NIC leo balaa

Kwa idadi hiyo ya watu hata umakini kwenye interview hautakuwepo. Hii ni kupotezea watu muda hasa wale wa mikoani
 
Du udom nasikia walienda watu karibia 12,000 na leo 8,000 du hatareeeeee ngoja niendelee na kilimo kwanza huko kwenye maajira balaaaaaaa
 
nafasi nne jumlisha moja jumla Tano waliofika kwenye interview 8000 jamani kikwete ama kweli bomu alilolitengeneza litalipuka hivi karibuni kama Lowasa alivosema sijawahi ona hata ukipga probability ya kupata kazi unajikuta haumo kabisa ukumbi ulifurika na kutapika watu

Naamini kuwa wamekuja wengi lakini si kiasi hicho!!! Kwani hawa NIC hawafanyi shortlisting? Hata kama wanawapa kwanza mtihani, hiyo idadi ni kubwa mno. Kwa nafasi tano wangeita 100 halafu ndo waanze mchujo
 
Ndo tumetoka jamani nashindwa kupost picha za watu na matujio mbalimbali ila cha kushangaza msimamizi mmoja alitaka kujua mie ni nani napiga picha nikamjibu mie sina cheo wala kazi nachukua picha kwa ajili ya kumbukumbu zangu ila inatisha wapendwa sijawahi ona nina shangaa wanaoshabikia serikali ya kikwete ya mafisadi pia matunda ya kuwa na wasomi wengi ndo haya ila mwisho wa yote sidhani kama tutafika 2015 salama wanaoiharibu nchi hii ni wabunge wanatunga sheria mbovu namshukuru Mungu kwamba aliyeona mbali kuanzisha vyuo tz itafikia hatua kama ya nigeria nyie subirini nasema haya kwa uchungu sana na leo niliamua kwenda makusudi maana sikuenda pspf na NAO
 
Maana ya kushort list ni nini?

Thats is it..........mimi nimekuwa involved na recruitment processes many times na sijawahi kuliona hili. Nadhani mwaka jana NSSF nao walifanya hivyohivyo pale Diamond Jubilee.......aidha ni uvivu au kukosa maarifa.....hatua ya mwanzo ni pale unapotangaza nafasi ya kazi,ni lazima ueleze vigezo ambavyo automatically vita wafanya watu wasombe kazi kwa idadi kubwa....ukisema tu anahitajika mhasibu mwenye degree basi uatapata watu 10,000
 
Naamini kuwa wamekuja wengi lakini si kiasi hicho!!! Kwani hawa NIC hawafanyi shortlisting? Hata kama wanawapa kwanza mtihani, hiyo idadi ni kubwa mno. Kwa nafasi tano wangeita 100 halafu ndo waanze mchujo

mpendwa hakika nisemayo ni ya kweli sipo hapa JF kupoteza Muda wangu nilikuwemo ndani I hope soon nitaziweka picha zote nilizopga humo ndani kama uliwahi fika diamond jubilee ukumbi B na C ulifurika mpaka mlangoni na wakapelekwa ukumbi mwingine
 
ina maaana hao 8,000 wote hawana ajira, na hapo ni nafasi 4 tuu, daaah na mwakani wengine wanakuja mtaani..???? daaahhhh ajira ni noumaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mi ninachoshauri, waambieni wadogo zenu wasome sana ili wasiwe kama wahasibu niliowaona last week ofisini kwetu. Nakubari kuwa waliosoma uhasibu ni wengi lakini wanaoujua ni wachache! kwa hiyo msiogope tu wingi, wengine ni kama wamesoma hakuna!

Mi nafanya kazi na international org hapa tz, tangu mwezi jana tulikuwa tunaitaji wahasibu wawili, hatukutangaza gazetini, ila tulitangaza ndani humo. tulipokea application zaidi ya 400. tukaamua kuchuja, tukatafuta wenye GPA above 3.5 ili kuwapunguza, huwezi amini tulibaki na less than 30 application! Tukaongeza kigezo cha mtu awe angalau na full Module E, tulibaki na sita tu!

Kwa hiyo jamani msilahumu sana, kwanza GPA zinawaruhusu au mnairahumu tu serikali? eti mtu ana 3.0, naye anataka aitwe NAO! si utani huu! ni hayo tu!
 
NSSF mwaka juzi it was the same. tulikuwa wengi mno hadi niliona kama nimepoteza nauli yangu tu na gharama za malazi na chakula kutoka ukerewe mwanza kuja dar
 
Nafasi 5, hapo toa angalau 2 kwa wale watakaopata ajira kwa njia ya 'vimemo', zinabaki 3 kwa ajili ya watoto wa wakulima. Hapo wengine washasahau ndani ya misikiti na makanisa kunafananaje wanaabudu G.P.A tu..Nawatakia mafanikio.
 
Mi ninachoshauri, waambieni wadogo zenu wasome sana ili wasiwe kama wahasibu niliowaona last week ofisini kwetu. Nakubari kuwa waliosoma uhasibu ni wengi lakini wanaoujua ni wachache! kwa hiyo msiogope tu wingi, wengine ni kama wamesoma hakuna!

Mi nafanya kazi na international org hapa tz, tangu mwezi jana tulikuwa tunaitaji wahasibu wawili, hatukutangaza gazetini, ila tulitangaza ndani humo. tulipokea application zaidi ya 400. tukaamua kuchuja, tukatafuta wenye GPA above 3.5 ili kuwapunguza, huwezi amini tulibaki na less than 30 application! Tukaongeza kigezo cha mtu awe angalau na full Module E, tulibaki na sita tu!

Kwa hiyo jamani msilahumu sana, kwanza GPA zinawaruhusu au mnairahumu tu serikali? eti mtu ana 3.0, naye anataka aitwe NAO! si utani huu! ni hayo tu!

GPA co ishu, wangap wana uper au first lakn walimeza tu na kuotea mthan wakapita? Kwanza vyuo vinadiffer ingekuwa 2nafanya mthan m1 kama necta sawa, vyuo vngne wanafavour vngne ndo hvyo? Unakuta m2 ana gpa kubwa bt he has nothng kichwani....
 
Jamani hii ni shida kubwa kwa wanaoomba ajira waajiri ni lini mtafanya kazi kwa weredi? this is un professional! haiwezekani nafasi tatu shortlist mnaitwa watu 600 haipo hiyo,kinachohitajika ni kufanya kazi kwa kwa kuongozwa na maadili ya Human Resource katika ajira,badilikeni jamani huu ni udhalilishaji kuwaleta watu wengi kiasi hiki wakati ambapo probability ya kuipata hata hiyo kazi yenyewe ni almost 0.001! naomba kuwakilisha wakauu.

Yani wanaboa hao HR wa siku hizi. Very unproffessional na hao mabosi wao sijui kwanini wanaruhusu. Hakuna shortlisting? Shame on them.
Wanaokuja kwenye inyerview wenyewe wamekopa nauli. Huo ni udhalilishaji,period!
 
GPA co ishu, wangap wana uper au first lakn walimeza tu na kuotea mthan wakapita? Kwanza vyuo vinadiffer ingekuwa 2nafanya mthan m1 kama necta sawa, vyuo vngne wanafavour vngne ndo hvyo? Unakuta m2 ana gpa kubwa bt he has nothng kichwani....

Jamani, hata tusemeje, GPA inamata! na mimi binafsi nimeshasimamia interview mbili tangu nilipopata kazi, moja ya uasibu na nyingine ya internal auditor. wenye GPA kubwa wanajiweza na hata ukiangalia performance ya NBAA, wanaofaulu ni wenye GPA kubwa, this meas, wanajua wanafanya nini? sasa ndugu mtu atakuwa na GPA ndogo alafu useme anajua?

Uasibu si kujua DR na CR bwana! mtu hajui IFRS, IAS, ISAs, sa huyo ni muhasibu gani?

hacheni zenu bana, vijana hawako competent!
 
Sijawahi ona hali kama ya leo hapa Diamond Jubilee kwa haraka harka nikihesabu watu waliokuja kwenye interview ukumbi mzima ulijaa na ukatapika labda wizara husika ingelikuwa inahudhuria interview hizi wangelijua nichoongea hapa watu waliofika ni kama 6000 nafasi zilizotangazwa ni assistant accountant4 na internal auditor 1 hali ngumu sana jamani

Mkuu pole sana.Naona leo umejifunza nini maana ya MAISHA!Maana jana kuna mchango ulitoa ulidharau na kudhalilisha sana kazi nyingine.Si unakumbuka uliandika kazi ya ualimu ni ya div 4?Any way maisha ni vita,hakuna kukata tamaa.Majeshi mbele kwenye utafutaji ila acha dharau zako.
 
Au ni walkin interview? Hata kama wameamua kusaili wote hao (manake posho ya kusaili si ya kitoto), si wangetoa ratiba! Honestly,how do u interview watu 8000! Manake hata bongo star search sio hivyo!

madam acha hii kauli ikibidi ifute maana wenyewe wakiiona watahisi unawanaga aisee. haingii akilini kabsaaaaaaaaaa, post 5 watu hata wakiwa 100 still ni wengi mno
 
Back
Top Bottom