Nifanye nini karo la choo lisijae haraka?

Bujoro

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,046
2,131
Kwanini karo la choo linajaa haraka nifanyenini kisiwe kinajaa haraka?

Kama ambavo mada inajieleza hapo juu,

Naomba ushauri wako wa hali na mali, shimo au karo la choo changu kilijaa miaka 5 ya kukitumia nikaita wale wanao nyonya na magari wakakafanya hiyo kazi na kikawa kitupu kama mwanzo.

Cha ajabu baada ya kukitumia kwa mwaka 1 na nusu tu kimejaa tena wakati idadi ya familia yaani watu hawajaongezeka nilitegemea itachukua tena angalau miaka mingine hata 4 au 3 kuja kujaa, sasa nimetumia mwaka 1½ tu kimejaa, tatizo ni nini na nini nifanye ili angalau kisiwe kinajaa haraka hivo?

Ukinisaidia ushauri na mbinu za kufanya utakuwa umewasidia na wengine ambao wanapitia mada hii ahsanteni sana na samahani kwa usumbufu.

Karibuni sana.
 
Mpunguze kiasi cha chakula mnachokula, Kumbuka “garbage in, garbage out”

Tenganisha karo la mzigo na maji taka, mf maji ya kuoga, kufua nk yawe na njia yake tofauti.

Mkuu nyonya nyonya watakula wapi kama hamtaki makaro yajae waje kufyonza?? Haha
 
Nadhani inategemea na maeneo uliyopo yana udongo wa aina gani. Kama mimi huku kwetu nina miaka 20 sasa shimo halijajaa... na niko na njemba zinakunya balaa.

Lakini nikiwa Sinza... njemba zikiwa bado miduchu...hatukuwa tunamaliza mwaka bila kuita nyonyanyonya...

Kuna dawa za kichina nimeona jamaa wengi wenye mabaa wanazitumia. Shimo likijaa wanamimina kwenye shimo baada ya muda mzigo unashuka chini...
 
Mpunguze kiasi cha chakula mnachokula, Kumbuka “garbage in, garbage out”

Tenganisha karo la mzigo na maji taka, mf maji ya kuoga, kufua nk yawe na njia yake tofauti.

Mkuu nyonya nyonya watakula wapi kama hamtaki makaro yajae waje kufyonza?? Haha
Ni shimo 1 tu sina sehemu nyingine ya kuchimba harafu pia vyuma mkuu we mbinu ingine ya kusaidia mana hata nikinyonya kitajaa tena na inaweza kywa haraka zaidi
 
Maji ya sabuni mnayooga yanauwa wale wadudu funza wanashindwa kuvuruga kinyesi kiwe majimaji kipenye kwenda ardhini badili njia ya maji ya bafuni yasiingie humo
Sasa mbona mwanzo kilichelewa kujaa na safar hii niliponyonya nmejaa fasta kwann hapo
 
Pole sana! Sabuni inaua bacteria wanaoozesha kinyesi na hivyo decomposition ya kinyesi inachukua muda mrefu. Funza hahusiki hapa bwana luhuye
Hili nilikuwa sikijui kusema kweli ngoja nijioange nichimbe tu karo lingine kwa ajili ya maji ya kuoga
 
Pole Kwa hiyo changamomtomkuu
Hujafafanua vyema
Una mashimo yote mawili? Yaani septic soakwaypit? Jibu hapo then tuendelee
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom