Nifanye nini ili nisimkumbuke? Ananiumiza sana

[emoji23] mm nilikua najionaga mjanja ila kuna sehemu nikaja kamatika wee niliteseka. Toka siku ile huwa siwacheki watu yakiwakuta sababu naelewa.
Pole sana rafiki
 
Uachie moyo kazi ya kusukuma damu, usiweke watu huko mama...
 
Basi awe makini sana sababu najua kwa sasa ni mpweke, huo upweke unaweza kumfanya akawa na mtu ilimradi tu kumbe kabugi mara mbili.
Namshauri awe na mtu tu wacheki afya anyanduane kwa uhuru kama sehemu ya kutoa stress kwa kipindi hiki kwanza. after time asettle mambo yake vizuri ampate mume sahihi lakini akisema akae tuu kumbukukumbu zitajirudia za huyo mwanaume. afanye hivyo
 
Pole kwanza na changamoto za mahusiano,nina jambo moja tu la kukwambia IFANYE AKILI YAKO IFANYE KAZI na SIO HISIA ZAKO_wapo wanaume wengi wanatafuta mwanamke kama wa aina ya yako na hawawapati_Dada yangu kumbuka MUDA na UMRI wako ni wa thamani sana na ukiendelea kuupoteza UTAJUTA HUKO MBELENI..Fanya maamuzi magumu!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inauma sana jamni bhc tu [emoji24][emoji24][emoji24] ukiangalia mtu unampenda Sana lakin anakutesa kisaikolojia adi kazi unashindwa kufanya kwa weledi , inanitesa Sana mm
Iyo ni laana ya kula nauli za wanaume wengine yumwema
 
Futa kila kilicho chake, Fanya mambo yako, vaa vizuri, kula vizuri, kunywa maji kwa wingi usisahau na matunda ipo siku utakutana na anayejua thamani yako. Tatizo lako unajishusha sana na kutumia sana hisia kuliko akili. Ilikuwa lazima ujifunze mahusiano Kwa njia ngumu kama hiyo ili ukomae vizuri.
 
Kukaa single kunaumiza mala mbili zaidi, unataka kusema huna mwanaume wa back-up ?
 
Habari zenu wana jukwaa wa JF, nombeni ushauri jamani, nifanyaje nimsahau huyu mwanaume?

Nilikuwa kwenye mahusiano na kaka mmoja jina sitomtaja tangu mwaka 2018, tumedumu vizurii kabisa toka kipindi hicho tupo chuo mpaka tukamaliza. Baada ya kumaliza chuo kila mtu akaenda mkoani kwakwe japo mawasiliano yalikuwa vizuri kabisa, nauli natumiwa naenda kwake mpaka ikafika kipindi nikapata kazi mkoa aliyopo yeye.

Tukashukuru Mungu, maana mahusiano yetu yalizidi kuimarika kadri siku zinavyoenda. Kipindi hicho yeye anahangaika na biashara zake kuna muda anafilisika (mtaji unakufa), mimi natoa nusu ya mshahara wangu aongezee ili aendelee na biashara.

Tatizo likaja kipindi mambo yake yamemnyookea, akabadilika gafla akawa mtu wa wanawake sana, yaani sijui hata hiyo tabia aliitolea wapi?! Tena ikawa siyo kujificha ni waziwazi. Mara unamfumania anaomba msamaha anabadilika hata mwezi mmoja lakini anarudia tabia ileile!

Mwaka huu ilikuwa tarehe 24 mwezi wa kwanza, ilitokea kutoelewana naye baada ya mimi kuwa namfatilia kwanini anakuwa ananisaliti. Hapo ndiyo alinambia mimi na wewe basi, fanya mambo yako songa mbele sikuhitaji tena kwenye maisha yangu! nikiuliza sababu ni nini ananiambia tatizo lako unanifatilia sana na unasikiliza maneno ya watu wanakudanganya kuwa mimi naingiza wanawake huku ndani kwangu.

Nikasema sawa, kama kukuuliza ni shida basi naomba unisamehe kwasababu nakupenda sana, lakini akakataa. Nikaumia, nikalia na nikazoea nikaendelea na maisha mengine.

Ilivyofika mwezi wa tano akaanza kunitafuta akidai turudiane, nikawa na wasiwasi naye lakini ilivyofika tarehe 27 mwezi wa saba nikamsamehe nikarudiana naye, tukaendelea na mahusiano. Ahadi nyingi, nikawa nafurahia mahusiano lakini cha kushangaza mwezi huu tarehe 5 akabadilika gafla.

Mawasiliano ni mchana tu akiwa kazini, usiku hapokei simu wala hajibu ujumbe na muda mwingine nalimwa 'block'. Ilivofika tarehe 8 akanambia kunamwanamke mwingine ameenda kwakwe na amekataa kuondoka hivyo mimi nisijaribu kwenda kwake, na nikienda tu yeye atahama hapo anapoishi au mkoa kabisa atahama, na nikijaribu tu hiyo ndiyo itakuwa tiketi ya mimi na yeye kuachana.

