Ni wapi ulipotoka, ulipo sasa na unategemea kuwa wapi baada ya miaka 5?

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Aug 10, 2021
2,035
2,682
Uzi huu unalenga kuwasaidia vijana ambao hawajui wapite wapi na wapi ili wafikie ndoto zao, jieleze kwa kina toka mwanzo ulipoanza haso zako, kipindi ambacho ulikuwa huna hata pesa ya kula, haso ulizopitia, huku ukionyesha njia na biashara unayofanya sasa, changamoto zake, ilikuwasaidia wengi toa ukweli wako, haina maana ya kutudanganya maana najua uzi huu utawasaidia mamia ya vijana Tanzania.
 
Mtoa mada naanza hivi, story yangu yakuhaso inaanza 2011 MMorogoro, baada ya kumaliza form 4 nilifeli, ilikuwa kipindi kigumu sana kwangu, form 4 nilimaliza 2010 ,ndio nilipoamua kwenda Morogoro kwa baba mdogo kusomea udereva katika chuo cha national sugar ilovo[Mkamba Kilombero].

Nilipofika tu nikaanza chuo nakumbuka nilisoma kwa miezi 3 hivi, nyuma ya nyumba ya baba mdogo kulikuwa na shamba nusu heka pembeni kulikuwa namfereji ambao unajaa maji full kila mvua inaponyesha, maji hayo ndo watu walikuwa wanatumia kunyeshea mashamba yao.

Kilombero ni sehemu iliyobarikiwa sana, kuna wakulima wa mpunga, miwa n.k, pia kuna wafugaji wa nguruwe, kuku n.k, lile shamba nilimuomba mwenyewe nililime akakubali maana lilikuwa kama pori hakuna aliyekuwa analima, jamaa alikubali nilime bure sikumpa ela yeyote.
 
HARAKATI ZA KULIMA SHAMBA

Baba mdogo alikuwa na jembe lake butu, pia mpini ulikuwa mfupi alafu umepasuka, nilimuomba mother ela akanitumia kama elfu 20 hivi, nilitoa nakumbuka kulikuwa hakuna makato kama sasa,nilitoa elfu 18 hivi,nilitoa elfu 5 nikanunua mpini mpya kabisa,nikatoa buku nikapeleka jembe kwa wanao noa,nikabaki na elfu 12.elfu 5 nilienda kwenye maduka ya pembejeo nikanunua mbegu za mchicha za kisasa kwa elfu 6, kipakiti kilikuwa kama robo hivi.

jembe nikaliweka mpini vinzuri,nikajiandaa kwa shughuli kubwa kesho ya kulima
 
Nilidamka asubuhi sana saa 12:45 nikamuomba Mungu anitangulie kwenye harakati zangu za kuanza kulima shamba,nilifika shambani nikaanza kulima,nilijisemea mwenyewe kama sita maliza kulima shamba hilo kwa masaa 7 basi sitakulachai wala kula chakula,mapambano yalianza jamani jamani nilikomaa kama utumwa mpaka ikafika hatua mkononi kukawa na sugu za maji,naposema sugu za maji najuwa unajua,kwenye viganja kulitoka maji maana ndo ilikuwa ndo mara ya kwanza kulima toka nizaliwe,mikono iliuma kinyama
 
Nilikomaa kibishi hivyo hivyo mpaka sugu zikatoa damu,nilijifunga kitambaa nikaendelea nilimaliza kulima shamba la nusu heka saa kumi na moja jioni,siku nzima nilishinda na maji na kula miwa sikula chai wala chakula
 
Kesho yake ndo ikawa siku ya kutengeneza matuta ,nilitengeneza matuta nikamaliza,niliingia mtaani nikapita kwa watu wanaofuga kuku na nguruwe niliwaomba mbolea wakaniambia nichukue kwa tani ninayotaka,nikaanza kusomba kwa gunia,nilikomaa siku nzima nikajaza mbolea za kutosha kwenye matuta yote, nilifunga kazi kwa siku hiyo
 
