Mkuu ngoja nami niseme neno hapa kuhusiana na hii kitu
Kwanza nakubaliana na wale wanaosema kuwa Lucifer ndie ibilisi kwasababu zifuatazo
Kwanza Lucifer ni neno lililotokana na neno la kilatini lenye maana ya "mwenye nuru" au "aliyetiwa nuru".Jina hilo alipewa wakati bado ni malaika mbinguni na alikuwa ni kinara wa sifa na alikuwa ni mwenye kutoa nuru kweli.Alipokokosa ule ukinara wake aliokuwa nao huko mbinguni wa uimbaji aliondoka nao lakini akawa hana tena ile nuru lakini hiyo haikubadilisha kuwa ndie Lucifer
Nikija kweye hiyo mista ri uliyoi quote iko hivi;
Isaya 14:12 inasema:
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
Na ufunuo 22:16 inasema;
16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.
Mkuu hapo kuna maneno haya "ile nyota ya kung'aa ya asubuhi" ambayo ni maneno ya Yesu na "Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi".Hayo maneno yana maana tofauti na hayazungumzii kitu kimoja
Asubuhi ni tofauti na alfajiri
Lakini pia kuna kitu wengi hawakioni hapo,ambacho hawakioni hapo ni hiki "mwana wa subuhi" Lucifer ametajwa kuwa ni "mwana wa asubuhi" kwasababu Yesu ambae ni nyota ya asubuhi ndie aliyemuumba Lucifer ndio maana anaitwa hivyo
Lucifer kuitwa nyota ya alfajiri kuna maana kuwa sio nyota ya subuhi,Nyota ya alfajiri iko na inajulikana jina lake nadhani ni venus [sina uhakika] na nyota ya subuhi ni jua
Lucifer anaitwa nyota ya alfajiri na Yesu nyota ya asubuhi kwakuwa ni kweli Lucifer ana nuru [kama ilivyo nyota ya asubuhi [venus] na Yesu nae ana nuru lakini ni kuzidi ile ya alfajiri [Jua]
Hiyo ni rahisi kujulikana kwasababu Jua lina nuru kuliko nyota,lakini zaidi sana nyota nazo zinatoa nuru kutoka kwenye jua hivyo kuthibitisha kuwa ni mwana wa asubuhi kwakuwa kwanza bila Yesu hakuna nyota kwamaana ya uumbaji lakini pia bila Yesu hakuna nyota kwamaana ya nyota kutoa mwanga wake kwenye jua
Kwa kifupi uwepo wa nyota unategemea uwepo wa jua,kwa maneno mengine uwepo wa Lucifer unategemea amri ya Yesu
Kwa ufafanuzi huo mdogo nadhani nitakuwa nimeeleweka kwa kiwango cha kutosha
Ubarikiwe
CC:
Kaunga ,
MaxShimba , @Shlendler
Stefano Mtangoo !!
I stand to be corrected!