Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,871
- 6,513
Enzi za ‘zidumu fikra za mwenyekiti ‘ hazipo tena. Tunapaswa kuacha kuvhukua Nukuu zake ili zitumike kama reference huko Bungeni.
Socialism, Poor Education, Setup mbovu ya muungano, lack of transparency, lack freedom of speech nk ni katika failures kubwa sana chini ya uongozi wake.
Kuna masuala mengi sana yanaonesha huyu mzee wtu hakuwa anafanya mambo kwa maslahi na ustawi wa taifa bali ni aidha kwa maelekezo, ubinafsi, hofu ama ajenda anazozijua mwenyewe.
Suala la Muungano linamuweka sana uchi mzee wetu huyu na ndo kama legacy aliyotuachia basi warithi wake wote hawataki kugusa wala kubadili utafikiri ndo kiapo chao.
Julius ametuachia huu mgogoro mkubwa sana na hajawahi kuutolea ufafanuzi wa kitaalamu na kisheria zaid ya kutumia nguvu.
Kwa waliosoma kitabu cha “The dark side of Nyerere’s legacy” by Ludovick Simon Mwijage mtakubaliana nami kuwa sasa Ni wakat wa kuanza kujadili mienendo na maamuzi ya mwalimu na kuondoa dhana ya utakatifu wa bila kuhoji.
Ni wakati wa kubadili FALSAFA NA MITAZAMO YA MWALIMU