Case Study: Kama kwenu hakuna wafanyabiashara, komaa na shule, Biashara iwe ni Plan B, Usiige wengine bila kufikiria hali ya kwenu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
kwenye familia / ndudu zako wa karibu kukiwa na watu waliofanikiwa kwa kufanya biashara inakuwa rahisi kwa wengine kuingia kwenye biashara tofauti na wale wasio na familia au ndugu walifanikiwa kibiashara, sisemi kuwa Huwezi kufanikiwa kabisa bila kuwa na historia ya biashara kwenye familia yenu, ila chance of failure ni kubwa, so make it plan B

Kwenu ni kule ambako una ukaribu nako iwe ni familia, ndugu ama ukoo. ukitaka kupajua kwenu angalia watu mnaokutana nje ya misiba na sherehe kufanya vikao vya kimaendeleo.

Ukiona huko kwenu hakuna damu ya kufanya biashara, wanaozifanya wana hali mbaya kiuchumi, hawasogei, n.k. ni jibu tosha kabisa hata ukitaka kuja kufanya biashra hao ndio watakuwa mentors wako nao watakuunga kwenye hio chain mtafanana, Ni heri angalau ukomae na shule ujaribu bahati yako kwenye ajira husika, ikishindikana ingia kwenye biashara kama Plan B.

Mfano mdogo wakinga nimeishi nao huku Iringa na Mbeya, ni kabila la 3 kwa biashara hapa nchini nyuma ya wachaga na wapemba, Na ni Mbeya hapo hapo kuna wanyakyusa lakini unaona wazi kabisa wanyakyusa hawana damu ya biashara ndio maana wanaaswa sana wasome na ukiangalia elimu imewabeba sana wana mgao wao mzuri tu kwenye ofisi na vitengo vya serikali, lakini kwa wakinga ambao kiukweli hata shuleni wanasua sua hawana presha sana hata wakifeli au wakimaliza shule wana channel ya kushikwa mkono kuanza kufundishwa biashara, mitaji, connections, n.k.

Kwa Arusha nimewahi kuishi kuna jamii za wameru, waarusha na wachaga, Japo kuwa wameru na waarusha wana mwamko mdogo kwenye elimu lakini nimeweza kuwaona waliothubutu kwa sasa wana kazi zao na mishahara si haba na wengine wameongezea biashara ila kwa walioacha shule wanapata msaada kidogo kibiashara huko makwao kwasababu kuna mwamko mdogo wa biashara, wengi huishia kuwa boda boda. lakini kwa upande wa wachaga hata kwa wale wanaoacha shule wakirudi huko kwao wanapata channel ya kupata pa kuanzia kwenye biashara kwa kufunzwa, kupewa mtaji, n.k. uzuri hawa ni kila mwaka huwa wanakutana huko vijijini kwao na wanapeana motisha za maendeleo kiasi kwamba hata nyumba za nyasi zimekuwa historia.
 
N.B: Walengwa ni wale wanaoweza kusomeshwa shuleni na sio kulazimika kufanya biashara sababu ya kukosa ada.

Wakuanzisha circle ya wafanya biashara lazima hapatikane tu. Hata hao waliona na wanafamilia wafanyabiashara at some point hawakuwa nao.
 
Kuna substance katika hii hoja. Usijidanganye kuwa utatoboa kirahisi kwa kufanya biashara ukaacha kutilia maanani mambo ya shule. Biashara ina dynamics nyingi tu, ikiwa ni hizo connection, mitaji, mentorship n.k. Anachosema mtoa mada ni kuwa kwenye familia yenu kukiwa na watu waliofanikiwa kwakufanya biashara, inakuwa rahisi sana kwako kufanikiwa. Hasemi kuwa Huwezi kufanikiwa kabisa bila kuwa na historia ya biashara kwenye familia yenu, ila chance of failure ni kubwa, so make it plan B. Mimi nimemuelewa
 
kwa hali ya sasa ajira zilivyozakuminyana unadhani asemacho bwana mkubwa bado ni valid?
Si ndo hapo... siku hizi elimu ni sehemu ya kuondoa ujinga na kupata connection. Ukisoma kutegemea ajira ukifika duniani utapata sonona.
Bora hata ukiwa binti, utakaa nyumbani bila masimango au unaweza kuolewa. Ukiwa kijana wa kiume ukikaa nyumbani tu utasimangwa mpaka utafute pa kwenda
 
Kwa hyo wakinga ni wa tatu baada ya wapemba na wachaga? 🤔 Nlitaka niandike ila baada ya kusoma hapa nimeishiwa stimu ya kutype
Wakinga biashara zao no uchuuzi sana sana, nje ya hapo huwapati kwenye stocks, aviation, exports, n.k. na hata hapo kariakoo don wake ni mchaga
 
Wachaga kariakoo wanamiliki magorofa mengi sana na pia wanafanya biashara eq kina mushi, chuwa, lamwai..... Wakinga wapo wengi pia lkn hao wapemba wanafanya biashara gani
 
Back
Top Bottom