Kuna uhusiano gani katika hili? Msaada tutani

Joined
Sep 3, 2025
Posts
48
Reaction score
85
Wakuu salaam,

Nakuja kwenu ndugu yenu, kaka yenu pia mdogo wenu kwa heshima kubwa nikihitaji msaada wenu wa mawazo nikaamini Kuna watu wanauzoefu wa namna yoyote au uelewa mkubwa kuzidi wangu.

Kwanza niweke wazi kwamba katika maisha yangu na uhai wangu huu katika kitu sipendi kukiona ni maiti, Ndio Yaani nikiona binadamu ambaye roho yake imeacha mwili Huwa najisikia vibaya sana pia huwa napoteza nguvu ya ndani, nakua naona kama maisha hayana maana tena yaani napoteza morali ya kufanya kitu chochote na hali hii niliigundua nikiwa na miaka 12.

Nilikua form one ambapo mwanafunzi mwenzetu alifariki kwahiyo shule nzima ilitulazimu kumuaga baada ya kuona ule mwili kwakweli hali yangu ilibadilika na ilinichukua muda mrefu sana mpaka kurudi hali yangu. Baada ya hapo nilifikia maamuzi kwamba sitokuja tena kuangalia maiti.
Kutokea hapo sijawahi kuangalia maiti mpaka nimefikia umri huu nilionao Leo.

Turudi kwenye maada iliyonileta kwenu. Ni kwamba hivi nilipoanza kujitambua zaidi kuna kitu nilikinotice kwenye maisha yangu. Yaani mtu anapokaribia kufariki huwa najikuta najitenga nae Yaani sitaki ukaribu wowote na huyo mtu na sio kwamba anakua ameniudhi hapana ila huwa najikuta tuu nakua nakaa mbali nae au namkwepakwepa na baada ya muda nasikia amefariki.

Jambo hili limetokea zaidi ya mara tatu sasa kwa watu tofauti ikiwepo mtoto mchanga wa miezi chini ya sita, pia hali kama niliyoielezea hapo juu imeanza kunitokea kwa mtu wangu wa karibu sana, alizoea kunipigia simu ila sasa hivi hanipigii na hata siwazi sana na zaidi sitamani tena anipigie simu, Pia Kuna siku nilimuota ananikabidhi mdogo angu wa mwisho kwamba nimlee, huyu dogo yeye pekee ndio bado anasoma, pia mara mbili nimeota tumesimama mahali ila huyu ndugu yangu yeye hayupo.

Kinachonileta kwenu ni kuomba msaada juu ya hii Hali, Yaani nawezaje kuichukulia? Je! Niwe nawafuata watu nawambia kinachoendelea mfano huyu ndugu yangu wa karibu au niendelee kubaki kuwa mtazamaji mpaka yatakapotokea? Lakini kubaki kuwa mtazamaji Bado pia huwa inanisumbua sana akilini kitu ambacho kinanifanya nitafute kwenda mbali na huyo mtu.
Kwenu wakuu naomba msaada wa ushauri au yeyote mwenye uzoefu wa haya mambo.

Karibuni.
 
Fupisha report yako, unajielezea sana huendi kwenye hoja ya msingi
 
Mkuu miili yetu huwa ina ushirikiano mkubwa sana na mazingira yetu. Kuna watu ambao ni highly sensitive kwenye nishati. Mtu anapougua sana au kufika mwisho wa safari yake, biologically energy level yake huwa inashuka kwa kasi sana.

Kwa sababu wewe una ile trauma na phobia ya kifo tangu utotoni, akili yako itakuwa inasoma hiyo hali mapema kama danger signal. Kinachotokea ni automatic reflex action ya mwili wako kujitenga ili kujilinda usipate maumivu.

Yani mfumo wako wa ulinzi wa mwili ndio unafanya kazi yake. Work on your phobia first, mengine yote yataisha.
 
Kwa upande wangu kwanza naomba kama huyu ambaye unamdhania huenda atakufa soon,akifa naomba utupe mrejesho kwenye uzi huu,nataka kujua ukweli zaidi juu ya hizi hisia zako

Lakini pili ni kweli kuna watu wana nguvu mbali mbali ambazo wamejaaliwa kuwa nazo ,kuna ile inaitwa telepath ile hali ya mtu kuwasiliana kihisia au kuhisi jambo fulani linamtokea mtu fulani ambaye upo mbali nae na kweli baadae inakuwa hivyo

Mfano binafsi,nikimkumbuka mtu basi ujue nae ananikumbuka,mara nyingi najisikia kumpigia mtu simu unakuta muda si mrefu ananipigia kama sio leo basi ujue kesho,na nikimwambia mtu huyo ujue nilitaka kukupigia ananipiga madongo kwamba we muongo umeona nimekuchek ndio maana unasema hivyo,mpaka now naamua kupiga kimya tu

