Nifanye nini ili nisimkumbuke? Ananiumiza sana

Ulipoenda chuo ulifata vitu 2, ukasomea degree yako lakini pia ukasomea mahusiano na huyo jamaa.
Jamaa ashajua unampenda na anhaweza kwambia chochote ukakubali.

Labda uende kwa wale washauri wa mahusiano, naonaga wanavusha watu kwenye nyakati ngumu kama yako.
Kuja jamaa fb wanamuita idd makengo(kama sijakosea), huwa anasifika kwa hizo mambo.
Jaribu huko.
 
yumwema ushauri wangu usimtafute mwanamume mwingine haraka haraka ili ufute maumivu unayopitia au ili umkomoe ex wako, hapo unajidanganya

Mara nyingi wanaofanya maamuzi wakiwa katika hali kama hiyo wanafanya kwa kupanick utajikuta umeangukia kwa mtu asiye sahihi tena.

Take your time, choose wisely
yumwema fata huu ushauri utakuja kushukuru badae,,ukiparamia mahusiano haraka haraka utaangukia pabaya zaidi.
 
Dada let it go!
Time is a good healer. Huyo jamaa hakupendi na havutiki nawe kimuonekano lakini anaamini fika kuwa wewe na material wife.
Muombe Mungu ipo siku atakuonesha aliyekuandalia kwajili yako.
 
Ya kimafia sana hii yani unaumia unakaza moyo ila yy sasa ataumia mwaka mzima. Hii mbinu uwe umeshachunguza na una uhakika jamaa ana mtu pembeni na anaonyesha dalili ya kukuacha basi fastaaaa unamute.
Hauja kutana na mnyama Miles ...ukisha ona nina mtu mwingine na umejua ....we jua tu kuwa ukifanya hivyo utakua imenirahisishia sana zoezi la kuachana na wewe.

Kwa sababu wanaume baadhi yetu tunaliogopa sana chozi la mwanamke asie na hatia .

Yaani mwanamke ambaye tukiachana anaanza kumlilia Mungu huyu ataniweza.

Ila akianza kinituna na kunionesha unyang,au kiwa nina kibamia na mengine ya dizaini hiyo hapa utakua umenipa kichwa na ahueni sana.
 
Asanteeniii Sana wanajukwaa kwa ushauri wenu ,,kiukweli kabla nilikua naona ninamzigo wa mawazo Sana moyo ulikua unavuja damu lakin baada ya kupitia mawazo yenu naona kunawepesi fulani nimeupata . asanteeeni kwa wote mlio lipokea na kunishauri mzurii na wale wote walio toa ushauri kwa kukejel na kucheka ,,wote nawapenda Sana sana
 
Pole, siku nyingine ujue kuna tofauti kati ya mume na bwana japo wote ni wanaume,usimpe bwana haki za mume, na usimpe mume haki za bwana, haki za mume zinalindwa na mkataba wa ndoa, sheria za Mungu na sheria za nchi na mtazamo wa kijamii.
 
Dah poleh sana n n ngum kwa kweli kumsahau labda upate mtu ataekupenda zaidi ya yy
 
Utamsahau tu, wengine tulipenda tukaingia kwa miguu yote ila matokeo yake yalikua maumivu makubwa,miezi kumi na moja sasa tangu niamue kuwa it's over,niliacha aende zake.
 
Inauma sana jamni bhc tu [emoji24][emoji24][emoji24] ukiangalia mtu unampenda Sana lakin anakutesa kisaikolojia adi kazi unashindwa kufanya kwa weledi , inanitesa Sana mm
Hivi bado kuna akina dada wanaopenda kama wewe?
 
Utamsahau tu, wengine tulipenda tukaingia kwa miguu yote ila matokeo yake yalikua maumivu makubwa,miezi kumi na moja sasa tangu niamue kuwa it's over,niliacha aende zake.
Naamini na mm nitakua poa tu
 
Hivi bado kuna akina dada wanaopenda kama wewe?
Nipo ala nadhani nilikosea kumpenda naamnin ningempata wa kuthamin upendo wangu angeenjoy Sana ,,bhc tu nimeishia kua single[emoji24][emoji24][emoji24]
 
kwanza pole kwa unayopitia,tatizo kubwa kwa upande wako umempa nafasi kubwa kuliko unavyojipa wewe binafsi ni wakati wa kubatizwa upya na kuwa na msimamo thabiti.
N.B:Wanaume wazuri wapo huwezi jua mungu amepanga nini!
 
