NIC leo balaa

Mwana UoA

Member
Nov 8, 2011
47
6
Sijawahi ona hali kama ya leo hapa Diamond Jubilee kwa haraka harka nikihesabu watu waliokuja kwenye interview ukumbi mzima ulijaa na ukatapika labda wizara husika ingelikuwa inahudhuria interview hizi wangelijua nichoongea hapa watu waliofika ni kama 6000 nafasi zilizotangazwa ni assistant accountant4 na internal auditor 1 hali ngumu sana jamani
 
haaaaa m ningekuwa nachukua contacts tu za mawifi zenu basi..interview watu 6000 si matapishi hayo....bora restless developemnt kitu kwa simu then finalist 3 ...watu tunapumulia kandarasi ziko uchagoni
 
nafasi nne jumlisha moja jumla Tano waliofika kwenye interview 8000 jamani kikwete ama kweli bomu alilolitengeneza litalipuka hivi karibuni kama Lowasa alivosema sijawahi ona hata ukipga probability ya kupata kazi unajikuta haumo kabisa ukumbi ulifurika na kutapika watu
 
mpaka sas tumefikia elfu8000 kuna watu wmehamishwa kwenda ukumbi mwingine hewa hamna kabisa yaani watu wanazidi kumiminika
 
Si mmeendelea kulikumbatia liserikari la mkoloni mweusi CCM ngoja muone moto wake! Ajira ngumu na ni hatari kama Kifo.
 
Jamani hii ni shida kubwa kwa wanaoomba ajira waajiri ni lini mtafanya kazi kwa weredi? this is un professional! haiwezekani nafasi tatu shortlist mnaitwa watu 600 haipo hiyo,kinachohitajika ni kufanya kazi kwa kwa kuongozwa na maadili ya Human Resource katika ajira,badilikeni jamani huu ni udhalilishaji kuwaleta watu wengi kiasi hiki wakati ambapo probability ya kuipata hata hiyo kazi yenyewe ni almost 0.001! naomba kuwakilisha wakauu.
 
Au ni walkin interview? Hata kama wameamua kusaili wote hao (manake posho ya kusaili si ya kitoto), si wangetoa ratiba! Honestly,how do u interview watu 8000! Manake hata bongo star search sio hivyo!
 
1. Unategemea nini kama serikali ina maafisa mipango kila wilaya, mkoa, kanda na kila wizara wizara ambao hawafanyi kazi zao inavyotakiwa kisa ni ndugu wa wakubwa?
2. Unategemea nini serikali haitengenezi mazingira ya utengenezaji wa ajira kwa ajili ya wahitimu na kuongeza uzalishaji na pato la taifa?

3. Unategemea nini watu wenye mamlaka ya kutunga sera na mambo kadha wa kadha kuhusu maendeleo ya nchi yetu lakini watu hawa wengi wao hawana uwezo wa desseminate hizo sera kwa walengwa,licha ya hilo hata kuibua sera nzuri zenye kusaidia jamii hazipo na wale wenye majukuu hayo uwezo ni mdogo.

Hapa jibu ni moja, watu mahususi wanahitajika kwa ajili ya kutupa mwongozo. Hii tabia ya kurundikana ndugu hata kama ni vilaza kwenye nafasi nyeti madhara yake ndo hayo ya kuwaita watu 6000 nafasi 4. Bullshit!
 
Hao watu 8000 wote hawana ajira, na ni walosoma accounts tu. Je walosoma fani nyingine? Na je ambao hawakufika vyuoni? Na hapo ni mkoa mmoja tu.


Ni hatari sana
 
Back
Top Bottom