Juzi kati tu kama siku tano au sita nimemkumba mama yangu,kila nikisema nimchek mara limetokea hili nasahau,yeye ndio akanipigia,nikamwambia ujue mama toka juzi nimekukumbuka nasema nakupigia mara najissahau,akaniambia hata mimi toka majuzi nimekukumbuka kweli mwanangu

Kwahiyo ni nguvu tu ambazo kila mtu amejaaliwa kuwa nazo
 
Asante mkuu hapa nimekuelewa, kiasi Fulani naweza kukuelewa ulipohusianisha na energy maana binafsi nikikaa pekee angu kwa muda mrefu huwa naweza kufeel Kila kitu.

Mfano, ukificha kitu afu niwe nakitafuta bhasi Huwa naenda exactly to the point na nakiona au labda mtu akiwa anahitaji kitu huwa naenda kuchukua nampa mpaka mwenyewe anashindwa kuelewa nimejuaje.
Kubwa zaidi imenitokea kwa watu zaidi ya watano ambao nakutana nao katika mazingira Fulani na nawambia kitu wanachotakiwa kufanya na wanafanikiwa.

Hivyo vyote hapo juu huwa naamini ni energy tuu ambayo huniwezesha kutambua mazingira na Nini nifanye kwa mtu aliyepokaribu.

Turudi kwenye maada, mfano wa huyo mtoto mchanga ni kwamba tulikua tunasafiri kwenye bus Mimi nipo siti ya nyuma alafu mtoto, baba na mama yake wamekaa siti ya mbele bhasi baba wa mtoto alikua akimnyanyua yule mtoto tunakua tunaonana na mtoto uso kwa uso namimi nilikua nafanya kama kucheza na yule mtoto mfano nachezesha kope na vitendo vingine kitu ambacho kilikua kinamfanya mtoto afurahi, Sasa baba wa mtoto aligeuka nyuma akaniangalia akaniambia yaani mtoto anachezea miguu kama anataka kukukimbilia. Tulivyofika safari tulikua tunaenda kambi baba mtoto alijaribu sana kumleta yule mtoto karibu namimi ili japo nimshike lakini moyo wangu ulikua unagoma na baadae nikaanza kumkwepa lakini baada ya kumaliza kambi Mimi nilienda kwenye biashara zangu na baada ya miezi miwili nilisikia katoto kamefariki,💔
Swali langu ni Je! Ningembeba yule mtoto angeendelea kuishi? Hapa ndio napata maswali zaidi kwamba nikichukua hatua nyingine naweza kubadilisha jambo?
 
Nasema kwa asilimia mia huwezi kubadilisha jambo,kwasababu uhai na kifo ni kazi ya Mungu pekee, wewe umepewa zawadi ya kuhisi energy inayokuzunguka,ni kama vile wanasema paka nao wanajua kama kuna mtu anakufa muda si mrefu kwa yule ambaye anafugwa na watu wake,anaweza kuja kukaa karibu na wewe kwa unyonge sana,kwa siku kadhaa halafu baadae unasikia mtu kavuta
 
Upo sahihi mkuu hasa hapo kwenye telepathy mara nyingi jambo hilo huwa linanitokea pia hasa kwa mtu ambaye ninabond nae nzuri,
Yaani kuna mtu huwa naweza mpaka kusoma mawazo yake😂😂😂 hii tabia niliacha maana ilikua inanipa shida, nashindwa kuwachukulia watu yaani unakuta mtu anaweza mambo ya kijinga na ukimuuliza mbona unawaza ujinga wewe anasema Mimi mchawi nimejuaje? Namshukuru Mungu alikitoa hiki kipawa kwangu maana ilikua hainipendezi kusoma mawazo ya watu, lakini pia ilinipa hasara maana nilianza kuwaamini watu hovyo kitu ambacho kimenipa hasara kubwa sana maishani mwangu natamani pia ningekuwa nacho Bado ili niwe najihami mapema.

Turudi kwenye maada hapo mkuu unaposema tusubiri jambo litokee kwa huyu mtu wangu wa karibu kwangu inakua ngumu ndio maana nimekuja kwenye jukwaa ili kuweka kupata mawazo mbadala.
 
Asante mkuu hapa nimekuelewa, kiasi Fulani naweza kukuelewa ulipohusianisha na energy maana binafsi nikikaa pekee angu kwa muda mrefu huwa naweza kufeel Kila kitu.

