Niijuavyo Freemasonry

Niijuavyo Freemasonry

mtoa mada umefafanua vizuri lakini ni lazima ufanye acknowledgement katika sources za information zako, ila unaposema hayo ni mawazo yako huru huo ni uongo wa wazi kabisa kama ufanywao na kikundi cha waasi cha UKAWA.

Naomba kuwasilisha
 
Kuhusu namba 666,wala usiwe na hofu maana haita kudhuru wewe wala ndugu yako,na sio namba ya madhara ndo mana huwa nadema hapa kila siku kuwa watu wanatafsiri visivyo mambo haya.,kuna vitu vingine haviepukiki tayar vipo na vingine vingi huvijui,lakini pia unatakiwa kujua kwamba hofu yako haitasaidia kitu maana huna haja ya kuwa na hofu.hakuna baya zaidi ya mema na usiogope mambo ya watu.karibu

Sio kweli hii namba ina madhara tena makubwa katika imani za watu wengine na hata katika mfumo wa maisha yetu ya kawaida,na ndiyo maana umekataa kuthibitisha kama ni namba au alama mojawapo inayotumika na hawa unaowazungumzia kila ninapokuuliza

Pia kafara za watu wanatoa ila sijui inakuaje watu wanasahau haraka haya matukio ya kafara za hawa jamaa.Ni vitu ambavyo viko wazi katika maisha yetu ya kila siku. So mleta uzi usiseme hawatoi kafara za binadamu. Hawa wako makini sana ndiyo maana huwezi sikia wanatoa kafara watoto wao la hasha ila kwa kutoa kafara za watoto wa wengine ndiyo namba moja.

Pia ndiyo hao walio namba moja kutoa kafara za member yoyote atakaye kiuka masharti yao.Hapa sasa hawaangalii sura wala cheo. Uwe king,princess,prince,raisi,jenerali wa majeshi,mwanamuziki lazima wakuondoe tu.

Kuwatetea hawa ni kama kujaribu radha ya sumu kwa kuionja
 
Eiyer,


Salaam na heshima mbele.
Kwenye bold, nadhani kuna walakini. Nyota zinajitegemea mwanga wake na hata uwepo. Kwa rejea ya awali, Jamii Intelligence kuna mada ihusianayo na nyota - "Ufahamu Kuhusu Nyota za Angani" ya 27/03/14 hususani bandiko za Kifyatu. Sijajua kuweka link wala mention.
 
Asante mkuu kwa kuwadadavulia,japo nilijua nikiandika kwamb masonic imeanza tangu wakati wa mfalme solomon watu wataelewa.thax alot


Kaka salaam.
Umetumia nguvu kubwa sana kutushawishi kwamba umeyatoa mawazoni mwako hayo maelezo na kwamba hujafanya rejea yoyote, si kitabuni wala mawazoni mwa wengine. Huyo mwingine kaonyesha vizuri uhusiano na Suleiman (Hiram Abiff?) na katambua alipoitoa.

Kwanini unasisitiza ni mawazo yako?
Hilo neno Freemasons/Masonic si umesoma mahali?
Haitapunguza umuhimu wa mada wala kukushusha hadhi kusema umetoa wapi mawazo yako ama nini kimekufanya ukafikiria yote hayo. Zaidi itakoleza ladha ya mjadala. Hata mifano unayotoa haishawishi kwamba umewaza tu!
 
mtoa mada umefafanua vizuri lakini ni lazima ufanye acknowledgement katika sources za information zako, ila unaposema hayo ni mawazo yako huru huo ni uongo wa wazi kabisa kama ufanywao na kikundi cha waasi cha UKAWA.

Naomba kuwasilisha

Kwa nn huamini kama ni mawazo yangu??basi amini
 
COCKINGTON,

Tatizo ni uthibitisho wa yale uyasemayo.Utoaji kafara ya watu sio msingi wa masonic na sio kwamba kila afa linapotikea basi masonic wanahusika.HIzi ni propaganda ambazo dini kama ukiristo na uislam huzisambaza ili kuichafua masonic,na kufanya watu wajue kwamba masonic ni waovu.Lakin amini nakwambia hiyo sio masonic.
 
