Rogie
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 7,601
- 6,723
Share experience yako....,
Uliniumiza i wish ungejua
Nilikuumiza na nini H.O.E? Pole
Share experience yako....,
Uliniumiza i wish ungejua
Habari zenu wanaJF,
Nimeamu kuwa member baada ya kuwa nasoma tu kila siku, hii ni kutaka kushare na nyinyi angalau naweza kupata ushauri. Huyu dada nilikua nae kwenye mahusiano kwa miaka mitatu sasa. Ule mwaka wa mwanzo alikua hayupo active sana, ila baadae akaonyesha kunikubali sana tukawa tunaishi kama wapenzi, ingawa kutokana na kusoma mimi nikahamia mkoani kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu yeye nikamuacha kule mkoa wa nyumbani.
Alionyesha kunijali, wivu mwingi, na pia alitii kila nililokua namwambia. Mara nyingi alikua akipanda gari na kuja huku mkoani kwangu na tulikua tukifanya mengi. Nilimtambulisha nyumbani wakamkubali kutokana na nidhamu yake ya hali ya juu aliyokua akionekana nayo. Mwisho nikaamua kupeleka barua, akanikubalia ila hapa ndipo akaanza kunizungusha. Akidai kuwa watu wa kwao wamemwambia asubiri kwanza!! Basi akazungusha sana kama miezi mi4 hivi.
Mmoja kati ya watu wa nyumbani akaja akanitonya siku hiyo kuwa hyo demu wako nasikia anaolewa..nikamjibu haiwezekani, akajitahidi kunithibitishia kuwa habari zile ni sahihi na zinatoka kwao haswa mimi nikabisha. Na nilikuwa na kila sababu ya kubisha sababu wakati naelezwa maneno haya huyu demu alikua kifuani kwangu na hiyo ni siku ya 3 tangu aje. Nikamuuliza vzri akacheka sana na kunambia hakuna ktu kama hcho, ww ndo mume wangu.
Naomba nifupishe hii story ila naamini mtanielewa maana nashindwa kuandika kila ktu hapa. Sikuwa na taarifa, nilikaa nikiamini kuwa yeye ni wangu tu. Nilipata likizo, nikawa niko nae sana kule nyumbani. Usilolijua ni sawa na usiku wa giza tu. Kumbe wakati mimi naanza likizo yeye alikua amebakiza siku 20 kabla ya ndoa.
Basi tukaendelea mpaka ilipobaki wiki moja kabla ya harusi, akiamini kuwa anaenda kuwekwa ndani na sitomuona tena, ndio hapo aliponambia anaenda Dar kwa matibabu. Nikaitikia na kumuombea Mungu sana apone haraka. Basi tukaendelea kuwasiliana na kupeana moyo, akawa ananipa updates za hosptali, mara ndo naingia kwa dakitari, mara nesi kaja, mara subiri kidogo nawekewa drip, nk.
Mimi dua zote kwake huku namaliza status zangu za pole kwenye Whatsapp kumbe ndugu yake mmoja ambaye anaujua ukweli na aliambiwa jinsi ninavyodanganywa anatizama halafu anacheka tu. Mamayangu naye kila siku anapiga simu kumpa pole huyu msichana na bila aibu anaitikia na kuzidi kumdanganya. Watu wote nyumba nzima wanamuombea dua apone haraka ili barua ipelekwe. Kimbembe kilikuja Jumanne ambayo Ijumaa yake ndo ilikua harusi.
Hiyo jumanne ilikuja kadi ya mwaliko wa harusi. Sikuwepo, ikasomwa pale na nikasubiriwa kwa hamu, wakaja wakanionyesha, sikuamini nikampigia simu mbele yao na kuweka loudspeaker, nilipomuuliza kuhusu harusi akakata simu na hakupokea tena usiku ule. Sikuweza kulala. Asubuhi akanitext na kunieleza maneno mengi kuwa amelazimishwa. Mimi nikawa namuitikia tu, nikajaribu kufuatilia kwa kina sana nikajua ni pesa ilihusika, jamaa alikuja nyuma yangu akalipa milions nyingi sana, ila huyu demu akakosa cha kunidanganyia, akaona aendelee kunifanya zoba tu.