Habari zenu wana jukwaa wa JF, nombeni ushauri jamani, nifanyaje nimsahau huyu mwanaume?

Nilikuwa kwenye mahusiano na kaka mmoja jina sitomtaja tangu mwaka 2018, tumedumu vizurii kabisa toka kipindi hicho tupo chuo mpaka tukamaliza. Baada ya kumaliza chuo kila mtu akaenda mkoani kwakwe japo mawasiliano yalikuwa vizuri kabisa, nauli natumiwa naenda kwake mpaka ikafika kipindi nikapata kazi mkoa aliyopo yeye.

Tukashukuru Mungu, maana mahusiano yetu yalizidi kuimarika kadri siku zinavyoenda. Kipindi hicho yeye anahangaika na biashara zake kuna muda anafilisika (mtaji unakufa), mimi natoa nusu ya mshahara wangu aongezee ili aendelee na biashara.

Tatizo likaja kipindi mambo yake yamemnyookea, akabadilika gafla akawa mtu wa wanawake sana, yaani sijui hata hiyo tabia aliitolea wapi?! Tena ikawa siyo kujificha ni waziwazi. Mara unamfumania anaomba msamaha anabadilika hata mwezi mmoja lakini anarudia tabia ileile!

Mwaka huu ilikuwa tarehe 24 mwezi wa kwanza, ilitokea kutoelewana naye baada ya mimi kuwa namfatilia kwanini anakuwa ananisaliti. Hapo ndiyo alinambia mimi na wewe basi, fanya mambo yako songa mbele sikuhitaji tena kwenye maisha yangu! nikiuliza sababu ni nini ananiambia tatizo lako unanifatilia sana na unasikiliza maneno ya watu wanakudanganya kuwa mimi naingiza wanawake huku ndani kwangu.

Nikasema sawa, kama kukuuliza ni shida basi naomba unisamehe kwasababu nakupenda sana, lakini akakataa. Nikaumia, nikalia na nikazoea nikaendelea na maisha mengine.

Ilivyofika mwezi wa tano akaanza kunitafuta akidai turudiane, nikawa na wasiwasi naye lakini ilivyofika tarehe 27 mwezi wa saba nikamsamehe nikarudiana naye, tukaendelea na mahusiano. Ahadi nyingi, nikawa nafurahia mahusiano lakini cha kushangaza mwezi huu tarehe 5 akabadilika gafla.

Mawasiliano ni mchana tu akiwa kazini, usiku hapokei simu wala hajibu ujumbe na muda mwingine nalimwa 'block'. Ilivofika tarehe 8 akanambia kunamwanamke mwingine ameenda kwakwe na amekataa kuondoka hivyo mimi nisijaribu kwenda kwake, na nikienda tu yeye atahama hapo anapoishi au mkoa kabisa atahama, na nikijaribu tu hiyo ndiyo itakuwa tiketi ya mimi na yeye kuachana.

Aisee ndugu zanguni, mpaka leo nashindwa kuzoea! Nimelazwa hospitali na dripu za maji juu lakini nashindwa kumsahau.

Naomba mnisaidie namna ya kumsahau.
Kama upo serious, njoo DM nikupe mbinu. Watu tulishapita huko zamani sana. Nakuelewa, ni ngumu sana, inahitaji techniques.
 
Aiseee Pole,kwani amekuwa mtoto wa dandu au super danger mpaka ushindwe kumsahau? Move on achana na 'EMpty Head" huyo.
 
Huu ni kama ubatizo wa Moto wa kuingia utu uzima [emoji1787][emoji1787] sitasahau ule mwaka mapenzi konyo.
 
Tatizo hamweki picha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom