Kisa cha Mke wa Bokassa rais wa CAR na Rais wa Ufaransa Valéry Giscard

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
324
909
…Valéry Giscard d’Estaing alikuwa ni Rais wa Ufaransa kuanzia mwaka 1974 hadi 1981.

Jean-Bedel Bokassa alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) mwaka 1966 hadi 1979.

Ndani ya miaka 13 ya utawala wake, alibadili mfumo wa utawala nchini mwake CAR na kuwa utawala wa Kifalme… Baadae akajipachika cheo cha «Mfalme Mkuu» (Emperor).

Viongozi hao wawili (wanaosalimiana, picha ya juu), walikuwa ni marafiki wakubwa sana.

Urafiki wao uliingia doa pale ambapo Rais Valéry wa Ufaransa alianza mahusiano ya kimapenzi na mmoja kati ya wake wa Rais Bokassa wa CAR

Rais Bokassa alikuwa na wake 17, watoto 50.

Mke wake wa 6, Catherine Denguiadé (picha ya chini), ambaye aliteuliwa na Rais Bokassa kuwa «First Lady» na aliyeambatana naye katika ziara zote ndani na nje ya nchi, akawa mchepuko wa Rais Valéry wa Ufaransa

Festi ledi huyu, alisafiri mara kwa mara, kutoka Bangui, mji mkuu wa CAR na kuja hapa Paris, kwa mchepuko wake, huku akimuaga mumewe kuwa anafuatilia biashara zake.

Baada ya Rais Bokassa kugundua mahusiano hayo, urafiki wake na Rais Valéry ukaishia hapo.

Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na mtawala wake wa zamani (Ufaransa) ukayeyuka kama mshumaa.

Rais Bokassa akatangaza kuanzisha sarafu mpya ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuachana na sarafu ya Ufaransa (Franc CFA), akapiga marufuku magazeti ya Ufaransa nchini mwake, akaachana na mipango yote ya kiuchumi kati ya Ufaransa na nchi yake na baadae akatangaza utawala wa Kifalme na kubadili jina la nchi na kuwa «Central Africa Empire», kwa Kifaransa «Empire Centrafricain»…

Baada ya urafiki kati ya marais hao wawili kuvunjika, upande wa pili, mapenzi yakanoga kweli kweli, kati ya Bi Catherine na Rais Valéry… Bi Catherine akapewa ujauzito na Rais Valéry… 🫃

Lakini bado Rais Bokassa akaendelea kuwa kero katika mahusiano hayo… Mkewe Catherine hapewi tena ruksa za kutoka nchini kwake na kuja Ufaransa

Rais Valéry akaamua kumuondoa madarakani swahiba wake wa zamani…

Septemba 20, 1979, Rais Bokassa akiwa ziarani nchini Libya kwa swahiba wake Muammar Gaddafi, Rais Valéry aliwatuma makomandoo kutoka hapa Ufaransa na kwenda kupindua serikali ya Bokassa, jambo ambalo walifanikiwa na baadae wakamrejesha madarakani David Dacko, aliyekuwa amepinduliwa na Jean-Bedel Bokassa hapo kabla, kwa msaada wa Ufaransa

Mahusiano ya kimapenzi kati ya Catherine na Rais Valéry yakaendelea…

Lakini kutokana na ziara za mara kwa mara za huyu Bi Cathe alizokuwa akifanya ikulu hapa Paris, festi lady huyu akaanzisha mahusiano mengine na René Journiac (picha ya juu, aliyezungushiwa duara)…

Huyu Mheshimiwa Journiac alikuwa ni Katibu Mkuu hapo Ikulu ya Ufaransa na Mshauri wa Rais Valery katika masuala ya Afrika…

Rais Valery alipogundua mahusiano hayo, akamuagiza Mheshimiwa René Journiac Libreville, Gabon kwa swahiba wake Omar Bongo… Akampa pia ujumbe anaotakiwa kumpelekea Rais Ahmadou Ahidjo, wa Cameroon

Rais Valery akamwambia Rais Bongo, amalizane na huyo mshauri wake huko huko Gabon yaani ahakikishe asirudi Ufaransa akiwa hai…

Bila kujua ya kwamba ndio safari yake ya mwisho, Mheshimiwa René Journiac akaondoka Ufaransa na kuelekea Libreville, mji mkuu wa Gabon

Baada ya ziara yake ya kwanza kumalizika nchini Gabon ikawekwa bomu kwenye ndege yake kutoka Gabon kuelekea Cameroon bomu lililolipuka baada tu ya kutua katika uwanja wa ndege wa Ngaoundéré, nchini Cameroon February 6, 1980…

Rais Jean-Bedel Bokassa alifariki mwaka 1996 kwa matatizo ya moyo baada ya kuishi maisha ya dhiki sana uhamishoni Côte d’Ivoire na Ufaransa Story yake ni ndefu… Siku nikipata wasaa, nitaisimulia kwa mapana humu…

Rais Valery Giscard d’Estaing, kutokana na skendo hiyo pamoja na ile ya almasi nchini CAR hakuchaguliwa muhula wa pili nchini Ufaransa Alifariki mwaka 2020 kutokana na maambukizi ya corona…

Bi Catherine Denguiadé yupo hai mpaka sasa. Ana umri wa miaka 74, anaishi nyumbani Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo anajishughulisha na kilimo cha mihogo.

Screenshot_20240301-232747.png
 
View attachment 2921837
Story za vijiweni..
Ukweli ni kwamba Hawa jamaa walikuwa marafiki..Bokassa alifanya rafiki yake Valery akose kuchaguliwa urais kwa mara ya pili kisa alipokea almasi kutoka kwa Bokassa
 
Back
Top Bottom