Fundisi Muhapa,

Nikikwambia umuelezee Nyerere ama uchumi wa tanzania papo kwa papo bila kutumia rejea ama kitabu chochote,kile utachosema kutoka kichwan ndo kama hiki nimeandika hapa.Sijasema kwamba nimeanzisha maneno yangu mwenywewe hapana ila sijakopy sehem hii ni kwa jinsi nnavojua mimi.nadhani umeelewa mkuu.
 
Nimekuwa nikijaribu kila wakati kufikiri na kufanya tafiti kwa kutumia akili binafsi bila machapisho wala vitabu rejeaa ma msaada hadithi za kusimuliwa,.moja ya mambo ambayo huwa nafikiria ni kuhusu jamii inayosemekana ni jamii ya siri(Free mason) kama wengi wanavoiita.,,

...

Tazama kauli yako hapo palipokolezwa. Hata mifano unayoitoa kufafanua (uchumi, baba wa taifa, n.k.) inakanusha ulichoeleza hapo. Japo ni maoni yako ila lazima kuna rejea unazo mawazoni ambazo ndo zimechochea utoke na maoni hayo-baada ya kuzichambua. Ndo hicho ambacho kinasisitizwa hapa. Kwamba ulianzaje kutafiti tu akilini mwako na ukapata cha kutafiti ni freemason? Jina tu ulitoa wapi?

Mada inazungumzia uijuavyo freemason. Maana yake umejishughulisha kutafuta elimu hiyo kwingi ama kwa tafiti za kina hadi ukaijua. Ndo ulizifanyia akilini mwako bila rejea yoyote?

Mbele kidogo unasema "Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo nimegundua ...". Mimi nasisitiza umegundua baada ya kuchambua vyanzo kadhaa si kwamba umetumia akili yako tu. Sio udhaifu kukiri vyanzo vilivyosisimua akili hadi ukawaza, kuchambua na kugundua mapya yalojifichamo "... ambayo pia yaweza kuwa tofauti na wengi wanavofikiri."

Tupo pamoja?
 
Tatizo ni uthibitisho wa yale uyasemayo.Utoaji kafara ya watu sio msingi wa masonic na sio kwamba kila afa linapotikea basi masonic wanahusika.HIzi ni propaganda ambazo dini kama ukiristo na uislam huzisambaza ili kuichafua masonic,na kufanya watu wajue kwamba masonic ni waovu.Lakin amini nakwambia hiyo sio masonic.

1.Hapo kwenye blue,wewe mwenyewe umeshindwa kunithibitishia kama 666 ni alama mojawapo wanayotumia au la. Sijajua kwa nini unakwepa kutoa jibu

Pili Hapo katika rangi nyekundu inaelekea wewe unajua hawa jamaa wanahusika na maafa na haya maafa siyo ya ng'ombe wala kuku ni ya mwanadamu ambaye wanataka kumtawala kama mpango wao unavyosema katika hadithi yako.

Sasa swali langu ni hili "TUTAJIE MAAFA JAPO MATATU MAKUBWA AMBAYO HAWA JAMAA WAMEYATENGENEZA NDANI YA MIAKA 20 ILIYOPITA "

Kila lakheri
 
sio mawazo yako mkuu kwa maana mimi ni mmoja kati ya watu wanaojitahidi kufuatilia kwa karibu kstory za FREEMASON katika makala mbalimbali za watu magazetini na katika mitandao pia sijaona tofauti na story uliyotupa wewe zaidi ya kuwa katika mtazamo tofauti na wengi wanaodhania freemason ni wapinga kristo.

Kwa nn huamini kama ni mawazo yangu??basi amini
 
COCKINGTON,

Namba 666,ni kama namba zingine na sio na hata kama inatumika haina maana kwamba wanahusika na maafa!,Mbona namba saba inatumika sana pia hata kiimani za dini zenu??,kwan ina maana mbaya?? Mfano kuna mabara saba,maajabu saba,mapigo saba,roho saba za paka n.k kwa nn saba??,na pia mbona saba imetajwa sana katika Biblia hujahoji?.

HAkuna maafa ambayo yanatengenezwa na masonic na wala hawako kwa ajili ya kufanya maafa.Huo ni uoga na propaganda za dini zenu.
 
