Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,227
Kuna mtu kwa kiasi fulani kajaribu kujibu tatizo lako.Kwanini karo la choo linajaa haraka nifanyenini kisiwe kinajaa haraka?
Kama ambavo mada inajieleza hapo juu,
Naomba ushauri wako wa hali na mali, shimo au karo la choo changu kilijaa miaka 5 ya kukitumia nikaita wale wanao nyonya na magari wakakafanya hiyo kazi na kikawa kitupu kama mwanzo.
Cha ajabu baada ya kukitumia kwa mwaka 1 na nusu tu kimejaa tena wakati idadi ya familia yaani watu hawajaongezeka nilitegemea itachukua tena angalau miaka mingine hata 4 au 3 kuja kujaa, sasa nimetumia mwaka 1½ tu kimejaa, tatizo ni nini na nini nifanye ili angalau kisiwe kinajaa haraka hivo?
Ukinisaidia ushauri na mbinu za kufanya utakuwa umewasidia na wengine ambao wanapitia mada hii ahsanteni sana na samahani kwa usumbufu.
Karibuni sana.
Inaelekea hapo ulipojenga kuna high water table.
Maji yanayo jaa hayatokani mia kwa mia na choo cha nyumba yako, bali na maji ya ardhini.
Kimsingi hilo ni tatizo kubwa.
Njia rahisi ni kujenga septic na soak pit.
Ambapo soakpit iwe na mabomba yenye matobo(french drains) za kupeleka maji yaliyo ozeshwa na kusafishwa na septic tank hadi mitaroni.