hiyo nilikaaa naye siku nzima.

Yule kaka alikuwa mkristo lakin alikuwa ni mtu mstaarabu sana. Safari ilianza tukawa tunazungumza hili na lile ilimradi midomo isichache.

Tulipofika mwanza tulibadirishana namba za simu kisha kila mmoja akaelekea kwenye uelekeo wake.

Nilipenda utulivu wake na maongezi yake kwani yalikuwa ya staha na yaliyojaa hekima , pamoja na hilo ukarimu wake ulikuwa kivutio kikubwa kwangu kwani kila alichonunua njiani alininunulia nami pia.

Baada ya kuacha zilipita siku tatu ndipo akanitumia meseji ya kunisalimu Tuliendelea na mawasiliano kwa muda wa mwezi mmoja tukajikuta tume fall in love...

Kipindi nimekubali kuanza nae mahusiano sikujali habari ya tofauti za dini kwakuwa nilijua ilikuwa kwa muda tu., kumbe sikujua kuwa muonja asali huwa haonji Mara moja.

Tulianza mahusiano , nikajikuta nimezama mzima mzima, tukadumu miezi sita tukiwa kwenye penzi moto moto,, hakuna akiyetamani kuona mwenzie anakwenda mbali.

Ikafika kipindi tukakubaliana kufunga ndoa, yaani alinifanya niwe kipofu maana sikutaka kuona namkosa , na yeye hivyo hivyo,ingawa kila nilipokumbuka namna ya kuwaeleza wazazi nilihisi wangekuwa kikwazo.

Nikajitutumua na kuwaeleza , kwakweli haikuwa rahisi,nilipingwa na kila mtu nyumbani. Nilimpigia simu mpenzi wangu na kumueleza msimamo wa wazazi, nakumbuka aliniuliza swali moja tu..unanipenda kwa dhati nikajibu ndiyo ..akajibu nisiwe na hofu tutavuka pamoja.

Nyumbani wakanipa mashart kama nataka kuolewa na Alex (siyo jina halisi) basi nimwambie akubali kubadili dini.

Binafsi niliona isingekuwa rahisi mwanaume kubadiri dini kumfuata mwanamke hata hivyo pia sikuona vyema kuona my man anabadiri dini kwasababu yangu maana niliamini mm ndiye wa kumfuata.

Nikamwambia vile wazazi walivyosema..Alex alinijibu for the sake of our love nipo tayari kubadiri lkn mm sikuona vyema mwanaume kumfuata mwanamke hivyo nilimzuia asifanye hivyo aniache nipambane.

Nilitafuta muda nikaongea na baba kwa undani akanielewa na kumshawishi mama hatimaye tukaruhusiwa kufungua ndoa...

Nilikubali kubadiri dini kwaajili ya upendo nimkamfuata Alex ...tukafunga ndoa mwaka 2008 , maisha yakaendelea, sikuwa na shaka na upendo wa Alex kwangu.

Nakumbuka tulianza maisha tukiwa masikini sana Alex akiwa Mwalimu wa sekondari nami nikiwa mwalimu wa shule ya msingi.

Baada ya miaka mitatu Alex aliniomba aache kazi aingie kwenye biashara, nilipinga lkn baadae nikakubali.

Nakumbuka alianza na biashara ya Mbao toka mafinga , biashara ikakuwa akafungua duka kubwa la vifaaa vya ujenzi. Biashara ikawa kubwa sana kiasi cha kunilazimisha namimi kuacha kazi ili tusaidiene kusimamia.

Nashukuru Mungu tulikuza mtaji tukajikutana tunaingia kwenye biashara ya mabasi.

Wakati yote haya yanaendelea Alex alizidisha upendo kwangu , nilichofanya nikumtii na kumpenda zaidi, tulipendana na kudumu ktk upendo.

Mungu ametujalia watoto watatu sasa na tukiwa na biashara nyingi huku tumeajili zaidi ya watu 300.

Mpaka hivi naandika Upendo wangu na Alex unaongezeka kila kukicha

Nihitimishe kwa kusema Upendo wa kweli hauzuiliwi na chchte.

Wasalaam.
Kwa hiyo toka 2008 ongeza miaka 3 ni 2011. Kwa hiyo toka mwaka 2011 mkaanza biashara ya mbao hadi mabasi na kuajiri watu 300!! Ni ndani ya miaka 6 tu!!! Mmefanikiwa sana, hebu Nipe siri ya kufanikiwa huko...kwa maana ya mtaji mlioanza nao na techniques zote hadi kufanikiwa hivyo...samahani lakini mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hesabu za haraka kutoka 2008 mpaka sasa ni kama miaka 9, nikitoa miaka 3 ya ualimu inabaki 6. Miaka 6 tu mmeuaga umaskin na kuajiri watu 300, si mchezo sijui mna kiwanda
acha kuhoji sana wewe
 
salma star UNASEMA ULIKAA SITI MOJA NA MKRISTO 'ILA ALIKUWA MSTAARABU'
INA MANA KWENYE UISLAMU MNAAMINISHWA WAKRISTO SYO WASTAARABU, WAKARIMU NA HAWANA STAHA? NA NI WATU WA KUWATENGA?

HONGERA KWA KUWA MKRISTO NA KUMPATA MWENZA UNAYEENDANA NAYE.

MAPENZI SYO DINI NA HAINA MAANA YOYOTE KUOKEWA NA MTU WA DINI YAKO WAKATI HAUNA FURAHA NAYE
 
Hakuna nisichokijua hata wewe ukitaka nikufundishe tafuta muda..kifupi Nina amani maina nipo kwenye mwanga zaidi
Ukisema hakuna usichojua hapo si kweli uislam dada ni mpana sana usije ukafikiri ni jambo dogo kama unavyofikiri.
Naomba nikukumbushe ya kuwa "HAIKUWA CHOCHOTE HII DUNIA BALI NI JAMBO LENYE KUPITA" kwa hiyo usihadaike na mapambo yake hadaa zake, mkumbuke mola wako aliyekuumba na akakupa wingi wa neema zisizo na idadi wa kipimo.
Labda nikuulize swali jengine
"Je umekubali kuuza akhera yako kwa ajili ya maisha mafupi yenye kupita?"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana na pia shukrani kwa kushare nasi habari hii ya kuonyesha mapenzi ya kweli yapo bado Tanzania. Mapenzi ya kuanza kama maskini kabisa lakini mkapambana hadi kuweza kuajiri watu 300.

Warembo wengi siku hizi hupenda ready made njemba mwenye kila kitu, hivyo nawe ungekuwa hivyo penzi lenu lisingetokea maana ungempiga chini baada ya kugundua kwamba hana chochote.

Halafu nimependa pia msimamo wako wa kupambana na wazazi hadi wakakubali kuolewa na pia kubadili dini. Wakati nasoma hii nilidhani itaishia vibaya jamaa kakutelekeza baada ya kuwa tajiri lakini si hivyo bado mnaonyeshana mapenzi ya kweli katika ndoa yenu ya karibu miaka 10 sasa.

Ni adimu sana kusikia mapenzi ya kweli kama haya siku hizi, ni pesa tu yule hana pesa yule ana kibamia, yule ananuka mdomo, yule jamaa ni mshamba sana mimi wa MUJINI wapi na wapi na watu wa kuja. Mwenyezi Mungu awajaalie zaidi.

Wasalaam wana MMU!

Najisikia kushare nanyi story ya mahusiano yangu maana ina mafunzo mengi ndani yake.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwanamke niliyelelewa kwenye familia ya watu wa imani na msimamo thabiti wa dini ya kiislam.

Baba na mama yangu ni swala tano hivyo hata sisi watoto tulijikuta tuna angukia huko huko!

Siku moja nikiwa natoka dar kwenda kuanza kazi mwanza nilibahati kukaa jirani na mkaka mmoja. Nikiwa nimevalia waswahili wanasema kininja.

Baada ya kuingia kwenye basi nilifika ktk siti yangu na kumsalimia jirani yangu ambaye siku hiyo nilikaaa naye siku nzima.

Yule kaka alikuwa mkristo lakin alikuwa ni mtu mstaarabu sana. Safari ilianza tukawa tunazungumza hili na lile ilimradi midomo isichache.

Tulipofika mwanza tulibadirishana namba za simu kisha kila mmoja akaelekea kwenye uelekeo wake.

Nilipenda utulivu wake na maongezi yake kwani yalikuwa ya staha na yaliyojaa hekima , pamoja na hilo ukarimu wake ulikuwa kivutio kikubwa kwangu kwani kila alichonunua njiani alininunulia nami pia.

Baada ya kuacha zilipita siku tatu ndipo akanitumia meseji ya kunisalimu Tuliendelea na mawasiliano kwa muda wa mwezi mmoja tukajikuta tume fall in love...

Kipindi nimekubali kuanza nae mahusiano sikujali habari ya tofauti za dini kwakuwa nilijua ilikuwa kwa muda tu., kumbe sikujua kuwa muonja asali huwa haonji Mara moja.

Tulianza mahusiano , nikajikuta nimezama mzima mzima, tukadumu miezi sita tukiwa kwenye penzi moto moto,, hakuna akiyetamani kuona mwenzie anakwenda mbali.

Ikafika kipindi tukakubaliana kufunga ndoa, yaani alinifanya niwe kipofu maana sikutaka kuona namkosa , na yeye hivyo hivyo,ingawa kila nilipokumbuka namna ya kuwaeleza wazazi nilihisi wangekuwa kikwazo.

Nikajitutumua na kuwaeleza , kwakweli haikuwa rahisi,nilipingwa na kila mtu nyumbani. Nilimpigia simu mpenzi wangu na kumueleza msimamo wa wazazi, nakumbuka aliniuliza swali moja tu..unanipenda kwa dhati nikajibu ndiyo ..akajibu nisiwe na hofu tutavuka pamoja.

Nyumbani wakanipa mashart kama nataka kuolewa na Alex (siyo jina halisi) basi nimwambie akubali kubadili dini.

Binafsi niliona isingekuwa rahisi mwanaume kubadiri dini kumfuata mwanamke hata hivyo pia sikuona vyema kuona my man anabadiri dini kwasababu yangu maana niliamini mm ndiye wa kumfuata.

Nikamwambia vile wazazi walivyosema..Alex alinijibu for the sake of our love nipo tayari kubadiri lkn mm sikuona vyema mwanaume kumfuata mwanamke hivyo nilimzuia asifanye hivyo aniache nipambane.

Nilitafuta muda nikaongea na baba kwa undani akanielewa na kumshawishi mama hatimaye tukaruhusiwa kufungua ndoa...

Nilikubali kubadiri dini kwaajili ya upendo nimkamfuata Alex ...tukafunga ndoa mwaka 2008 , maisha yakaendelea, sikuwa na shaka na upendo wa Alex kwangu.

Nakumbuka tulianza maisha tukiwa masikini sana Alex akiwa Mwalimu wa sekondari nami nikiwa mwalimu wa shule ya msingi.

Baada ya miaka mitatu Alex aliniomba aache kazi aingie kwenye biashara, nilipinga lkn baadae nikakubali.

Nakumbuka alianza na biashara ya Mbao toka mafinga , biashara ikakuwa akafungua duka kubwa la vifaaa vya ujenzi. Biashara ikawa kubwa sana kiasi cha kunilazimisha namimi kuacha kazi ili tusaidiene kusimamia.

Nashukuru Mungu tulikuza mtaji tukajikutana tunaingia kwenye biashara ya mabasi.

Wakati yote haya yanaendelea Alex alizidisha upendo kwangu , nilichofanya nikumtii na kumpenda zaidi, tulipendana na kudumu ktk upendo.

Mungu ametujalia watoto watatu sasa na tukiwa na biashara nyingi huku tumeajili zaidi ya watu 300.

Mpaka hivi naandika Upendo wangu na Alex unaongezeka kila kukicha

Nihitimishe kwa kusema Upendo wa kweli hauzuiliwi na chchte.

Wasalaam.
 
njiwa KWANI WEWE UNA UHAKIKA KUWA UTAIONA PEPO? UMETENDA DHAMBI NGAPI HAPA DUNIANI MPAKA UNAMHUKUMU MTU ALIYEBADILI DINI?

KUBADILI DINI SIYO KUMBADILI MUNGU, MUNGU NI MMOJA TU NA DINI NI NJIA TU YA MAWASILIANO KATI YA BINADAMU NA MUNGU.. HVYO KUITWA MUISLAMU HUKU UKITENDA DHAMBI HAIKUONDOLEI ADHA YA MOTO HUKO JEHANAMU.. KABLA YA KUMHUKUMU MWENZAKO JIHAKIKISHE KUWA WEWE NI MSAFI KWA 100%

ALIYERITHI DINI NI MPUMBAVU KULINGANISHA NA MTU ALIYEINGIA KATKA DINI AKIWA NA AKILI ZAKE TIMAMU.
 
Swala ka Dini Ni mmoja ya maswala yanayo haribu Maisha ya watu kuna watu wana chelewa kuoa na kuolewa na kujikuta hawaolewi na kuoa kabisa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom