Nifanye nini ili nisimkumbuke? Ananiumiza sana

Habari zenu wana jukwaa wa JF, nombeni ushauri jamani, nifanyaje nimsahau huyu mwanaume?

Nilikuwa kwenye mahusiano na kaka mmoja jina sitomtaja tangu mwaka 2018, tumedumu vizurii kabisa toka kipindi hicho tupo chuo mpaka tukamaliza. Baada ya kumaliza chuo kila mtu akaenda mkoani kwakwe japo mawasiliano yalikuwa vizuri kabisa, nauli natumiwa naenda kwake mpaka ikafika kipindi nikapata kazi mkoa aliyopo yeye.

Tukashukuru Mungu, maana mahusiano yetu yalizidi kuimarika kadri siku zinavyoenda. Kipindi hicho yeye anahangaika na biashara zake kuna muda anafilisika (mtaji unakufa), mimi natoa nusu ya mshahara wangu aongezee ili aendelee na biashara.

Tatizo likaja kipindi mambo yake yamemnyookea, akabadilika gafla akawa mtu wa wanawake sana, yaani sijui hata hiyo tabia aliitolea wapi?! Tena ikawa siyo kujificha ni waziwazi. Mara unamfumania anaomba msamaha anabadilika hata mwezi mmoja lakini anarudia tabia ileile!

Mwaka huu ilikuwa tarehe 24 mwezi wa kwanza, ilitokea kutoelewana naye baada ya mimi kuwa namfatilia kwanini anakuwa ananisaliti. Hapo ndiyo alinambia mimi na wewe basi, fanya mambo yako songa mbele sikuhitaji tena kwenye maisha yangu! nikiuliza sababu ni nini ananiambia tatizo lako unanifatilia sana na unasikiliza maneno ya watu wanakudanganya kuwa mimi naingiza wanawake huku ndani kwangu.

Nikasema sawa, kama kukuuliza ni shida basi naomba unisamehe kwasababu nakupenda sana, lakini akakataa. Nikaumia, nikalia na nikazoea nikaendelea na maisha mengine.

Ilivyofika mwezi wa tano akaanza kunitafuta akidai turudiane, nikawa na wasiwasi naye lakini ilivyofika tarehe 27 mwezi wa saba nikamsamehe nikarudiana naye, tukaendelea na mahusiano. Ahadi nyingi, nikawa nafurahia mahusiano lakini cha kushangaza mwezi huu tarehe 5 akabadilika gafla.

Mawasiliano ni mchana tu akiwa kazini, usiku hapokei simu wala hajibu ujumbe na muda mwingine nalimwa 'block'. Ilivofika tarehe 8 akanambia kunamwanamke mwingine ameenda kwakwe na amekataa kuondoka hivyo mimi nisijaribu kwenda kwake, na nikienda tu yeye atahama hapo anapoishi au mkoa kabisa atahama, na nikijaribu tu hiyo ndiyo itakuwa tiketi ya mimi na yeye kuachana.

Aisee ndugu zanguni, mpaka leo nashindwa kuzoea! Nimelazwa hospitali na dripu za maji juu lakini nashindwa kumsahau.

Naomba mnisaidie namna ya kumsahau.
Wanawake kama nyie ni wachache Sana na Huwa mnaangukia pabaya...
 
itabidi ifike hatua ukubaliane na ukweli tu miaka minne alokupotezea sio mingi sana,emu fanya hivi kipindi hiki emu nunua kiwanja afu anza kujenga kwa mshahara wako
 
Ilikua lazima upitie huu ubatizo wa moto ili akili yako ikae sawa kuhusu mahusiano, mimi nilipigwa na kitu chembamba sana chenye ncha kali nikajifunza mambo mengi. Vijue vitu vinavyo kupa amani na furaha alafu penda kuvifanya hata kwa uchache, usiweke bond ya furaha yako kwa jitu lolote lile ambalo muda wowote linaweza kukubadilikia.
 
Habari zenu wana jukwaa wa JF, nombeni ushauri jamani, nifanyaje nimsahau huyu mwanaume?

Nilikuwa kwenye mahusiano na kaka mmoja jina sitomtaja tangu mwaka 2018, tumedumu vizurii kabisa toka kipindi hicho tupo chuo mpaka tukamaliza. Baada ya kumaliza chuo kila mtu akaenda mkoani kwakwe japo mawasiliano yalikuwa vizuri kabisa, nauli natumiwa naenda kwake mpaka ikafika kipindi nikapata kazi mkoa aliyopo yeye.

Tukashukuru Mungu, maana mahusiano yetu yalizidi kuimarika kadri siku zinavyoenda. Kipindi hicho yeye anahangaika na biashara zake kuna muda anafilisika (mtaji unakufa), mimi natoa nusu ya mshahara wangu aongezee ili aendelee na biashara.

Tatizo likaja kipindi mambo yake yamemnyookea, akabadilika gafla akawa mtu wa wanawake sana, yaani sijui hata hiyo tabia aliitolea wapi?! Tena ikawa siyo kujificha ni waziwazi. Mara unamfumania anaomba msamaha anabadilika hata mwezi mmoja lakini anarudia tabia ileile!

Mwaka huu ilikuwa tarehe 24 mwezi wa kwanza, ilitokea kutoelewana naye baada ya mimi kuwa namfatilia kwanini anakuwa ananisaliti. Hapo ndiyo alinambia mimi na wewe basi, fanya mambo yako songa mbele sikuhitaji tena kwenye maisha yangu! nikiuliza sababu ni nini ananiambia tatizo lako unanifatilia sana na unasikiliza maneno ya watu wanakudanganya kuwa mimi naingiza wanawake huku ndani kwangu.

Nikasema sawa, kama kukuuliza ni shida basi naomba unisamehe kwasababu nakupenda sana, lakini akakataa. Nikaumia, nikalia na nikazoea nikaendelea na maisha mengine.

Ilivyofika mwezi wa tano akaanza kunitafuta akidai turudiane, nikawa na wasiwasi naye lakini ilivyofika tarehe 27 mwezi wa saba nikamsamehe nikarudiana naye, tukaendelea na mahusiano. Ahadi nyingi, nikawa nafurahia mahusiano lakini cha kushangaza mwezi huu tarehe 5 akabadilika gafla.

Mawasiliano ni mchana tu akiwa kazini, usiku hapokei simu wala hajibu ujumbe na muda mwingine nalimwa 'block'. Ilivofika tarehe 8 akanambia kunamwanamke mwingine ameenda kwakwe na amekataa kuondoka hivyo mimi nisijaribu kwenda kwake, na nikienda tu yeye atahama hapo anapoishi au mkoa kabisa atahama, na nikijaribu tu hiyo ndiyo itakuwa tiketi ya mimi na yeye kuachana.

Aisee ndugu zanguni, mpaka leo nashindwa kuzoea! Nimelazwa hospitali na dripu za maji juu lakini nashindwa kumsahau.

Naomba mnisaidie namna ya kumsahau.
Jifanye kafa
 
Back
Top Bottom