Ni wakati sasa Tanzania iwe na wabunge 185 tu. Wabunge 199 wapunguzwe wote wanalitia hasa Taifa hawana masaada kabisa

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
3,362
5,809
Ndiyo ! Hayo ni maoni yangu ya dhati kabisa ili kupunguza matumizi ya fedha za umma

Tanzania ina halmashauri 185 tu ambazo zingetosha kabisa kuwakilishwa na mbunge mmoja mmoja kila halmashauri wakisaidiwa na madiwani

Kuwa na wabunge 384 kwa nchi kama tanzania ambayo ina changamoto nyingi za kimaendeleo kwa wananchi ni matumizi mabaya kabisa ya pesa za umma

Hawa wanao itwa wabunge wa viti maalumu wooote ni wakuondolewa wamekuwa mzigo kwa taifa na hawana faida chanya kwa watanzania

Wabunge wote wawe wakuchanguliwa na wananchi na taratibu za kuwapata hawa wabunge pia ziangaliwe upya nchi ina matatizo mengi sana inahitaji wabunge wachapa kazi na wenye nia ya dhati kutatua kero za watanzania na sio kupata wabunge wenye ubingwa wa kujibizana bungeni kwa maneno machafu na kejeli.

Tukiokoa pesa ambayo ingetumika kwa wabunge 199 kuwalipa posho na gharama zinginezo ilihali hawana tija yeyote kwa taifa itasaidia sana kuboresha changamoto nyingi sana

Piga hesabu posho na marupupu yoote wanayo lipwa wabunge hao kwa kipindi chote cha ubunge wao pesa hiyo ingejenga madarasa mangap na vituo vya afya vingapi

Yawezekana kuna wakati Mh. Rais anapata wakati mgumu ku alocate fedha za kutatua changamoto za watanzania kwa sababu pesa nyingi zinahudumia wanasiasa ambao kimsingi hawana tija wala michango chanyana ya kimaendeleo kwa wananchi wanao wazunguka.
 
Tatizo la Bunge letu ni muundo wake . Na hasa tatizo kubwa la Tanganyika ni katiba yetu ya 1977.

Odhis *
 
Siyo kazi yake
Nadhani unajua fika kabisa kwamba waziri wa fedha anapeleka budget ya serikali bungeni ijadiliwe ndipo ipitishwe na bunge

Sasa swali kwako , hiyo budget ya serikali huwa anakaa waziri wa fedha peke yake pasipo rais ambaye ndiye kiongozi mkuu wa nchi kuhusika?

Wakati huo fahamu kwamba sio kila kikao cha kupanga budget ya serikali utaambiwa wewe wa mchamba wima huko.

Wewe utasubiri itakapo wasilishwa bungeni ili usikie hao wabunge wanavyo anza kuchambana badala ya kujadili maswala ya msingi
 
Kwa nchi changa kabisa kama hii kimaendeleo ambayo uchumi wake bado ni legelege sana, hoja yako ni nzuri sana.
Lakini kwa kuwa wanaohusika ndio wanufaika wakuu watapinga kwa nguvu zote bila ya kuangalia itikadi zao.
Na hapo ndio utakuja kugundua kuwa tofauti ya chama tawala na chama cha upinzani ni bendera na mavazi yao, ila wote DNA yao inafanana.
 
mchamba wima mama yako shenzi, matusi ya nini?
Nadhani wewe ndiye uliye tukana na unahitaji kupigwa ban kabisa maana mchamba wima nisehemu na wanaishi watanzania ipo tanga lakini pia pemba ipo sasa kama hukuelewa ungeuliza ndugu na isitoshe huyo mama yangu unaye mtaja hapa hana hata babari kama kuna mtu kamtusi hapa, ungenilenga mimi mwenyewe kama lengo lako lilikuwa kunitukana mama hausiki kutajwa tajwa humu maana si yeye aliye post

Kwa sababu mamaangu mimi nadhana ni mama yako pia na huenda akawa bibi yako kama sikosei umefika mbali sana heshimu heshim wazazi hata kama si wako
 
Watanzania wote wanaishi kwenye halmashauri?
Nje ya halmashauri hakuna watu?

Mgawanyo wa halmashauri uko Sawa na idadi ya watu?....

Walio mbali na halmashauri zao?
 
Hivi ukisema halmashauri ni 185 ina maana kuna wilaya hazina halmashauri?..au wilaya pia zipo 185?na set up ya Zanzibar ikoje?
Wana halmashauri ngapi?
 
Watanzania wote wanaishi kwenye halmashauri?
Nje ya halmashauri hakuna watu?

Mgawanyo wa halmashauri uko Sawa na idadi ya watu?....

Walio mbali na halmashauri zao?
Sijaelewa una tetea nini na ndio maana nikasema wakisaidiana na madiwani au hukunielewa mkuu? Nafahamu katika halmashauri kuna rural na urban na ndio maana kukawa na madiwan wa kila kata ambao hao pia ni viongozi wa kisiasa chini mbunge hilo liko bayana kabisa na wala halihitaji majadala
 
Back
Top Bottom