Nifanye nini ili nisimkumbuke? Ananiumiza sana

yumwema

Member
Nov 10, 2022
30
45
Habari zenu wana jukwaa wa JF, nombeni ushauri jamani, nifanyaje nimsahau huyu mwanaume?

Nilikuwa kwenye mahusiano na kaka mmoja jina sitomtaja tangu mwaka 2018, tumedumu vizurii kabisa toka kipindi hicho tupo chuo mpaka tukamaliza. Baada ya kumaliza chuo kila mtu akaenda mkoani kwakwe japo mawasiliano yalikuwa vizuri kabisa, nauli natumiwa naenda kwake mpaka ikafika kipindi nikapata kazi mkoa aliyopo yeye.

Tukashukuru Mungu, maana mahusiano yetu yalizidi kuimarika kadri siku zinavyoenda. Kipindi hicho yeye anahangaika na biashara zake kuna muda anafilisika (mtaji unakufa), mimi natoa nusu ya mshahara wangu aongezee ili aendelee na biashara.

Tatizo likaja kipindi mambo yake yamemnyookea, akabadilika gafla akawa mtu wa wanawake sana, yaani sijui hata hiyo tabia aliitolea wapi?! Tena ikawa siyo kujificha ni waziwazi. Mara unamfumania anaomba msamaha anabadilika hata mwezi mmoja lakini anarudia tabia ileile!

Mwaka huu ilikuwa tarehe 24 mwezi wa kwanza, ilitokea kutoelewana naye baada ya mimi kuwa namfatilia kwanini anakuwa ananisaliti. Hapo ndiyo alinambia mimi na wewe basi, fanya mambo yako songa mbele sikuhitaji tena kwenye maisha yangu! nikiuliza sababu ni nini ananiambia tatizo lako unanifatilia sana na unasikiliza maneno ya watu wanakudanganya kuwa mimi naingiza wanawake huku ndani kwangu.

Nikasema sawa, kama kukuuliza ni shida basi naomba unisamehe kwasababu nakupenda sana, lakini akakataa. Nikaumia, nikalia na nikazoea nikaendelea na maisha mengine.

Ilivyofika mwezi wa tano akaanza kunitafuta akidai turudiane, nikawa na wasiwasi naye lakini ilivyofika tarehe 27 mwezi wa saba nikamsamehe nikarudiana naye, tukaendelea na mahusiano. Ahadi nyingi, nikawa nafurahia mahusiano lakini cha kushangaza mwezi huu tarehe 5 akabadilika gafla.

Mawasiliano ni mchana tu akiwa kazini, usiku hapokei simu wala hajibu ujumbe na muda mwingine nalimwa 'block'. Ilivofika tarehe 8 akanambia kunamwanamke mwingine ameenda kwakwe na amekataa kuondoka hivyo mimi nisijaribu kwenda kwake, na nikienda tu yeye atahama hapo anapoishi au mkoa kabisa atahama, na nikijaribu tu hiyo ndiyo itakuwa tiketi ya mimi na yeye kuachana.

Aisee ndugu zanguni, mpaka leo nashindwa kuzoea! Nimelazwa hospitali na dripu za maji juu lakini nashindwa kumsahau.

Naomba mnisaidie namna ya kumsahau.
 
Habari zenu wana jukwaa wa jf,,
Naombeni ushauri jamn nifanyaje nimsahau huyu mwanaume? Nilikua kwenye mahusian na kaka mmoja jina sitomtaja tangu mwaka 2018 tumedumu vizurii kabisa toka kipindi hicho tupo chuo mpka tukamaliza ,baada ya kumaliza chuo kilamtu akaenda mkoani kwakwe japo mawasiliano yalikua vjzuri kabisa nauli natumiwa naenda kwake mpaka ikafika kipindi uzoea nimelazwa hospital na drip za maji juu lakin nashindwa kumsahau ,,naomba mnisaidie namna ya kumsahau
Umeniumiza sana na mimi.

Si Kwa hali unayopitia bali kunisomesha hadithi yote bila ya nukta wala mkato.

Yaani unatakiwa usome bila kuhema au kufumba macho au kumeza mate.

Natamani ninge-attach sauti namna ya kusoma kisa cha binti yetu.

Nipo hospital. Nimekosa pumzi. Tuendelee kupata drip wote.
 
Pole
 
Mbona kila kitu kipo wazi jamaa kaoa wew alikuwa anakutumia tuu kama daraja avuke na kwa bahati mbaya ame gundua wew ni mbovu kihisia juu yake so Ana kufanya anavyo taka yeye....

Huna thaman kwenye maisha yake anaishi na wew kwa mazoea tuu na baadhi ya vitu ananufaika nawe

Kingine anakuonea wivu ndio mana anakurudia rudia kila wakati

... Sasa unacho takiwa ni kujitambua kutumia akili kuliko hisia usipo sikia utaambulia ukimw kutoka kwake wana ume kila kukicha wapo wana tafuta wana wake we Una kumbatia jitu
Unakosa watu muhim kwenye maisha yako

Pole Sana binti
 
Pole sana yumwema. Inauma mno mno mno. Kwanza kabisa huyo inawezekana ndiye chaguo lako la Mungu. Kaa kwa imani yako muulize Mungu kama ni yeye kweli Mungu alimleta kwako.

Nafsi ikisema hapana basi jipe muda, funga na kusali kwa muda wa siku saba utaona matokeo, utamsahau kabisa
 
Mbona kila kitu kipo wazi jamaa kaoa wew alikuwa anakutumia tuu kama daraja avuke na kwa bahati mbaya ame gundua wew ni mbovu kihisia juu yake so Ana kufanya anavyo taka yeye....

Huna thaman kwenye maisha yake anaishi na wew kwa mazoea tuu na baadhi ya vitu ananufaika nawe

Kingine anakuonea wivu ndio mana anakurudia rudia kila wakati

... Sasa unacho takiwa ni kujitambua kutumia akili kuliko hisia usipo sikia utaambulia ukimw kutoka kwake wana ume kila kukicha wapo wana tafuta wana wake we Una kumbatia jitu
Unakosa watu muhim kwenye maisha yako

Pole Sana binti
Asantee kwa ushauri nimekuelewa
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom