Nicolae Ceauşescu: Swahiba wa Julius Nyerere, Rais wa Romania na mjamaa kindakindaki aliyeuawa kifo cha kumiminiwa risasi na wanajeshi (Firing Squad)

Nicolae Ceauşescu: Swahiba wa Julius Nyerere, Rais wa Romania na mjamaa kindakindaki aliyeuawa kifo cha kumiminiwa risasi na wanajeshi (Execution by Firing Squad )

Nicolae Ceausescu akiwa pamoja na mzee Rashidi Mfaume Kawawa.

View attachment 1563431

Picha kadhaa zilizopigwa kwa kukosa utaalam mahususi zinaonyesha hali ya watu kutoamini kile kinachoendelea katika chumba kidogo wakati ambao ndugu Nicolae na Elena Ceausescu, mtu na mkewe, walioitawala Romania kwa zaidi ya miaka 24, walipokuwa wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya kijeshi (Military Tribunal) katika kambi yao mnamo mwezi Desemba 25, mwaka 1989.

Nicolae Ceausescu akiwa na mzee Ali Hassan Mwinyi.

(Mzee Mwinyi Mungu azidi kukupa afya njema, maisha marefu na baraka tele kwa maana ulizungumza kwa hekima na busara nyingi katika msiba wa mzee Mkapa kule kijijini Lupaso Masasi. Tanzania hii bado inahitaji wazee kama wewe)

Siku tatu kabla walikuwa bado na matumaini ya kuendelea kukandamiza maandamano makubwa yaliyoandaliwa na watu wao waliokuwa wamezama katika dimbwi zito la umasikini wa kutupwa, lakini hatimaye walisimamishwa kizimbani wakituhumiwa kwa mauaji ya kimbari, wazee wawili (Nicolae na Elena Ceausescu) walikuwa wamevaa makoti ya bei ghali ambayo yalikuwa ni mtego wa mwisho wa utawala wao.

Kuna baadhi ya picha kutoka katika makumbusho ya taifa zinaonyesha hao akina Ceausescus, wakiwa amepigwa na bumbuwazi lakini wakionesha ukaidi, wakiwatazama maafisa wa jeshi waliojazana kwenye chumba hicho, kwa askari anayeshikilia Kalashnikov aliyekuwa analinda mlango, na kwa mtu aliyesimama kuwahutubia akiwa amevaa suruali ya jeans na sweta nene la jeusi na kitambaa kilichokuwa na rangi za bendera ya Romania kilichovingirishwa mkononi mwake.

Dani Voinea alikuwa mwendesha mashtaka wa kijeshi ambaye alikuwa ameamriwa kuandaa mashtaka dhidi ya akina Ceausescus. Alisafiri kwa helikopta kutoka Bucharest hadi kambi ya Targoviste umbali wa takriban kilomita 80 ili kuipeleka hati ile ya mashtaka katika kesi hii iliyokuwa inaonekana kama vile ni ya maigizo tu iliyopangwa haraka haraka.

Shtaka kuu lilikuwa mauaji ya kimbari - ingawa haikujulikana ikiwa vifo hivyo vyote vya watu 60,000 ambavyo walituhumiwa kusababisha vilitokea wakati wa siku zile nne za mapinduzi au katika utawala wao wote - na adhabu waliopewa ilikuwa ni kuuwawa na kupigwa risasi.

Voinea alitoa hati ya kukamatwa kwa hao akina Ceausescus. Katika makao makuu ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti ilikutwa hati kutoka mwezi Desemba 17 na 19 ambapo Ceausescu aliamuru wanajeshi kufyatua risasi kwa waandamanaji huko Timisoara, jiji la magharibi ambalo mapinduzi yalianza kabla ya kulipuka huko jijini Bucharest mnamo mwezi Desemba tarehe 21.

Nicolae aliamuru maelfu ya watu kutiwa mbaroni na kupelekwa katika magereza, ambapo walipigwa. Kuzuiliwa kinyume cha sheria na mauaji ya wapinzani wa kisiasa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu na waliadhibiwa wakati huo na kifo. Kwa hivyo hii ndiyo dhana ya kisheria ambayo ilitumikia kutoa hukumu ile ya kifo.

Kesi hiyo ilifanyika katika mazingira ya taharuki, machafuko na hofu kubwa: karibu watu 250 walikuwa wameuawa na 1,000 waliumia katika mapigano na vikosi vya usalama kabla ya akina Ceausescus kukimbia Bucharest mnamo Desemba 22. Karibu wengine 900 walikufa na 2,150 waliumia katika vurugu za machafuko ambazo zilifuata kabla ya kukamatwa kwao siku hiyo hiyo.

Kikundi cha wanasiasa wachache wa kikomunisti na maafisa wa jeshi wanaojiita National Salvation Front (NSF) waliingia walipoona kuna mwanya wa kiuongozi na walidai kupigania haki za watu dhidi ya "magaidi" na vikosi vya siri vya waliokuwa wanamuunga mkono ndugu Ceausescu; ilikuwa kundi hili lililoamuru kuundwa kwa mahakama ya kijeshi huko Targoviste dhidi ya Nicolae na mkewe.

Watu walikuwa wakifa kila siku mitaani, ripoti za hujuma za 'kigaidi' zilikuwa zimeanza. . . na waandamanaji walikuwa wakidai kwamba Ceausescus ashtakiwe. Watu waliwachukia, kwa sababu walikuwa wamepokea hisia hizo za chuki kutoka waandamanaji wa mitaani. . . Nicolae alikuwa ameamuru watu wasio na silaha wapigwe risasi, watu ambao hawakuchukua wala kubeba hata kisu na walikuwa wakipigia kelele wakidai uhuru tu, na sio hata mkate, bali kuwa huru tu ndio dai lao kuu.

Ceausescu (aliyekuwa na umri wa miaka 71 wakati ule) aliishutumu mahakama ile kwa kuzusha tuhuma za uongo na akasema atakuwa tayari kuwajibika kwa bunge la Romania pekee, na wala yeye wala Elena (mkewe aliyekuwa na umri wa miaka 73 kwa wakati ule) - kiongozi mwenzake ambaye alikuwa kama vile naibu waziri mkuu tangu mwaka 1980 - hakuonyesha ishara yoyote ya kujutia maovu yake.

Elena aliendelea kutaka kuingilia kati na kukatisha kesi lakini Nicolae alikuwa anaweka mkono wake mdomoni mwa Elena ili kumfunga asiongee. Walionekana kufikiria kesi hiyo ilikuwa kwa sababu ya kuonekana tu na hakuna chochote kitakachotokea kwao. Punde tu wakati mikono yao ilipofungwa na kutolewa kwa nguvu ndipo walipoanza kupiga makelele.

Voinea alikuwa ameodnoka katika chumba kile cha mahakama kabla ya majaji wa jeshi kutoa uamuzi ambao wengi walikuwa wanautegemea wa kukutwa na hatia, na alikuwa amefika nje ya mahakama ile kabla kelele hazijamfanya ageuke. Wanajeshi kadhaa walikuwa wakimchukua Ceausescu nje na kumburuta chini kwa pamoja. . . Askari waliwasukuma ukutani na walipokuwa wakirudi nyuma walianza kupiga risasi.

