Nifanye nini karo la choo lisijae haraka?

Watu wanakulisha matango pori hapa mkuu. Hakuna decmposition sijui mnaogea sabuni wala kula sana hapa.

Tatizo lako ni kwamba, cesspit au septic tank lako liko sehemu ambayo ina low water table. Ka maana nyingine chimo lako la choo limekuwa kama kisima cha maji. KInacholijaza sio sewage yenu bali ni maji yanayoingia toka nje (underground water flow). Hili ni tatizo linalowakabili watu wote wanaoishi sehemu zenye majimaji kama Sinza. Sintashangaa kusikia tatizo lako ni kubwa hata zaidi wakati wa mvua.

Tatizo ulikosea wakati wa kulijenga. Katika sehemu za maji, unapojenga cesspit lazima ulisilibe sana kwa cement ili lisiingize maji kutoka nje kwa kupitia chini au kuta za pembeni. Lazima liwe water tight kama vile unavyotengeneza swimming pool.

Sasa solution ni kujenga jipya kwa jia niliyokueleza hapo juu, maana sio rahizi kuli-seal cesspit lililokwisha tumika.

Unapojenga la pili unaweza kulifanya lililopo liwe lina-overflow kwenda la pili. KUmbuka kwamba wakati wa kiangazi kikali unaweza ukawa na vesspit ambalo linakausha maji kwa kuwa udongo unaolizunguka unakuwa mkavu na hivyo maji yanaflow kutoka kwenye ceepit lako kwenda nje. Wkati maji nje ya ceepit yamezidi basi yatasababisha kulijaza cesspit. KUna kitu kama diffusion hivi kinafanyika.

THeory ya kuweka chumvi ni katika suala zima la diffusion, kwamba unaongeza concentratio ya chumvi ndani ya tank inayasababisha maji ya-flow kuelekea sehemu ambayo ina concentration ndogo ya chumvi. Watoto watakuambia kuhusu flow of fluid from high to low concentration through a semipermeable membrane. Ndicho kjnachofanyika ukiweka chumi nyingi.
Sasa kama mimi nimejenga sehemu ya udongo wa mfinyanzi na shimo ni moja nafasi ni ndogo, pia majirani hawajajenga mashimo mazuri nahisi pia maji yao yatembea yanakuja kwangu , ushauri pls nimejenga shimo la kawaida linajaa mwezi nikaamua kuweka biodigester nalo maji yanatoka nje ya fensi hadi nimeitiwa manispaa ushauri pls
 
Hii ndio fomula ya kushusha choo/ kuyeyusha choo:

-Chumvi ya mawe 5kg
-Chlorine lita 1
-Chokaa 5kg.

Changanya kisha mwaga kwenye shimo la choo/ chamber.
 
Kwanini karo la choo linajaa haraka nifanyenini kisiwe kinajaa haraka?

Kama ambavo mada inajieleza hapo juu,

Naomba ushauri wako wa hali na mali, shimo au karo la choo changu kilijaa miaka 5 ya kukitumia nikaita wale wanao nyonya na magari wakakafanya hiyo kazi na kikawa kitupu kama mwanzo.

Cha ajabu baada ya kukitumia kwa mwaka 1 na nusu tu kimejaa tena wakati idadi ya familia yaani watu hawajaongezeka nilitegemea itachukua tena angalau miaka mingine hata 4 au 3 kuja kujaa, sasa nimetumia mwaka 1½ tu kimejaa, tatizo ni nini na nini nifanye ili angalau kisiwe kinajaa haraka hivo?

Ukinisaidia ushauri na mbinu za kufanya utakuwa umewasidia na wengine ambao wanapitia mada hii ahsanteni sana na samahani kwa usumbufu.

Karibuni sana.
Pamoja na mbinu hiyo ya kutenganisha maji ya bafuni fanya hii ambayo mm ilinisaidia na nishawahi kuipost humu

Sasa inategemea na msingi wako wa nyumba upoje,kama upo chini sana haitawezekana ila kama juu tatizo litaisha

Cha kufanya(kama msingi upo juu) bomoa shimo la choo,pandisha urefu wa kama rula 2 hv kutoka usawa wa ardhi...yani shimo liende juu cm 60+ kutoka usawa wa ardhi then lile bomba linalomwaga uchafu usilipitishie kwa pembeni..lipitishie juu..yani limwage uchafu kupitia juu ya shimo

Nakwambia utasahau kabsa hilo tatizo la shimo kujaa..kwani BY NATURE maji hayawezi kujaa hadi kumwagika nje ya shimo(labda hilo shimo liwe na chemchem haswaa)..lazma yatafika sehemu yatajibalance yenyewe..hayataongezeka yanabaki hapo hapo

Tatizo ni kwamba bomba la kumwaga uchafu umelipitishia kwa pembeni hivyo maji yakijaa bila hata kufika juu,yanakuta lile bomba then tatizo linaanzia hapo

Tumia hiyo njia utajionea mwenyewe
 
Kwanini karo la choo linajaa haraka nifanyenini kisiwe kinajaa haraka?

Kama ambavo mada inajieleza hapo juu,

Naomba ushauri wako wa hali na mali, shimo au karo la choo changu kilijaa miaka 5 ya kukitumia nikaita wale wanao nyonya na magari wakakafanya hiyo kazi na kikawa kitupu kama mwanzo.

Cha ajabu baada ya kukitumia kwa mwaka 1 na nusu tu kimejaa tena wakati idadi ya familia yaani watu hawajaongezeka nilitegemea itachukua tena angalau miaka mingine hata 4 au 3 kuja kujaa, sasa nimetumia mwaka 1½ tu kimejaa, tatizo ni nini na nini nifanye ili angalau kisiwe kinajaa haraka hivo?

Ukinisaidia ushauri na mbinu za kufanya utakuwa umewasidia na wengine ambao wanapitia mada hii ahsanteni sana na samahani kwa usumbufu.

Karibuni sana.
Hongereni kwa kujaza choo
 
4 Years later.Haya mlete mada tunaomba mrejesho wa ulichofanya, wengine tuna the same problem as we speak.
 
nimejenga sehemu yenye muinuko udongo wake ukifika chini kama 5m unakutana na mfinyani.nimekutana na kisanga kama hiki,sasa hivi shimo hata ukioga unaona linamwaga maji kwa njee na harufu hadi kero.
Ngoja naweza kupata suluhisho hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom