Yaani kuwa na uelewa wa mambo mbambali ni mateso makubwa hasa kwenye nchi ya Tanzania nimegundua watu wenye uelewa mdogo wa mambo (ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisayansi) wana raha kubwa sana na wanafurahia maisha vizuri, yaani kwao bora liende hawajui chochote kinachoendelea.
Kuna mambo mengi makubwa yanatokea tena yakuogopesha kwa mtu mwenye kufikiri vizuri, lakini wenzagu wenye uelewa mdogo wala hawapati machungu yoyote yale maisha kwao yanasonga mbele kama vile hakuna kinachotokea, kiufupi wenzagu raha wanayo.
Sasa naomba mnipatie mbinu ya kuondoa uelewa wa kutafakari na kuchambua mambo, ili niwe kama zezeta fulani na mi nifurahie maisha.
Nimeona njia pekee ya kufurahia maisha apa Bongo ni kuwa na uelewa mdogo wa mambo.