YANGU NI HAYA YAFUATAYO>
1. Hongera kwa kuleta ili jambo hapa JF maana tayari umshatua mzigo kwa 90% uliokuwa ukikusumbua moyoni na akili.
2. Wapo wengi waliopitia mitihani mikubwa ya maisha kuliko hayo yako lakni Mungu amewapa ujasiri waliyasahau and life go on....wana ndoa zenye furaha na Amani tele.
3. Huyo sio wako aliyekupangia Mungu......wako Yulee...nimepishana nae pale anakuja...TULIA..MUNGU ATAKUPA WAKO..mtakaye...endana vema...na hata hivyo mshukuru Mungu amekuepusha na huyo mwanamke...!
4. Usije ukalipa KISASI....MUNGU ATAMLIPA...NA IPO SIKU ATAKUJA KULIA MACHOZI MBELE YAKO akikuomba msamaha.
5. Mfariji mama ...mwambie ULITELEZA TU...IPO SIKU...atafurahia kushuhudia NDOA YAKO NA WAJUKUU.
NB: Usilipe kisasi, mpotezeee, namba yake...m-block ili asizidi kukutia stress...usitafute binti haraka..TULIA ...wako anakuja.
well said, espcl.number 4. Ache wasiliana nae... ignore her and 1 day atarud omba radhi kwa magoti
wanawake wazuri na wenye tabia nzuri wapo wengi tu, we maliza masomo, utafute pesa ujijenge , baada ya hapo unachukua tu watoto wengi mbona hata virgin wapo. ishu ni kujipanga.
kama wazazi wake walikuwa na njaa na wanajua mahari inayotolewa itatosha mtaji kwa familia nzima kwa nini wasikubali?kwa mmoja akifa watazikwa pamoja?haya ni mapenzi tu.
Mpaka sasa naongea nae kwa upole sana, natamani ajue jinsi ninavyomchukia moyoni, lakin naona kama itaniharibia mipango yangu.
Nianze kwa kukupa pole mkuu,ninaona jinsi gani ulivyoumia haswa ukizingatia muda mwingi uliopoteza kwake...katika mahusiano kinachouma ni kupoteza muda ambapo mliweka malengo na siyo vitu vya thamani au mali...
Katika mambo ambayo unatakiwa ushukuru kwa MUNGU ni hilo kumjua mtu wako kwa undani kuwa ni asiye na msimamo na mpenda mali,na dhambi ya usaliti huwa haiishi,huyo mwanamke atakuja kumuumiza huyo jamaa aliyetoa mamilioni ili kumuoa na huyo mwanamke atakuja kuumizwa mahali ambapo atakuwa amependa sana,hii ndo misingi ya malipo ya hapa hapa dunian ilivyo,wapo kwenye furaha ya muda tu...
mwisho niseme "the best revenge is a massive success"
naelewa vyema hisia zako, nilikutwa na kilichokukuta last year January tofauti ni kuwa sikupewa taarifa ama mwaliko, ni jambo gumu mno asee. hata useme vipi najua moyo wako una maumivu makali mno. maana yalinikumba. binafsi nilichukua mwaka mzima kukubali na kusahau. mwombe Mungu akupe nguvu na uvumilivu. jiweke busy sana na mambo mengine, huna haja ya kuendelea na mawasiliano katiza pia. uaiwaze kulipiza kisasi achana nae chukulia kuwa amefariki.
Nianze kwa kukupa pole mkuu,ninaona jinsi gani ulivyoumia haswa ukizingatia muda mwingi uliopoteza kwake...katika mahusiano kinachouma ni kupoteza muda ambapo mliweka malengo na siyo vitu vya thamani au mali...
Katika mambo ambayo unatakiwa ushukuru kwa MUNGU ni hilo kumjua mtu wako kwa undani kuwa ni asiye na msimamo na mpenda mali,na dhambi ya usaliti huwa haiishi,huyo mwanamke atakuja kumuumiza huyo jamaa aliyetoa mamilioni ili kumuoa na huyo mwanamke atakuja kuumizwa mahali ambapo atakuwa amependa sana,hii ndo misingi ya malipo ya hapa hapa dunian ilivyo,wapo kwenye furaha ya muda tu...
mwisho niseme "the best revenge is a massive success"
Kwenye sentensi yako ya mwisho kabisaa nakubaliana na ww 1000%.
Ungekua mnywaji ningekupiga beer creti. Lol
It is what it is. Kuna watu nlisoma nao high school walikua dharau sanaa, leo choka mbayaaa wengine mateja saa hvi, wanasujudu sanaa tu. Maishani nimejifunza sanaa kuheshimu kila mtu, naongea na kucheka na yoyote hata watoto ili mradi adabu iwepo.
Upo sawa mkuu kuumizwa kupo
Duuuh hii Dunia ili ukomae ki Iman vizuri vitu kama hivi vipo,bila matatizo utajifunzaje....?? Shukuru Mungu limetokea mapema,UMEJIFUNZA.....Hao kuna msemo waswahili hisema jina la mwanamke ni TENDA WEMA NENDA ZAKO....Hawa watu ni Hatari sana,pôle sana......!!