Kwa kweli lilikuwa ni tukio la kushangaza sana. Ilikuwa ni tukio la kwanza la utekelezaji wa maujai dhidi ya kiongozi mkuu kabisa katika nchi na sio kitu ambacho kinaweza kusahaulika kirahisi kwa watu wa Romania.du aisee

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Causesco ni kielelezo cha hatari ya kutumia POLISI/JESHI kunyanyasa wananchi ....palitokea maandamano Romania ...akatuma polisi wakashindwa akaagiza Jeshi wakatumia sana nguvu ikashindikana ...option ya mwisho ikawa kuwatishia kuwakanyaga na vifaru nayo wananchi wakagoma .....wakajaribu kwaponda wachache na bado waliokuwa nyuma hawakukimbia ......damu zinamwagika ..
Polisi na wanajeshi wakaruka kwenye vifaru na magari yao kwa hasira na uchungu wakakimbia kuelekea ikulu ....wakamkamata Causesco na kumpeleka bungeni kumshtaki kwa kuwauwa wananchi ...akajibu nyodo ...wakamtwanga risasi akafa
 
Nicolae Ceauşescu: Swahiba wa Julius Nyerere, Rais wa Romania na mjamaa kindakindaki aliyeuawa kifo cha kumiminiwa risasi na wanajeshi (Execution by Firing Squad )

Nicolae Ceausescu akiwa pamoja na mzee Rashidi Mfaume Kawawa.

View attachment 1563431

Picha kadhaa zilizopigwa kwa kukosa utaalam mahususi zinaonyesha hali ya watu kutoamini kile kinachoendelea katika chumba kidogo wakati ambao ndugu Nicolae na Elena Ceausescu, mtu na mkewe, walioitawala Romania kwa zaidi ya miaka 24, walipokuwa wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya kijeshi (Military Tribunal) katika kambi yao mnamo mwezi Desemba 25, mwaka 1989.

Nicolae Ceausescu akiwa na mzee Ali Hassan Mwinyi.

(Mzee Mwinyi Mungu azidi kukupa afya njema, maisha marefu na baraka tele kwa maana ulizungumza kwa hekima na busara nyingi katika msiba wa mzee Mkapa kule kijijini Lupaso Masasi. Tanzania hii bado inahitaji wazee kama wewe)

Siku tatu kabla walikuwa bado na matumaini ya kuendelea kukandamiza maandamano makubwa yaliyoandaliwa na watu wao waliokuwa wamezama katika dimbwi zito la umasikini wa kutupwa, lakini hatimaye walisimamishwa kizimbani wakituhumiwa kwa mauaji ya kimbari, wazee wawili (Nicolae na Elena Ceausescu) walikuwa wamevaa makoti ya bei ghali ambayo yalikuwa ni mtego wa mwisho wa utawala wao.

Kuna baadhi ya picha kutoka katika makumbusho ya taifa zinaonyesha hao akina Ceausescus, wakiwa amepigwa na bumbuwazi lakini wakionesha ukaidi, wakiwatazama maafisa wa jeshi waliojazana kwenye chumba hicho, kwa askari anayeshikilia Kalashnikov aliyekuwa analinda mlango, na kwa mtu aliyesimama kuwahutubia akiwa amevaa suruali ya jeans na sweta nene la jeusi na kitambaa kilichokuwa na rangi za bendera ya Romania kilichovingirishwa mkononi mwake.

Dani Voinea alikuwa mwendesha mashtaka wa kijeshi ambaye alikuwa ameamriwa kuandaa mashtaka dhidi ya akina Ceausescus. Alisafiri kwa helikopta kutoka Bucharest hadi kambi ya Targoviste umbali wa takriban kilomita 80 ili kuipeleka hati ile ya mashtaka katika kesi hii iliyokuwa inaonekana kama vile ni ya maigizo tu iliyopangwa haraka haraka.

Shtaka kuu lilikuwa mauaji ya kimbari - ingawa haikujulikana ikiwa vifo hivyo vyote vya watu 60,000 ambavyo walituhumiwa kusababisha vilitokea wakati wa siku zile nne za mapinduzi au katika utawala wao wote - na adhabu waliopewa ilikuwa ni kuuwawa na kupigwa risasi.

Voinea alitoa hati ya kukamatwa kwa hao akina Ceausescus. Katika makao makuu ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti ilikutwa hati kutoka mwezi Desemba 17 na 19 ambapo Ceausescu aliamuru wanajeshi kufyatua risasi kwa waandamanaji huko Timisoara, jiji la magharibi ambalo mapinduzi yalianza kabla ya kulipuka huko jijini Bucharest mnamo mwezi Desemba tarehe 21.

Nicolae aliamuru maelfu ya watu kutiwa mbaroni na kupelekwa katika magereza, ambapo walipigwa. Kuzuiliwa kinyume cha sheria na mauaji ya wapinzani wa kisiasa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu na waliadhibiwa wakati huo na kifo. Kwa hivyo hii ndiyo dhana ya kisheria ambayo ilitumikia kutoa hukumu ile ya kifo.

Kesi hiyo ilifanyika katika mazingira ya taharuki, machafuko na hofu kubwa: karibu watu 250 walikuwa wameuawa na 1,000 waliumia katika mapigano na vikosi vya usalama kabla ya akina Ceausescus kukimbia Bucharest mnamo Desemba 22. Karibu wengine 900 walikufa na 2,150 waliumia katika vurugu za machafuko ambazo zilifuata kabla ya kukamatwa kwao siku hiyo hiyo.

Kikundi cha wanasiasa wachache wa kikomunisti na maafisa wa jeshi wanaojiita National Salvation Front (NSF) waliingia walipoona kuna mwanya wa kiuongozi na walidai kupigania haki za watu dhidi ya "magaidi" na vikosi vya siri vya waliokuwa wanamuunga mkono ndugu Ceausescu; ilikuwa kundi hili lililoamuru kuundwa kwa mahakama ya kijeshi huko Targoviste dhidi ya Nicolae na mkewe.

Watu walikuwa wakifa kila siku mitaani, ripoti za hujuma za 'kigaidi' zilikuwa zimeanza. . . na waandamanaji walikuwa wakidai kwamba Ceausescus ashtakiwe. Watu waliwachukia, kwa sababu walikuwa wamepokea hisia hizo za chuki kutoka waandamanaji wa mitaani. . . Nicolae alikuwa ameamuru watu wasio na silaha wapigwe risasi, watu ambao hawakuchukua wala kubeba hata kisu na walikuwa wakipigia kelele wakidai uhuru tu, na sio hata mkate, bali kuwa huru tu ndio dai lao kuu.

Ceausescu (aliyekuwa na umri wa miaka 71 wakati ule) aliishutumu mahakama ile kwa kuzusha tuhuma za uongo na akasema atakuwa tayari kuwajibika kwa bunge la Romania pekee, na wala yeye wala Elena (mkewe aliyekuwa na umri wa miaka 73 kwa wakati ule) - kiongozi mwenzake ambaye alikuwa kama vile naibu waziri mkuu tangu mwaka 1980 - hakuonyesha ishara yoyote ya kujutia maovu yake.

Elena aliendelea kutaka kuingilia kati na kukatisha kesi lakini Nicolae alikuwa anaweka mkono wake mdomoni mwa Elena ili kumfunga asiongee. Walionekana kufikiria kesi hiyo ilikuwa kwa sababu ya kuonekana tu na hakuna chochote kitakachotokea kwao. Punde tu wakati mikono yao ilipofungwa na kutolewa kwa nguvu ndipo walipoanza kupiga makelele.

Voinea alikuwa ameodnoka katika chumba kile cha mahakama kabla ya majaji wa jeshi kutoa uamuzi ambao wengi walikuwa wanautegemea wa kukutwa na hatia, na alikuwa amefika nje ya mahakama ile kabla kelele hazijamfanya ageuke. Wanajeshi kadhaa walikuwa wakimchukua Ceausescu nje na kumburuta chini kwa pamoja. . . Askari waliwasukuma ukutani na walipokuwa wakirudi nyuma walianza kupiga risasi.

Kwa kweli lilikuwa ni tukio la kushangaza sana. Ilikuwa ni tukio la kwanza la utekelezaji wa maujai dhidi ya kiongozi mkuu kabisa katika nchi na sio kitu ambacho kinaweza kusahaulika kirahisi kwa watu wa Romania.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wewe na familia yako kura zenu mkimpa msaliti wa Nchi haitaathiri kitu kwa sababu Dr Magufuli ni kipenzi cha Watanzania na tutampigia kura kwa 98% Vijana wachache wa Chadema mwaka huu mtajiua sana.
 
Asante Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati, Mungu akupe afya uendelee kututumikia.
 
Sijawahi kuwapenda madikteta kama Idd Amin pamoja na Mobutu.

Sipendi double standard...!!!!
Iddi Amin alikua mtu poa Sana, alikua mzalendo wa kweli kwa nchi yake, ndio maana
_ akaamua kutangaza Sera ya kuwafukuza raia went asili ya bara Asia Ili arudishe uchumi kwa waganda halisi
_akaamua kuvamia kipande Cha mkoa wa kagera na kulazimisha kiwe ni Uganda(alifanya kwa ajili ya waganda) hakuvamia ili yeye akaishi pale.
_kwa kuwa alikua muislam, aliamua kujiunga na waislam wenzake duniani(Gaddafi) kupigana dhidi ya adui(wewe kwenye comment zako umemuita Western).

Swali linakuja kwako unaposema kwamba Western ndio wanafanya mipango ya kuondoa viongozi wazalendo kwa nchi zao, halafu likija suala la iddi Amin unamuita dikteta, nashindwa kukuelewa vizuri, iweje yule wa kijani(tz) unamtetea na kumuita mzalendo ilhali matendo mengi meusi yametokea wakati wake mpaka mwanae akabatizwa jina la Maliyamungu (Kama yule wa uganda)

Halafu ikija ishu ya iddi Amin unamuona ni dikteta? Ni Bora ukawa wazi kwamba uko upande gani hapa nchini.
 
Jamaa alikua anajipenda sana huyu, mpaka anauliwa wanaenda nyimbani kwake walikuta misuti mipyaa ya bei mbaya ipo kabatini haijavaliwa kabisa. Alipenda kuweka picha zake kila kona ya nchi, alikua Dictator aliyekuwa na cult of personality kubwa sana na alipinduliwa kimasihara tu hata hakuamini maana alikua anahutubia wananchi kamampindua hapo hapo.
Hakika binadamu wote tuna hulka ya kutopenda kuridhika.
 
Idd Amin alikuwa mtu mmoja mbaya na mkatili sana mkuu...
Hapana, kwa eidd nitasimama tofauti Sana na wewe ki mtizamo.

Amini nakwambia eidd alikua Bora mara Mia kuliko;

-Nkulunzinza.
-kagame.
-Museveni.
-Mgombea/gari la mkaa.

Wewe ni mliotekwa na propaganda za wazungu.

Amin alikua na maono ya mbali Sana, aliamua kuwaondoa wahindi mitaa ya Kampala ili awaruhusu raia wazawa wamiliki uchumi wao(niambie mgombea alishawahi hata kuwatishia wachina waondoke? Wachina wanaichezea tz watakavyo)

Amin alikua na mpango wa kuiunganisha Africa iwe moja, Yeye na Gaddafi ndio walikua na mipango hiyo kwa dhati kabisa.

Jaribu kufuatilia speech za Amin usikilize mtazamo wake, usikae na kusikiliza propaganda za tanzania , Mambo ya Amin kula nyama za watu, usiamini.
 
Kulikuwa na dada mmoja mrembo sana "Female Assassin" wa idara ya ujasusi ya KGB aliwahi kuficha risasi mbili ndani ya uke wake alipoenda kumuua mfanyabiashara mmoja maarufu sana katika hotelini huko jijini Minsk mji mkuu wa nchi ya Belarus.

Mfanyabiashara huyo alikuwa amepishana kauli na serikali ya USSR mwaka 1979.

Nipo ninaiandaa hiyo story alafu ikikamilika nitaiweka humu HARAKA SANA.
USSR
 
Back
Top Bottom