Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,918
- 30,259
John Iliffe amepata kusema kuwa historia ya TANU nyingi iko katika mikono ya watu.
Hakika maneno haya ni ya kweli wala hayana shaka.
Nimepokea nyaraka nyingi na picha kutoka kwa watu zinazohusu historia ya TANU na historia ya Mwalimu Nyerere kutoka kwa watu na sehemu ambazo sikutegemea kabisa.
Nimepokea simu kutoka kwa rafiki yangu yuko Kilwa Pande ananiambia kakutana na kijana amekaa anaaangalia video yangu moja nazungumzia historia ya uhuru wa Tanganyika.
Huyu ndugu yangu akamfahamisha yule kijana kuwa anamfahamu huyo anaemtazama kwenye hiyo video.
Hivi ndivyo nilivyokutana na huyu kijana akanipa kipande cha historia ya nyumba ya Bi. Mgumba, nyumba ambayo Mwalimu Nyerere alilala mwaka wa 1955 wakati wa kueneza TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.
Yule kijana akanirushia picha ya nyumba hiyo na akanipa na simu za mtu ambae yeye alikuwa kijana mdogo kiasi cha miaka 10 wakati Nyerere alipokwenda Kilwa Pande.
Huyu bwana Sheikh Suleiman Mwandu nilimpata na tukafanya mazungimzo.
Nilistarehe na nafsi yangu.
‘’Mimi nilikuwa na umri kiasi cha miaka 10 wakati Nyerere alipokuja Pande wakati wa kupigania uhuru akapokelewa na Bwana Abdul Manafi, baba yake Bi. Mgumba.
Hawa vijana wa leo wanapoieleza ile nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere wanasema kalala nyumba ya Bi. Mgumba.
Huyu Bi. Mgumba wakati ule yeye alikuwa mtoto lakini hiki kizazi cha leo wamekuta nyumba ile anakaa Bi. Mgumba kwa kuwa baba yake Abdul Manafi alikuwa keshafariki na Bi. Mgumba ambae jina lake khasa ni Halima bint Abdi Manafi ndiye akiishi nyumba ile.
Aliyempokea Mwalimu Nyerere ni Bwana Abdul Manafi na yeye alikuwa mtu akijiweza akifanya biashara ya duka hapo nyumbani kwake.
Pamoja na yeye walikuwa Khamisi Mamboya, Bakari Suleiman Mtondoo na Suleiman Shaweji ambao baadae walikuja kuwa viongozi wa tawi la TANU hapa Kilwa Pande.
Hii nyumba ambayo unayopicha yake ndiyo khasa nyumba aliyofikia Mwalimu Nyerere lakini ile ilikuwa nyumba ya makuti hii nyumba hivi sasa imeezekwa bati.
Mwalimu Nyerere aliingia na mguu wa kulia Kilwa Pande akitokea Kilwa Masoko na alikuja na boti inayoitwa, ‘’Makunganya.’’
Mtandula ndipo kilipo kivuko kuja Pande.
Hapa ilibidi nimkatishe kauli mpashaji habari wangu Sheikh Suleiman Mwandu kutaka uhakika kama nimesikia vizuri kuwa Mwalimu Nyerere kenda Kilwa Pande na boti inaitwa Makunganya.
Hassan Omari Makunganya alipigana na Wajerumani na walipomkamata walimnyonga na mnara wa kumbukumbu yake na wazalendo wengine upo Kilwa.
Hapakuwa na tawi la TANU lakini Pande kulikuwa na wanachama wa TANU waliokuwa na kadi zikiuzwa senti hamsini lakini wakizificha kuogopa serikali.
Mwalimu Nyerere aliingia Pande kwa mguu wa kulia kwa kuwa siku ile usiku wake kulikuwa na mkesha wa Maulidi, kulikuwa na Ziara ya kila mwaka ya Tariqa Qadiriyya tarehe 14 kuamkia 15 Rajab.
Mji ulikuwa umefurika watu kutoka vijiji vya jirani kuitika mwito wa Khalifa wao Sheikh Athmani Ahmed aliyechukua uongozi wa kutoka kwa Sheikh Khamis Abdallah ambae alikuwa kafariki mwaka wa 1952.
Usiku ule katika Maulid yale uwanjani kwa Sheikh Ahmed Athmani Waislam wakatangaziwa kuwa kesho Julius Nyerere anakuja Pande watu watoke kumpokea Mtandula na kutakuwa mkutano wa hadhara uwanjani kwa Abdul Manafi na Julius Nyerere atawahutubia wananchi wa Tanganyika.
Hivi ndivyo TANU ilivyobisha hodi Pande na wananchi sasa wakapata nguvu ya kuitangaza TANU.
Ikawa makarani wa kununua mbata na korosho katika kazi zao wakiwahimiza wale wanaokuja kuuza mazao yao kuwa watoe senti hamsini wakate kadi ya TANU.
Kama wanavyopenda kusema Waingereza, ‘’The Rest is history,’’ yaani yaliyobakia ni historia.
Hakika historia ya uhuru wa Tanganyika iko katika vichwa vya watu kama alivyosema John Iliffe.
Picha: Nyumba ya Mzee Mwinyimkuu Manafi aliyofika Baba wa Taifa Kilwa Pande mwaka wa 1955, wa katikati ni Hassan Omari Makunganya alipokamatwa na Wajerumani.