Nifanyeje niwe na uelewa mdogo?

Nifanyeje niwe na uelewa mdogo?

Ukishakua member wa ukawa tayari unakua umetimiza lengo lako
 
Pengine na wewe inawezekana unauelewa mdogo,ndio maana unateseka..
 
Yaani kuwa na uelewa wa mambo mbambali ni mateso makubwa hasa kwenye nchi ya Tanzania nimegundua watu wenye uelewa mdogo wa mambo (ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisayansi) wana raha kubwa sana na wanafurahia maisha vizuri, yaani kwao bora liende hawajui chochote kinachoendelea.

Kuna mambo mengi makubwa yanatokea tena yakuogopesha kwa mtu mwenye kufikiri vizuri, lakini wenzagu wenye uelewa mdogo wala hawapati machungu yoyote yale maisha kwao yanasonga mbele kama vile hakuna kinachotokea, kiufupi wenzagu raha wanayo.

Sasa naomba mnipatie mbinu ya kuondoa uelewa wa kutafakari na kuchambua mambo, ili niwe kama zezeta fulani na mi nifurahie maisha.
Nimeona njia pekee ya kufurahia maisha apa Bongo ni kuwa na uelewa mdogo wa mambo.
Piga punyeto...
 
1. Achana na JF
2. Acha kusikiliza na kuangalia taarifa za habari na kusoma magazeti
3. Acha kabisa kufuatilia current events zozote zile
4. Shinda Instagram na uwafuate wasanii wa bongo fleva na bongo movie
5. Tafuta team ya kujiunga nayo - kama team Wema, team Mondi, team Kiba, n.k.
6. Kuwa mmbea - fuatilia kwa ukaribu bifu za akina Mange, Linda, Recho, na KichwaP😀
7. Kuwa fan wa Le Mutuz
U nailed it all babu, but/lakini huyu Le Mutuz si ndio akili kubwaz with 3 degree?
 
Njia ni moja tu: kuwa Dini fanatic. Dini zinafanya wengi kuwa vichaa kuliko kitu kingine chochote. Popote dini ilipokolea maendeleo ni sifuri.
 
Ni kweli kuna jamaa nilimuliza rais alikuwa kenya juzi jamaa akasema hamna kitu kama hicho

Nikamwambia mwana bungeni mambo yamesha haribika Mbowe kakinukisha jamaa ananijibu acha ujinga kwani bunge lilisha anza vikao vyake?

Yaani kuna raia wahajui nini kinacho endelea humu duniani tofauti na kuangalia maisha yake!

Kuna watu flani wanaishi maporini Wahazabe yaani hawa jamaa ndiyo funika wanajua rais ni Nyerere hadi leo! Enzi za Nyerere alikuwa anaenda kuwatembelea anawapelekea asali!
 
Mkuu kuanzia namba moja hadi tatu uko sahihi na utamsaidia kwa hii shida yake.
Namba nne na tano ataongeza maarifa ya upande wa pili, atabobea huko kwenye ma team na umbea ambayo nayo itamsumbua. Kwa ufupi yeye hataki apate shida na kitu anachokifaham. Akaishi porini kwa watindiga na wadzabe!!
Kwenye hiyo orodha ongeza kipengele cha kuangalia picha za uchi na kupiga nyeto kwa sana.
 
Kwenye hiyo orodha ongeza kipengele cha kuangalia picha za uchi na kupiga nyeto kwa sana.

Ha ha haaa hiyo itamuongezea ilim ya aina nyingine. Atataka kujua zaidi afanye nini aridhike zaidi na kujifurahisha?
 
Yaani kuwa na uelewa wa mambo mbambali ni mateso makubwa hasa kwenye nchi ya Tanzania nimegundua watu wenye uelewa mdogo wa mambo (ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisayansi) wana raha kubwa sana na wanafurahia maisha vizuri, yaani kwao bora liende hawajui chochote kinachoendelea.

Kuna mambo mengi makubwa yanatokea tena yakuogopesha kwa mtu mwenye kufikiri vizuri, lakini wenzagu wenye uelewa mdogo wala hawapati machungu yoyote yale maisha kwao yanasonga mbele kama vile hakuna kinachotokea, kiufupi wenzagu raha wanayo.

Sasa naomba mnipatie mbinu ya kuondoa uelewa wa kutafakari na kuchambua mambo, ili niwe kama zezeta fulani na mi nifurahie maisha.
Nimeona njia pekee ya kufurahia maisha apa Bongo ni kuwa na uelewa mdogo wa mambo.
omba uwe mwanachama wa ccm
 
Back
Top Bottom