KUMWAGA MBEGU SHAMBANI
Mbegu nilizonunua hazikutosha kwa matuta yote, nilichanganya mbegu na mchanga ili zisitawame sehemu moja,nilizimwaga vinzuri zote nikamaliza
 
Harakati zangu zinaanza 2015 baada ya kuferi kidato Cha nne, nikaingia mtaani kusajili lain za mitandao baada ya miezi mitatu nikawa na laki tatu. KWA bahati nzuri baba yangu alinisaidia kupata kazi ya kibarua katika kampuni moja hivi mshahara laki 3 nikaanza kupika kazi ndani ya miaka mitatu mkataba ukaisha na skua na option ya kuongeza mkataba.

Nilipo toka kazin nilianzisha biashara ya huduma za kifedha nikafanikiwa kukuza mtaji mpaka milion 4.8 hadi kufikia mwaka 2020 mwezi wa 8. Baada ya hapo niliona nibuni biashara nyingine ndani ya biashara niaanza kuuza sm na vifaa vyake. Kumbe nilikua navutia wezi wakaanza kuniandama kwa kuniibia mpka kuuwa walinzi...... Dah Ni story ndefu ila nimeandika kwa ufupi Sana.
 
Harakati zangu zinaanza 2015 baada ya kuferi kidato Cha nne, nikaingia mtaani kusajili lain za mitandao baada ya miezi mitatu nikawa na laki tatu. KWA bahati nzuri baba yangu alinisaidia kupata kazi ya kibarua katika kampuni Mona hivi mshahara laki 3 nikaanza kupika kazi ndani ya miaka mitatu mkataba ukaisha na skua na option ya kuongeza mkataba, nilipo toka kazin nilianzisha biashara ya huduma za kifedha nikafanikiwa kukuza mtaji mpaka milion 4.8 hadi kufikia mwaka 2020 mwezi wa 8. Baada ya hapo niliona nibuni biashara nyingine ndani ya biashara niaanza kuuza sm na vifaa vyake. Kumbe nilikua navutia wezi wakaanza kuniandama kwa kuniibia mpka kuuwalinzi...... Dah Ni story ndefu ila nimeandika kwa ufupi Sana.
Big up sana mkuu
 
Kazi ikawa kumwaga maji asubuhi na jioni nilikomaa kwa mwezi mmoja,mchicha shambani ulikubali hatari, kusema kweli niliuza mchicha kwa jumla na reja reja awamu ya kwanza nilipata 120000, nikanogewa ikawa ni kuvuna na kulima,nilifanya hivyo kwa mwaka mmoja nikajikusanyia ndani laka 800000
 
Baada ya kuzidi kuandamwa wezi walifanikiwa kunirudisha nyuma pia soko la sm likashuka, makato ya huduma za kifedha zikapanda nilififia ki mtaji kutokana na changamoto haza za kuibiwa nilirud KUTOKA 5.ml mpka 3.5 ml, mpka kufikia mwezi wa 9 nimeamua kuhamia jijin Dar mji wa kibiashara lakin kule nyumban nimemuacha mama yangu mzazi aendeleze biashara huku mm nikitafuta sehem sahihi kwa Dar lakin mpka Sasa naona nimeferi kabisaaa.
 
Baada ya kuzidi kuandamwa wezi walifanikiwa kunirudisha nyuma pia soko la sm likashuka, makato ya huduma za kifedha zikapanda nilififia ki mtaji kutokana na changamoto haza za kuibiwa nilirud KUTOKA 5.ml mpka 3.5 ml, mpka kufikia mwezi wa 9 nimeamua kuhamia jijin dar mji wa kibiashara lakin kule nyumban nimemuacha mama yangu mzazi aendeleze biashara huku mm nikitafuta sehem sahihi kwa dar lakin mpka Sasa naona nimeferi kabisaaa.
Bado mapema ndugu ebu endelea kutafuta
 
Back
Top Bottom