Na kipindi hiki cha harusi (ambaye yeye alikifanya cha ugonjwa) alinipiga vizinga sana, yaani zaidi ya laki nne ndani ya wiki moja. Nadhni ndo aliamua kunikamua kwa mara ya mwisho. Hadi siku ya harusi bado alikua ananipigia simu, mimi nikamwambia leo unaolewa concentrate kwenye ndoa yako, mimi niache. Lakini alkua hakubali sababu pamoja na ujinga wake huu alioufanya alikua akinifahamu vzuri kuhusu maamuzi yangu.
Mungu mkubwa, kipindi kile cha hasira nilipata counselling kubwa sana kutoka kwa wazee, sikufanya maamuzi magumu. Mama yangu nlimshuhudia akitoa chozi kwa kudanganywa na mtoto mdogo, ila nikampoza na kumuomba msamaha. Licha ya kuwa alibadilishiwa namba na mumewe lakini still alintafuta na namba yake mpya ninayo. Bado mpka sasa natafuta cha
kumfanya huyuhanithi, baradhuli kwa sababu kuu hizi:
1. Kwanini alipoona mimi simfai asingenambia mapema tu kuliko hivi alivyofanya?!
2. Kwanini afikie hatua hadi amdanganye mtu ninayemuheshimu zaidi hapa ulimwenguni (mama) ambaye hata mimi mwenyew sijawahi kumdanganya.
3. Hii wiki moja kabla ya kuolewa alikuwa akiwaambia ndugu zake kuwa huyu jamaa sitamsahau ngoja nimle vyake vya mwisho mwisho maana akili zake za kilevi sana. Sielewi alikua na lengo gani hapa.
4. Kama alijua anao wa kumpa vingi na vya kumtosheleza, kwanini achkue vyangu vichache?
Kwakweli ndugu zangu hili jambo naweza nikalieleza simpo sana hapa, lakini liliniuma kwa zaidi ya mwezi mzma sikuwa normal semesta ya jambo hili ndo semesta nlifanya vibaya zaidi kulko zote. Anywayz, now niko normal na akili imetulia, na inaniambia lazima nilipe kisasi. Natamani na yeye ajutie one day ! Sababu sijaona mantiki ya kufanya hivi.
Kabla sijaamua, ndugu zangu, hebu tupeane ushauri. Maana kila ninavyojitahidi kusahau naona kama nimefanywa zoba sana afu akili yangu haitaki.
Natanguliza shukrani
Hizi comments za JF zimenifanya nisifikirie kabisa kulipa kisasi..nimeshafuta hilo wazo.
Forgive and forget
Mimi nataka nimroge akose ndoa yake afu arudi kwangu na mimi nimkatae.. Ili ajue uchungu ulivyo
Mahaba nivunje shingo, nipige sindano ya ganzi. Lol
On Serious Mode:
Mkuu let it go ili nafsi iwe nyepesi. Kuumizwa kupo....just kno urn't alone. 80% of us humu tumewahi umizwa in one way or another. Kuna watu nimewahi hadithiwa wameshaumizwa vibayaa sana in a way ingekua me or u tungeishia kujiua. Lakini wame recover nd got over it. Kuhudhuria nyumba za ibada ni muhimu nd dnt overeact u may worsen the situation. You still have a great life ahead of you. Cha kufanya ni kumlia ganzi tu nd keep ur distance kuna siku yatamkuta makubwa atajifunza na roho yake.
Kikubwa mshukuru Mungu huwez jua kakuepushia nn. Ulitaka kuoa muuaji.
Ukiwa katika mahusiano ya kimapenzi na mtu au ukiwa umeolewa/kuoa...lazima na jitahidi sana kupanua moyo wako...yaan moyo wako uwe kama jalala...hapo utayashinda mengi.