Aisee ndugu zanguni, mpaka leo nashindwa kuzoea! Nimelazwa hospitali na dripu za maji juu lakini nashindwa kumsahau.

Naomba mnisaidie namna ya kumsahau.
Sio kosa lake shida ni wewe unampenda sana huyo jamaa. Unapenda usipopendwa.
 
Acha mba mba mba nyingi endelea na maisha yako, FUTA picha na kumbukumbu zake zingine zote ulizo nazo,

usi wasiliane nae kwa namna yoyote ile ukikutana nae msalimie kwa mbali tuu usimsogelee kabisa, baada ya miezi mi 3 utaanza kumwondoa akilini kwako taratibu bila kutumia nguvu,

Nb: usimchukie
 
Ameshakuona wewe ni bwege mtozeni.
Kupenda ni kitu kingine aisee asikwambie mtu, huyu bidada alikuwa anatoa nusu ya mshahara wake kussuport biashara ya mpenzi wake kwa sababu alimpenda sana sio ubwege

Kuna wadau wamemshauri vizuri hayo maumivu anayopitia ya kusalitiwa na mtu anayempenda yataisha mdogo mdogo ajipe muda tu
 
Habari zenu wana jukwaa wa JF, nombeni ushauri jamani, nifanyaje nimsahau huyu mwanaume?

Nilikuwa kwenye mahusiano na kaka mmoja jina sitomtaja tangu mwaka 2018, tumedumu vizurii kabisa toka kipindi hicho tupo chuo mpaka tukamaliza. Baada ya kumaliza chuo kila mtu akaenda mkoani kwakwe japo mawasiliano yalikuwa vizuri kabisa, nauli natumiwa naenda kwake mpaka ikafika kipindi nikapata kazi mkoa aliyopo yeye.

Tukashukuru Mungu, maana mahusiano yetu yalizidi kuimarika kadri siku zinavyoenda. Kipindi hicho yeye anahangaika na biashara zake kuna muda anafilisika (mtaji unakufa), mimi natoa nusu ya mshahara wangu aongezee ili aendelee na biashara.

Tatizo likaja kipindi mambo yake yamemnyookea, akabadilika gafla akawa mtu wa wanawake sana, yaani sijui hata hiyo tabia aliitolea wapi?! Tena ikawa siyo kujificha ni waziwazi. Mara unamfumania anaomba msamaha anabadilika hata mwezi mmoja lakini anarudia tabia ileile!

Mwaka huu ilikuwa tarehe 24 mwezi wa kwanza, ilitokea kutoelewana naye baada ya mimi kuwa namfatilia kwanini anakuwa ananisaliti. Hapo ndiyo alinambia mimi na wewe basi, fanya mambo yako songa mbele sikuhitaji tena kwenye maisha yangu! nikiuliza sababu ni nini ananiambia tatizo lako unanifatilia sana na unasikiliza maneno ya watu wanakudanganya kuwa mimi naingiza wanawake huku ndani kwangu.

Nikasema sawa, kama kukuuliza ni shida basi naomba unisamehe kwasababu nakupenda sana, lakini akakataa. Nikaumia, nikalia na nikazoea nikaendelea na maisha mengine.

Ilivyofika mwezi wa tano akaanza kunitafuta akidai turudiane, nikawa na wasiwasi naye lakini ilivyofika tarehe 27 mwezi wa saba nikamsamehe nikarudiana naye, tukaendelea na mahusiano. Ahadi nyingi, nikawa nafurahia mahusiano lakini cha kushangaza mwezi huu tarehe 5 akabadilika gafla.

Mawasiliano ni mchana tu akiwa kazini, usiku hapokei simu wala hajibu ujumbe na muda mwingine nalimwa 'block'. Ilivofika tarehe 8 akanambia kunamwanamke mwingine ameenda kwakwe na amekataa kuondoka hivyo mimi nisijaribu kwenda kwake, na nikienda tu yeye atahama hapo anapoishi au mkoa kabisa atahama, na nikijaribu tu hiyo ndiyo itakuwa tiketi ya mimi na yeye kuachana.

Aisee ndugu zanguni, mpaka leo nashindwa kuzoea! Nimelazwa hospitali na dripu za maji juu lakini nashindwa kumsahau.

Naomba mnisaidie namna ya kumsahau.
Nitafute PM nikutulize bible! Vijana wa siku hizi hawajui kulea!
 
yumwema ushauri wangu usimtafute mwanamume mwingine haraka haraka ili ufute maumivu unayopitia au ili umkomoe ex wako, hapo unajidanganya

Mara nyingi wanaofanya maamuzi wakiwa katika hali kama hiyo wanafanya kwa kupanick utajikuta umeangukia kwa mtu asiye sahihi tena.

Take your time, choose wisely
 
Back
Top Bottom