MCHUNGAJI CHIRISTIAN JOHN NILIVYOTAJIRISHWA NA FREEMASONS KWA SIRI
Kwajina naitwa Chiristian John, wengi hupenda kuniita Mchungaji Chiristian. Natokea wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya na Kabila langu ni Mnyakyusa. Nimesoma shule ya Msingi Kibisi, nilifaulu na kujiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari Tukuyu Day. namba yangu ya simu ni 0759 889825

Familia yetu ni waumini wa Dini ya Kikristo na tumelelewa katika imani ya kiroho.Baba yangu zamani alikuwa ni mtumishi wa mungu,mchungaji John lakini kwa bahati mbaya alifariki duniani kwa ugonjwa wa Saratani ya Damu katika hospitali ya Makandana.

Kitendo cha kumpoteza baba hali ya kiimaisha ilianza kubadilika na kuwa ngumu sana tofauti na tulivyokuwa na baba mzazi. Mama alikuwa mjasiriamali katika soko la kiwira liliopo kilometa moja kabla ya kufika shule ya Sekondari ya kipoke ambayo inaendeshwa na Kanisa la Babtist.

Kuna kipindi nililazimika kutokwenda shule na kuongozana na mama sokoni ili mradi tuweze kupata pesa zitakazo kidhi mahitaji ya nyumbani.
 
SHAFII ABDALLAH,

Madhara ya story za kupikwa ndiyo haya, sasa umeshindwa kuelezea namna ulivyotajirishwa umeandika kisichoeleweka, ati ulikuwa unaenda na mama yako sokoni, au sokoni ndiyo freemason wenyewe ? unatunga story ili uje na uongo wa namna ulivyoptajirishwa na sijui kwako utajiri ni kitu gani, hujaeleza chochote kuhusu unachoitwa kutajirishwa wala namna ulivyotajirishwa, umeweka namba ya simu ili ndiyo upigiwe ueleze ulivyotajirishwa ?
 
Nimekuwa nikijaribu kila wakati kufikiri na kufanya tafiti kwa kutumia akili binafsi bila machapisho wala vitabu rejeaa ma msaada hadithi za kusimuliwa,.moja ya mambo ambayo huwa nafikiria ni kuhusu jamii inayosemekana ni jamii ya siri(Free mason) kama wengi wanavoiita.,,

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo nimegundua ambayo pia yaweza kuwa tofauti na wengi wanavofikiri.


Nitaaanza kwanza kwa kuifafanua maana ya Free mason na misingi yake,(narudia tena please hii ni kwa mujibu wangu na nnaandika kutoka kichwan sio machapisho yoyote).

Free Mason ama wajenzi huru,ni jamiii ama kikundi ambacho kina misingi toka zaman sana enzi za mfalme solomon.kwa jinsi nnavojua mimi kilianzaa kama umoja wa wajenzi waliokuwa maarufu sana wakati ule hasa katika mambo.ya ramani na usanifu majengo,kikundi hiki kilikuwa namisingi yake mashariki yakati.wakati kinaanza hawakuwa na nia yoyote mbaya kama inavyosemekana sasa.


Walianza kama umoja wa wajenzi na baadae kutanuaka hadi ulaya,asia,america kusini na kaskazin na pia africa kaskazin na ethiopia.malengo yao makubwa yalikuwa kusaidia nak udumisha umoja wao na kuendeleza chama chao.

UHUSIANO WAO NA UTAJIRI
Baada ya kupata wafuasi(wajenzi),kikundi hiki kilitanuka na kushawishi watu waliokuwa nau wezo wa kifedha kuwekeza na kujiunga nao ili kuweza kuendelza imoja wao.matajiri mbali mbali kutoka mabara hasa ya ulaya na asia pia marekani waliwasapoti na kuinua mfuko wao wa umoja wa wajenzi.

Walikuwa wakichukua tenda za ujenzi katika sehem mbalimbali duniani na hivo kuanzisha kampuni nyingi karibu kila bara na kanda kadhaa. Na kwa sababu hiyo walijitengenezea jina na heshima na kwa kuwa walikuwa wengi matajir waliweza kushawishi mambo mengi katika siasa,sayansi,na dini.waliweza kufanya mageuzi katika serikal nyingi na kuweka watu waliowataka wao.waliweza pia kufadhili tafiti mbalimbali za lisayansi na kuwasapoti watu maarufu na kuwaaminisha watu kuwa wao(watu),kuwa ni bora na wanauwezo mkubwa kuliko........


KUHUSISHWA KWAO NA SHETANI

Baada ya jamii hii kukua na kuota mizizi ikiwa kama jamii wa wasomi,wataalam,wabunifu na watu maarufu,ilianza kujipanua na kujiingiza katika serikal kubwa duniani.na kushawishi mambo ambayo yalikuwa na manufaaa kwao na hasa katika kuendeleza umoja na mfuko ama ustawi wao.,
Kutokana na kukua kwake wajenzi hawa,wakafikia hatua ya kuanzisha imani yao binafsi,ambapo moja ya misingi yao ni kuamini katika nafsi(sisi),(we the people),rejea hotuba za rais obama za kuapishwa.kwah iyo wakaanzisha utaratibu wao wa kuabudu ambapo wamekuwa wakitoa kafara na sadaka mbali mbali kutokana na imani yao.wamekuwa na ishara zao z kutambuana n.k

Kutokana na wao kuamini katika uwezo wao,wamekuwa wakihisiwa kuwa wanapinga uwepo wa anayeitwa mungu badala yake kwamba wanamuunga shetani mkono.madai haya binafsi nayapinga kwa sababu kuu zifuatazo.

1.aina ya kuabudu wanayotumia Free masoni ni ile iliyotumiwa na mnaowaita mababa wa imani,ibrahim(Abraham ),mussa na akina solomon na wengine wengi.ref.pia kabla ya kuja wakoloni africa tulikuwa tunatoa kafara hadi ya binadam kwa mizim(was that masonic worship??)

2.hakuna kitabu cha masonic rules kinachoeleza wazi kwamba hakuna mungu,ila rules zoa zinaonesha misimamo na personal charachters za mwanadam ambazo hazina uhusiano na kisichoonekana.

3.masoni hawatoi kafara ya kuua wanadam bali ni mbuz,kondoo ama wanyama ambao ni adim kuwaona.

4.chuki,uoga na udhaifu wa dini ndo chanzo cha kusingizia yote.

WANAFANYAJE KAZI
Msonic hufanya shughuli zao kwa umakini na kanuni zao ni za siri pia.wanavitabu na mafunzo ya misingi imara katika dini yao.ili kuhakikisha wanajieneza kwa kiasi kikubwa ,wao hudeal na watu maarufu ama utafiki ama bidhaa pendwa ambapo husapoti na kuendesha shughuli mbalimbali kwa ufanisi mkubwa.

NINI LENGO LAO??
1. Free masonic,hawana lengo baya kama ambavo tumekuwa tukisimuliwa kila siku katika media.,lengo lao ni kutaka kujitawanya karibu kila pembe ya dunia na hivo kupata wafuasi ama waimini wa kutosha.,

2.pia kuitawala dunia(huu ni mpango endelevu ),na kwa imani na plan zao utatimia kabla ya mwaka 2040,lengo lao ni kuona watu wote wanakuwa kitu kimoja na kuunda umoja mahal pote katika uso wa dunia.

3.kutaka kumtoa mwanadam hofu ya misemo kama,SIKU YA HUKUMU,LIFE AFTER DEATH,KIAMA,HEAVEN,HELL n.k,vitu ambavyo kwa iman yao havipo na ni vya kufikirika.

FREE MASON NI DINI??

Kwa mtazamo wangu mimi masonic sio dini kam wengi wasemavyo,..,najua hujanielewa lakini em tufafanue nn maana ya dini,kwa nijuavyo mimi Dini ni aina ya maisha(/shughuli za kimaisha) ambayo mwanadam anaishi/anafanya kila siku.shughulizi hizo ni kama kuzalisha,kutambika,na tamaduni zote.kwa hiyo nikisema dini ni utamaduni nadhn bado ntakuwa sawa.

Lakini masonic sio dini,kwa hiyo pia sio utamaduni bali masonik ni IDEA,kijerumani wanaita IDEE,masonic ni idea tu ya kufanya jambo kwa misingi na utaratibu,na hata wanapokutana pamoja na karafa zao wanazoa ripoti za utendaji kaz na kupeana mikakati ya baaadae,( kwa hiyo sio dini bali ni idea tu.),


NB,niaminivyo mimi masonic ni kama Idea zingine ama theory tu.sifa nyingine tunazitoa sisi ambazo hata wao hawana wala hawajafikiria.,samahan kwa wale nilio wakwaza kwa uzi huu,ni mawazo yangu binafsi yaweza kuwa niko wrong pia.


,kwa maelezo zaidi,tafuta kitabi changa kinaitwa Free Ideas, cha 2013 july.
 
Back
Top Bottom