Naomba Ushauri na Msaada Kuhusu OCD Inayonitesa Kila Siku

Naomba Ushauri na Msaada Kuhusu OCD Inayonitesa Kila Siku

Mjomba Malume

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2025
Posts
903
Reaction score
1,317
Wakuu salamuni.

Nimeamua kuanzisha huu uzi baada ya kuona hii hali imeanza kunipa usumbufu mkubwa kwenye maisha yangu ya kila siku. Kuna baadhi ya vitu navifanya kwa kurudia rudia sana kiasi kwamba vinanichosha na kunipotezea muda bila sababu ya msingi.

Mfano nikifunga mlango, baada ya kuondoka nahisi kama sijaufunga vizuri hivyo narudi tena kwenda kuangalia. Wakati mwingine narudia mara mbili hadi tano kuhakikisha tu umefungwa. Pia nikizima switch au vifaa vya umeme, lazima nijiridhishe mara nyingi kama kweli nimezima. Hata nikishaangalia bado mawazo yananilazimisha nirudi tena kuhakiki.

Hii hali imekuwa ikinifanya nichelewe mambo mengi, nipoteze muda kwenye vitu vidogo vidogo na wakati mwingine nikose kabisa amani ya moyo na raha ya kawaida. Kinachoniumiza zaidi ni kwamba akili yangu huwa inajua kabisa kuwa tayari nimefanya hicho kitu, lakini bado kuna msukumo wa kutaka kurudia kuhakiki tena na tena.

Nilijaribu kuwauliza baadhi ya watu kuhusu hii tabia, wengi wakaniambia huenda ni tatizo la OCD. Ndiyo maana nimekuja kwenu wakuu, labda kuna mwenye experience au uelewa kuhusu hili aniambie namna ya kupambana nalo au kupata solution yake.

Karibuni ushauri wenu wakuu.
 
1. Lala usingizi wa kutosha hasa wa usiku.
Hilo ni tatizo la kupoteza kumbukumbu.

2. Fanya vitu kwa wakati na mpangilio.
Anza ratiba yako mapema. Usi-rush

Kama unatakiwa kutoka saa 4 toka dakika tano au kumi nyuma. Jiandae mapema.

Ukiwa mtu wa harakaharaka kusahau au kutokukumbuka kilichotokea ni jambo la kawaida

3. Uwe na daily routine unayoitiki kwa alama utakayoiweka.
Mfano ukimaliza jambo fulani unaweka tiki kabla hujaingia jambo jingine.

Kila la kheri
 
OCD stands for Obsessive-Compulsive Disorder.

It is a chronic mental health condition where a person experiences uncontrollable, recurring thoughts (obsessions) and feels driven to repeat specific behaviors or rituals.
 
Wakuu salamuni.

Nimeamua kuanzisha huu uzi baada ya kuona hii hali imeanza kunipa usumbufu mkubwa kwenye maisha yangu ya kila siku. Kuna baadhi ya vitu navifanya kwa kurudia rudia sana kiasi kwamba vinanichosha na kunipotezea muda bila sababu ya msingi.

Mfano nikifunga mlango, baada ya kuondoka nahisi kama sijaufunga vizuri hivyo narudi tena kwenda kuangalia. Wakati mwingine narudia mara mbili hadi tano kuhakikisha tu umefungwa. Pia nikizima switch au vifaa vya umeme, lazima nijiridhishe mara nyingi kama kweli nimezima. Hata nikishaangalia bado mawazo yananilazimisha nirudi tena kuhakiki.

Hii hali imekuwa ikinifanya nichelewe mambo mengi, nipoteze muda kwenye vitu vidogo vidogo na wakati mwingine nikose kabisa amani ya moyo na raha ya kawaida. Kinachoniumiza zaidi ni kwamba akili yangu huwa inajua kabisa kuwa tayari nimefanya hicho kitu, lakini bado kuna msukumo wa kutaka kurudia kuhakiki tena na tena.

