Nikiwa kama msomi ninayefanya biashara nimeona wazi kwamba biashara inahitaji elimu ndogo hata ya darasa la 4 inatosha

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Nikiri wazi kwa sasa bado nipo kwenye ajira serikalini lakini biashara ndio inaniingizia mkwanja zaidi kuzidi ajira, kwenye ajira nachofaidika ni connections na sehemu nilipo kwenye ajira inanipa nguvu ya mamlaka flani kwenye sytem lakini kuhusu mkwanja kiukweli biashara ndio inanibeba zaidi.

Hadi sasa katika biashara yangu husika inayo deal na mambo ya maintanance za magari nimekutana na watu kibao ambao wengine wameishia hata form 4 lakini wanapiga mshinda viibaya mno na mimi kwa vile nipo kwenye biashara hii sijaona uhusiano wa elimu na biashara hii.

Kwa uzoefu wangu nilionao ni kwamba kwenye biashara silaha kuu ni kuwa na wateja.

Elimu inayohitajika zaidi kwenye biashara ni hesabu za kawaida kabisa za kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya. hizi ndio zitakusaidia kutoa chenchi, kuhesabu stock, kujua madeni, n.k.

Pia kwakuwa mali bila daftari hupotea basi ni vema uwe na daftari la mau ya cash, mauzo kwa mkopo (kama unakopa) na stock.

Kwenye suala la mambo ya sheria za serikali mamb yanazoeleka kabisa leseni utaenda jiji utapewa, tra utalipia kodi yao kadri ya makadirio yao (hapa huwa wanatumika vishoka ili ukadiriwe chini, ukileta ujuaji utajuta), n.k.

Biashara ni ngumu mara ya kwanza kama vile mtu asiejua kuendesha gari, mwanzani atakuwa anafanya makosa teana hata barabarani anaendesha kwa mikono miwili huku akiwa very attentive hata kwa mkao wake utamjua tu, lakini kadri muda unaenda anakuwa mzoefu ambae anaendesha kwa mkono moja tu huku amerelax na kashakitupa kinembo kile cha learner, changamoto alizopitia hata gari izimike msituni ataitengeneza ama kuwa na connections za mafundi warekebishe.
 
Kwa hiyo watoto wetu wasisome?
Watoto wasome kwa faida yao hasa katika professions wanazozitaka lakini kusea kwamba mtoto asome ili awapiku wafanyabiashara wengine wenye elimu za kawaida hio toa kichwani.

Biashara ni kama ngoma, ingia ndani ujipime na upate uzoefu kwa kucheza,
 
Upo sahihi sana. Mimi wakati naanza kujifinza kuendesha pikipiki ilibaki kidogo nikate tamaa na ile hali ya kunizimia mara kwa mara.

Ila kwa sasa naenjoy sana yaani naona nimechelewa sana kujua kuendesha pikipiki.
 
Upo sahihi sana. Mimi wakati naanza kujifinza kuendesha pikipiki ilibaki kidogo nikate tamaa na ile hali ya kunizimia mara kwa mara.

Ila kwa sasa naenjoy sana yaani naona nimechelewa sana kujua kuendesha pikipiki.
Mwanzo ndo uko ivo na uoga unakuwa nao mwingi ila ukishazoea wai imeisha iyo.ni nature ya kujifunza kitu kigeni
 
Back
Top Bottom