Mwalimu Nyerere alikataa wizi wa mali za umma ila alikubali uchafuzi wa uchaguzi: sasa hivi watawala wanataka fedha na uchafuzi wa uchaguzi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,124
Kwa mtizamo wangu Mwalimu Nyerere alifanikiwa sana katika kukataa kwa vitendo dhana ya kujilimbikizia mali. Aliridhika na kile kidogo alichopata na kuamua kwa dhati kutokubali kumvumilia mwizi wa mali za umma.

Kuhusu uchaguzi, mwalimu Nyerere katika miaka yake yote hakuwahi kukubali kuwekewa mpinzani kwenye uchaguzi. Huu ni udhaifu. Badala yake aliwahi kuwafungia wale walioonekana kumpinga aidha kifikra au kiutawala.

Uwezo wake mkubwa wakunyamazisha wanaompinga ulimsaidia kuendelea kutawala bila kuwa na mali wala fedha kwa sababu wapinzani wake awakutakiwa kufika kwenye sanduku la kura. Alimalizana na wapinzani wake nje ya ulingo wa wapiga kura na hivyo hakuna mpiga kura aliyepaswa kupewa kupewa takrima amchague. Ofcoz alipenda sana kupita bila kupingwa.

Aliposhawishi na kuratibu mfumo wa vyama vingi ndipo alipoingia kwenye rekodi mbaya zaidi ya uchaguzi. Aliingia kwenye kampeni 1995 akiwa anamnadi mkapa huku akipambana na Mrema. Kwa namna siasa zilivyoenda ilimlazimu anyamaze kuruhusu mfumo wa rushwa ufanye kazi ukisaidia na wachafuzi wa uchaguzi. Hakuweza kukemea.

Tunapomkumbuka leo tunapaswa kukumbuka pia mchango wake katika kunyamazia rushwa ya uchaguzi pale chama chake kilipoingia ulingoni. Kukaa kwake kimya kumechangia pia kukusekana kwa wakataa rushwa ya uchaguzi. Kilichoongezeka sasa kwa watawala wetu ni
1. Rushwa ya uchaguzi
2. Kujimilikisha mali
3. Undugu
4. Kutokuchukuliwa hatua kwa wezi na wakosaji.

Haya yote ni matokeo ya Mwalimu kushindwa kukemea uovu uliofanywa na chama chake.
 
Hata hivyo jambo jema ni kuwa unakiri kuwa Mwalimu alikuwa mwadilifu sana.

Kitu ambacho kinakosekana Kwa viongozi tulio nao sasa, ambao wao wameamua kuwa kuteuliwa kuwa Kiongozi, ni sawasawa na kupewa tiketi ya kuwa tajiri!
 
Back
Top Bottom