Mfano, ukificha kitu afu niwe nakitafuta bhasi Huwa naenda exactly to the point na nakiona au labda mtu akiwa anahitaji kitu huwa naenda kuchukua nampa mpaka mwenyewe anashindwa kuelewa nimejuaje.
Kubwa zaidi imenitokea kwa watu zaidi ya watano ambao nakutana nao katika mazingira Fulani na nawambia kitu wanachotakiwa kufanya na wanafanikiwa.

Hivyo vyote hapo juu huwa naamini ni energy tuu ambayo huniwezesha kutambua mazingira na Nini nifanye kwa mtu aliyepokaribu.

Turudi kwenye maada, mfano wa huyo mtoto mchanga ni kwamba tulikua tunasafiri kwenye bus Mimi nipo siti ya nyuma alafu mtoto, baba na mama yake wamekaa siti ya mbele bhasi baba wa mtoto alikua akimnyanyua yule mtoto tunakua tunaonana na mtoto uso kwa uso namimi nilikua nafanya kama kucheza na yule mtoto mfano nachezesha kope na vitendo vingine kitu ambacho kilikua kinamfanya mtoto afurahi, Sasa baba wa mtoto aligeuka nyuma akaniangalia akaniambia yaani mtoto anachezea miguu kama anataka kukukimbilia. Tulivyofika safari tulikua tunaenda kambi baba mtoto alijaribu sana kumleta yule mtoto karibu namimi ili japo nimshike lakini moyo wangu ulikua unagoma na baadae nikaanza kumkwepa lakini baada ya kumaliza kambi Mimi nilienda kwenye biashara zangu na baada ya miezi miwili nilisikia katoto kamefariki,💔
Swali langu ni Je! Ningembeba yule mtoto angeendelea kuishi? Hapa ndio napata maswali zaidi kwamba nikichukua hatua nyingine naweza kubadilisha jambo?
Mkuu hata kama ungembeba, kisingebadilika kitu. Na huwezi kubadilisha kifo cha mtu kwa kuchukua hatua mbadala, kwa sababu wewe sio chanzo. Hiyo intuition yako itumie kuwasaidia walio hai kama unavyofanya sasa hivi, lakini ukiona inakuletea woga na kujitenga, jua hiyo ni phobia yako ya utotoni ndiyo tatizo haswa.
 
Turudi kwenye maada hapo mkuu unaposema tusubiri jambo litokee kwa huyu mtu wangu wa karibu kwangu inakua ngumu ndio maana nimekuja kwenye jukwaa ili kuweka kupata mawazo mbadala.
Sasa unataka kufanya nini? Kwamba umueleze kuwa unakaribia kufa? Je utaeleweka? Au unataka kuitwa mchawi kwamba ulisema jamaa atakufa na kweli akafa?

Au unadhani unaweza badilisha hatima yake,kwamba ukimwambia inaweza kumuokoa na kifo,,hiyo kitu hakuna ikifika siku yako imefika,je kuna mtu angetaraji Lissu angekuwa hai,lakini siku yake bado,unakumbuka ile ajali ya ndege india,wakati ndege inapaa ikaungua,akapona mtu mmoja tu,basi jua kifo ni fumbo kubwa sana,kwahiyo wewe just observe mambo tu lkn huwezi badilisha chochote
 
Nasema kwa asilimia mia huwezi kubadilisha jambo,kwasababu uhai na kifo ni kazi ya Mungu pekee, wewe umepewa zawadi ya kuhisi energy inayokuzunguka,ni kama vile wanasema paka nao wanajua kama kuna mtu anakufa muda si mrefu kwa yule ambaye anafugwa na watu wake,anaweza kuja kukaa karibu na wewe kwa unyonge sana,kwa siku kadhaa halafu baadae unasikia mtu kavuta
Duuh! Sawa mkuu najaribu sana kukuelewa.

Kuna kipindi nilikua naota karibia Kila siku nakutana na watu wawili wamevaa mavazi meupe namimi pia nimevaa mavazi meupe kama wao jumla tunakua watatu, Lakini nikiwaangalia wale watu wanaonekana ni transparency namimi pia nakua transparency kama wao.
Nilikua napiga nao story nyingi sana alafu Kuna muda ni kama wanataka kuondoka ila Mimi natamani kuendelea kubaki nao, maana mazingira ya kule ni amani alafu ni Raha sana. Bhasi mmoja wapo alikua ananigusa begani najikuta nashtuka nipo kitandani na tayari ni alfajiri.

Hii pia ni Moja ya kumbukumbu ambayo iliniacha na gepu kubwa moyoni maana wale watu hawaji tena. Na ilitokea hivyo baada ya kuanza kuyachukia maisha ya hapa duniani Yaani nilikua natamani niwe naonana na wale watu. Je! Unaweza kuwa na uzoefu wowote na hii Hali?
 
Back
Top Bottom