Wabunge waliojiongezea mshahara hawajamchangia Rais Samia fomu. Walimu wanao lipwa pesa ya pipi wanamchangia fomu

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,731
Hili taifa linaangamia kwa ujinga, na ina hitajika uwe na akili ya ukichaaa kuamini kwamba Walimu wanao ishi life gumu sana, mishahara haitoshi, hawana posho, ila wao ndio wako mstari wa mbele eti kumchangia Raisi Fomu ya Uraisu na zike taasisi za umma zinazo lipwa vyema hawana hio time. Na walimu wanafanya hivyo wakiamini kwamba atawaongezea mishahara wawe sawa na wabunge.

Wabunge wa CCM walio jiongezea mishahara plus Posho hawamchangii Samia pesa ya fomu ya Uraisi. Hii lazima uwe na akili za ukichaaa kuamini jambo kama hili. kwa normal brain ni vigumu sana kuamini.Hii kwenye hii sayaru ya Dunia liko Tanzanua pekee na ni vigumu kulikuta kokote kule Duniani.

Walimu wanafanya hivyo katika misingi ya kuamini ndio njia pekee ya wao kupata masilahi zaidi, Kugoma hawawezi kabisa na haiwezi tokea kamwe. Wanachangishana fomu wakiamini hivyo kitu ambacho hakipo na wala hakitatokea sana sana wangoje pesa zao za kustafu watakazo lipwa.

Wenzao Kenya daily wanagoma na Walimu wa Kenya huwezi sikia huu ujinga kwao, yaani haiweze tokea wajipendekeze kwa wakina Ruto kisa waongezewe mishahara, wao wakitaka nyongeza ni kugoma tu basi.

Taifa kinaangamia kwa upumbavu kama wa hawa walimu wetu.
 
Hili taifa linaangamia kwa ujinga, na ina hitajika uwe na akili ya ukichaaa kuamini kwamba Walimu wanao ishi life gumu sana, mishahara haitoshi, hawana posho...
Ukisikia wapi wafanyakazi wa TRA, Ewura, Bank, Tiss, mawaziri, au taasisi yoyote inayolipa mishahara mikubwa wakamchangia rais?

Hiyo michango ya join the chain inafanywa na makapuku tuu.
 
Watu wajinga wanalalamikia walimu buure na kulazimisha waonekane wao ndiyo sababu nchi kudoda!!
Nchi hii inahitaji katiba ambayo viongozi watakuwa siyo watawala na hawako juu ya Sheria na nchi hii siyo miliki Yao.

1.) Walimu hawakuleta hii katiba ambayo rais ndiyo anaamua aongeze mshahara au aache na huna chakumfanya.

2.) Walimu hawakuleta katiba ambayo rais ndiyo huteua ampendaye Kwa cheo atakacho na humfukuza muda autakao.

3.) Walimu hawawezi kuandamana kwani kadagani imewahi kuandamana?
Wakulima,wafugaji,wafanyabiashara lini wameandamana?

4.) Walimu hawakuleta katiba inayomruhusu rais kukuweka ndani atakavyo ama viongozi wahovyo kukuteka na kukutesa apendavyo!

5.) LISSU alipigwa risasi nani aliandamana kupinga? Ni walimu walipaswa kuandamana?

6.) Chuo kikuu vijana wameshindaga njaa hawana pesa yakula wengine wanajiuza nilini waliandamana?
Wapumbafu muache kusemasema walimu wetu huku hamna mnachofanya zaidi ya kuandika upuuzi as if wewe ndiyo unaakili saana.

Mifumo yakikatiba imefanya kilamtu kuwa chawa ili aweze kula!!! Sasa hapo unalaumu walimu wanaojichawisha ili wafikiriwe kikipato vipi,tulitaka wafanyaje kama hakuna namna yawao kusaidika zaidi yahiyo?
 
Hili taifa linaangamia kwa ujinga, na ina hitajika uwe na akili ya ukichaaa kuamini kwamba Walimu wanao ishi life gumu sana, mishahara haitoshi...
Nafikiri wewe ndio mpumbavu kweli kweli zaidi ya walimu wetu ,unashindwa vipi kutofautisha chama cha walimu na walimu ,aliyekwambia walimu wamechaga kwa ajili ya form ni nani? Kila sehemu kuna walimu ,tafuta walimu watano karibu yako waulize kama wamechanga utapata mnajibu.
 
Mimi mwalimu niko huku namanyele kumbe nimemchangia Rais kuchukua fomu.... Nilikua sujui km nimemchangia hela rais! Km nimemchangia rais bila mm kujua basi haya ni maajabu ya dunia...
 
Back
Top Bottom