Sihitaji mahubiri kwenye comment yangu!hauoni upande wa pili kama jamaa nae amewekeza vitu vingi kuhusu huyo mwanamke kwa kutegemea wataanzisha familia pamoja kumbe kawekeza kwa mwanamke malaya!?umevaa viatu vya huyo jamaa lkn?
sio mahubiri kiongzo ni uhalisia wa Maisha,take it or leave it.
kwa hiyo wewe kwa ushauri wako unataka jamaa aje ampige mimba huyo binti asepe,kisa kawekeza kwa binti?
huo ndo ushauri pekee uliona nao mpaka sasa wa kuwapa wanaume wenzako wote wanaopitia hali kama ya mchumba wa mleta mada?
unadhani akifanya hivyo ndo kamkomoa?namna gani kiumbe kitakachozaliwa ndo kilichomtuma huyo binti afanye huo ujinga?kilikuwepo wakati nyie mnawezekezeana na kusalitiana?
naamini kuna njia nyingi sana za busara kutatua hii ishu lakini sio ya kumpachika mimba binti na kusepa,yaani kufanya hivyo ni kukosa utu kabisa,ukatili wa hali ya juu na Zaidi kabisa kutenda kijinga bila kufikiri na kujiongezea dhambi juu ambayo itakutafuna Maisha yako yote kwa kutelekeza kiumbe ambacho hakina hatia
na mind you this mkuu,kuna dhambi na matendo ambayo tukiyafanya yanaweza kuturudia sisi moja kwa moja,lakini yapo yale ambayo tunayafanya sisi lakini yanakuja kuwaathiri watoto wetu hapo baadae,hakuna kitu kinamuuma mzazi kama kuona mtoto wake akiteseka,kuonewa,kudharaurika au kutendewa kikatili kwa namna yoyote.Usiombe ukakutana na hali kama hizo.
Take Care Kiongozi,usimfanye mjinga mmoja akakufanya wewe utende bila kufikiri na kujiingiza kwenye hatia nzito.