Mkanganyiko na sio kidogo Mkuu, ni watu wengi ikiwemo hata mimi kwa kipindi kirefu niliamini kwamba Lucifer ina muwakilisha IBILISI, Lakini baada ya kupitia maandiko mbalimbali na maelezo mengi ya namna kuisoma Biblia na Kuelewa ndiyo nilipoweza nami kupata ufahamu wa kwamba kumbe ni makosa ya kifasiri tu,Chanzo cha Mkanganyiko ni maandiko yaliyomo kwenye Kitabu cha Isaya 14:12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! (KJV)
Kweli Ibilisi ndiye Nyota ya asubuhi ?
Tukiyachunguza maandiko vizuri tutaona kwenye ufunuo 22:16 ''Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi''
Hivyo Bwana Yesu Mwenyewe alijitambulisha kwamba yeye ndiye Nyota yenye Kung'aa ya asubuhi.
Yapo maandiko mengine ambayo yanathibitisha kwamba Yesu Kristo ndiye Nyota ya asubuhi.
2 Petro 1:19 19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Ufunuo wa Yohana 2:28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.
Ni wazi kwamba Nyota ya asubuhi ni sifa ambayo ni ya kipekee kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kamwe haiwezi kuwa ni sifa ya Shetani/Ibilisi.
Kiini cha mkanganyiko.
Mkanganyiko umetokana na maelezo yanayopatikana katika tafsiri ya Biblia ya KJV Isaya 14:12 (Hasa katika Kiingereza ambapo limetumike neno LUCIFER) kama ilivyoelezwa hapo juu, Neno Lucifer limetumika kama utambulisho wa nyota ya asubuhi,ikiwa ni katika maelezo ambayo ukiyasoma kwa haraka unaweza fikiri yanamzungumzia IBILISI na kumpa sifa ya Nyota ya asubuhi. Hasa ukisoma Isaya14:12 kama ulivyo.
Isaya 14:12-15
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Ukiisoma maandiko haya kwa makini utagundua si kweli kwamba shetani anapewa sifa na ukuu wa kwamba yeye ni Nyota ya Asubuhi bali ni lugha ya ''Kebehi'' dhidi ya majikwezo ya IBILISI,na kujipa sifa kwamba yeye ni LUCIFER (Nyota ya Asubuhi) na inaonyesha jinsi ambavyo kujikweza kwake kumedhiriwa hadi kushushwa chini mpaka kuzimu,wakati alijinasibu kuwa yeye atapaa kupita vipimo vya mawingu na kuwa sawa na aliye juu!
Ukitambua kwamba Lugha ilikuwa si kumsifia Ibilisi bali kubeza kujikweza kwake na kujipa sifa asizokuwa nazo utagundua kwamba bado matumizi ya neno LUCIFER kwamba ni Ibilisi yanakinzana na ukweli, kwamba alijiita LUCIFER kujikweza tu,lakini kiukweli hana sifa hizo hata chembe.