Nilijaribu kuwauliza baadhi ya watu kuhusu hii tabia, wengi wakaniambia huenda ni tatizo la OCD. Ndiyo maana nimekuja kwenu wakuu, labda kuna mwenye experience au uelewa kuhusu hili aniambie namna ya kupambana nalo au kupata solution yake.

Karibuni ushauri wenu wakuu.
Pole sana kwa changamoto unayopitia..
kuishi na ugonjwa wa kuwaza au kurudia jambo kupita kiasi (OCD) kila siku inachosha sana kiakili, lakini ugonjwa huu unatibika na unaweza kurudisha udhibiti wa maisha yako.

OCD inajumuisha mzunguko wa mawazo yanayoingia akilini bila kupenda na kusababisha wasiwasi mkubwa, yanayokulazimisha kufanya matendo ya kurudiarudia ili kupunguza wasiwasi huo.

Kupambana na hali hii peke yako ni ngumu, hivyo unahitaji mchanganyiko wa msaada wa kitaalamu na mbinu binafsi za kila siku ili kuushinda mzunguko huu unaokutesa.

Njia kuu na ya uhakika ya kushinda OCD ni kupata tiba sahihi ya kisaikolojia kutoka kwa wataalamu wa afya ya akili.

Dar es Salaam kuna vituo vinavyotoa Tiba ya Utambuzi wa Tabia (CBT), kama vile
1. Mind Matters (Haile Selassie Road),
2. hospitali ya London Health Center,
3. daktari binafsi Bosco Psychotherapist (Mkwajuni Road).

Pia, unaweza kufika katika Idara ya Afya ya Akili Hospitali ya Taifa Muhimbili au Hospitali ya Saifee kwa ajili ya ushauri wa kibingwa na uwezekano wa kuandikiwa dawa za kupunguza ukali wa wasiwasi ikiwa itahitajika.

Wakati unatafuta msaada wa daktari, unaweza kuanza kupunguza nguvu ya OCD kila siku kwa kuahirisha matendo ya kulazimishwa na kutoshindana na mawazo yanayoingia akilini.

Ukipata msukumo wa kukagua au kusafisha kitu, jiambie utafanya hivyo baada ya dakika tano, kisha ongeza muda huo kadri siku zinavyoenda ili kuufundisha ubongo kuvumilia wasiwasi bila kufanya tendo hilo.

Kubali mawazo hayo kama "wazo la OCD tu" na uyaache yapite yenyewe bila kuyapa uzito, huku ukipunguza msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi na kupata usingizi wa kutosha.

Mabadiliko makubwa huanza na hatua ndogo ndogo, na jambo la msingi ni kuwa na uvumilivu kwani kupona OCD ni mchakato wa hatua kwa hatua.

Ni muhimu pia kufunguka na kumshirikisha rafiki au mtu wa familia unayemwamini ili usijihisi uko peke yako katika mapambano haya magumu.
 
Tuanze na hiyo "OCD" ndiyo nini kitaalamu?
Obsessive–compulsive disorder (OCD) is a mental disorder characterized by intrusive thoughts (obsessions) and repetitive behaviors (compulsions) that individuals feel driven to perform to alleviate the distress caused by these thoughts. It affects approximately 1-3% of the general population and can significantly impair daily functioning.
 
Nimelewa ugali nadhani.Mkuu mleta uzi,naomba nikuelewe.Akili zangu nyembamba kama tishu.Tuanze na hiyo "OCD" ndiyo nini kitaalamu?
Obsessive-Compulsive Disorder (OCD) is a chronic, long-term mental health condition characterized by a distressing cycle of obsessions and compulsions.
Nenda hospital muone psychiatrists Kwaajili ya ushauri na pengine uanze dawa. Cha kukupongeza ni kkuwa angalau umejjua shida na ukoo positive. Hiii hali itaisha ukianza dawa. Usipo ttibbiwa utaanza kuwa aggressive na unaweza pata schizophrenia. Pole sana mwamba
 
Nashukuru kwa ufafanuzi na ushauri wako.Lakini,si mimi mwenye hiyo "OCD"!Ni mleta uzi mhishimiwa!
 
Back
Top Bottom