Je, ni Kweli falsafa za Mwalimu Nyerere zimeshapitwa na wakati? Ni Kweli Wananchi wanahitaji Upinzani halisi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,134
Falsafa za Mwalimu Nyerere ndio zilipelekea kuwapo baadhi ya Tunu

Moja ya falsafa hizo ni aina ya Upinzani tulionao ambapo kwenye kura ya maoni ni 20% ndio walitaka Upinzani

Nyerere akashauri Wengi wapewe wachache Wasikilizwe hivyo CCM ikapewa mali zote za Chama na wale waliotaka Vyama wakapewa Vyama

Katika mfumo huu huwezi kuitoa CCM kwa sababu ndio iliyoshikilia miundombinu yote ya kiulinzi, kiutawala na kisiasa

Hata ije Tume Huru haitafanya lolote kwa CCM kwa sababu Uhuru ni lazima uanzie kwa Watendaji ambao ni kichaa tu anaweza kuwatoa nje ya CCM

Kiukweli katika mfumo huu wa Vyama vingi Nyerere alituweka njia panda, Je Wananchi wa Leo wanahitaji Upinzani?

Viongozi wa Upinzani wametutia moyo kwa matendo yao?

Ni Kweli Vyama vya Upinzani vinatetea Wananchi au viko kiulaji (asali) zaidi?

Kwaresma njema!
 
Kwanza nikushukuru kwa hoja zako,pili nikukosoe kwa msimamo wako wa kulinda maslahi ya chama tawala.

Utangulizi wa Misingi ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema,"Kwa kuwa sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya Uhuru,Haki,Udugu na Amani;

Na kwa kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye DEMOKRASIA,ambayo Serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe Waliochaguliwa na linalowakilisha wananchi,na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila Woga wala Upendeleo wowote,na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa,na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu;

Kwa hiyo basi Katiba hii imetungwa na Bunge Maalum la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kwa Niaba ya Wananchi,kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo,na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya Demokrasia,Ujamaa na Isiyokuwa na dini."

Hivyo basi Katiba yetu haizungumzii Vyama au matabaka bali inasisitiza Umoja na Mshikamano kwa kufuata misingi ya Demokrasia(ambamo vyama mbalimbali vinalindwa na demokrasia kupitia katiba hii Ibara ya 13(1)(2)(4) na (5)) na Ujamaa (ambao ndio asili yetu ya Utanzania wetu katika kufanya kazi kwa upendo,umoja,ushirikiano)katika kudumisha nchi yenye upendo wa dhati,haki na wajibu wa kila raia,vyama,mamlaka,watumishi wa umma ili kufikia maendeleo halisi na ya kweli kwa kila Mtanzania.
 
Kwanza nikushukuru kwa hoja zako,pili nikukosoe kwa msimamo wako wa kulinda maslahi ya chama tawala.Utangulizi wa Misingi ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema,"Kwa kuwa sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya Uhuru,Haki,Udugu na Amani;
Na kwa kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye DEMOKRASIA,ambayo Serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe Waliochaguliwa na linalowakilisha wananchi,na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila Woga wala Upendeleo wowote,na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa,na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu;
Kwa hiyo basi Katiba hii imetungwa na Bunge Maalum la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kwa Niaba ya Wananchi,kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo,na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya Demokrasia,Ujamaa na Isiyokuwa na dini."
Hivyo basi Katiba yetu haizungumzii Vyama au matabaka bali inasisitiza Umoja na Mshikamano kwa kufuata misingi ya Demokrasia(ambamo vyama mbalimbali vinalindwa na demokrasia kupitia katiba hii Ibara ya 13(1)(2)(4) na (5)) na Ujamaa (ambao ndio asili yetu ya Utanzania wetu katika kufanya kazi kwa upendo,umoja,ushirikiano)katika kudumisha nchi yenye upendo wa dhati,haki na wajibu wa kila raia,vyama,mamlaka,watumishi wa umma ili kufikia maendeleo halisi na ya kweli kwa kila Mtanzania.
Katiba yenyewe ni ya 1977 wakati wa Chama Kimoja

Tena ilitengenezwa na Wanaccm wapatao 20 tu
 
Katiba hiyo hiyo ya chama kimoja mnamo mwaka 1992 ilitangaza kuwa,"Jamhuri ya Muungano itakuwa nchi ya Kidemokrasia na ya Kijamaa,isiyokuwa na dini,yenye kufuata Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa."(Ibara 3(1))
Kwahiyo 1992 CCM ilisajiliwa kama Chama kipya?
 
Kama unaamini kuwa kuna Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 yenye mamlaka yote yanayoihusu nchi yetu kwa nini useme ni katiba ya ccm?
CCM ni Chama Dola kilichoasisiwa 1977 Sawia na Katiba ya mfumo wa Chama Kimoja ya JMT
 
Kinachoiua ccm ni uhafidhina,ndio mana hii nchi imesimama kimaendeleo,pia ccm kwa kulazimisha mambo imegeuka kuwa chama dola.
 
Unaposema ccm hailazimishi,Je yale yote aliyoyafanya Rais wa Awamu ya tano yalikuwa yanatii ,kuilinda na kuitetea KATIBA YETU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA 1977 iliyomweka madarakani?
Hakuna Wakati wowote amevunja Katiba ya JMT 1977

Angevunja Katiba bunge la Vyama vingi lingehoji na kuchukua hatua
 
Falsafa za Mwalimu Nyerere ndio zilipelekea kuwapo baadhi ya Tunu

Moja ya falsafa hizo ni aina ya Upinzani tulionao ambapo kwenye kura ya maoni ni 20% ndio walitaka Upinzani

Nyerere akashauri Wengi wapewe wachache Wasikilizwe hivyo CCM ikapewa mali zote za Chama na wale waliotaka Vyama wakapewa Vyama

Katika mfumo huu huwezi kuitoa CCM kwa sababu ndio iliyoshikilia miundombinu yote ya kiulinzi, kiutawala na kisiasa

Hata ije Tume Huru haitafanya lolote kwa CCM kwa sababu Uhuru ni lazima uanzie kwa Watendaji ambao ni kichaa tu anaweza kuwatoa nje ya CCM

Kiukweli katika mfumo huu wa Vyama vingi Nyerere alituweka njia panda, Je Wananchi wa Leo wanahitaji Upinzani?

Viongozi wa Upinzani wametutia moyo kwa matendo yao?

Ni Kweli Vyama vya Upinzani vinatetea Wananchi au viko kiulaji (asali) zaidi?

Kwaresma njema!
Ukiichambua jamii ya watanzania utagundua kuwa wenye uelewa mkubwa na hasa wenye elimu kubwa wanapenda uwepo upinzani. Sehemu kubwa haioni tofauti ya chama kjmija na vyama vingi. Nyerere alijua tatizo lilikuwa uelewa akormtoa ushindi kwa 20 percent wenye uelewa.
Bado tuna jamii inayoamini mvua inakamatwa na mtu isinyeshe, lambalamba na chuma ulete nk.
Upinzani utakuwa real pale asilimia kubwa ya watanzania itakuwa imeelimika.
Kwangu mimi upinzani unapaswa kutiwa moyo na si kjuubeza.
 
Back
Top Bottom