2030 nikiwa rais, kila mkoa utakuwa na wabunge 2 tu. MaRC, maDC na maDED kukatwa

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Panapo majaliwa 2030 nitatimiza miaka 40 umri amabao utaniruhusu kugombea urais. Nikiukwaa urais nitafanya mabadiliko makubwa ya muundo wa serikali na sera zake.

Ili kuyapata mabadiliko haya nitaunda jopo la wataalamu 16 (8 toka Zanzibar na 8 toka Tanganyika) litakaloandika katiba mpya kwa niaba ya watanzania.

Natamani kuliona Tanzania nitakayiongoza ikiwa na:-
1. Serikali ndogo yenye mawaziri 5 na manaibu waziri 5.
2. Cheo cha makamu wa rais nitakifuta. Rais akiachia madaraka kwa sababu yoyote ile nafasi yake itajazwa kwa uchaguzi kama wafanyavyo Namibia.
3. Wabunge watakuwa 2 tu kwa kila mkoa. Mmoja mwanamke na mmoja mwanaume. Watapatikana kwa kugombea kama inavyofanyika hivi sasa. Kutakuwa na kura za kumpata mbunge wa kike na kura za kumpata mbunge wa kiume.
4. Nitafuta kitu kinachoitwa pension. Ili kutenda haki na kujenga usawa kwa wazee wote kila mtu atapatiwa posho. Posho hii itakuwa sawa kwa kila mzee, awe mkulima, awe mstaafu wa shirika la umma ama ikulu. Wote watapewa posho moja. Maana wote wamelitumikia taifa moja ktk nyadhifa na kazi tofauti. Thamani ya mzee Kikwete na mzee Matonya mkulima wa huko Dodoma vijijini wana thamani sawa, kwahiyo watahudmumiwa kwa usawa.
5. Afya itatolewa bure kwa watoto wote walio chini ya miaka 5, walemavu na wazee. Wengine wote watachangia, bila kujali ni mjamzito ama la.

6. Vyeo vifuatavyo nitavifuta. RC, DC na DED.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu mbariki Sexless
 
Hutufai, nenda kawe rais wa nchi uliyotokea kabla hujaja Tanzania

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Ubunge unapaswa kupatikana kulingana na idadi ya watu, sio jiografia ya mikoa, barabara, mito, maziwa au mapori.
Ndivyo inavyotakiwa. Huu ujinga wa kila mkoa wabunge wawili wa jinsia tofauti sijui watu wanautoa wapi!

Zanzibar inatakiwa kuwa na wabunge watatu kwenye bunge la muungano. Wawili toka Unguja, na mmoja toka Pemba.
 
Hao wawili toka Zanzibar ni wa nini?
 
Panapo majaliwa 2030 nitatimiza miaka 40 umri amabao utaniruhusu kugombea urais. Nikiukwaa urais nitafanya mabadiliko makubwa ya muundo wa serikali na sera zake.

Ili kuyapata mabadiliko haya nitaunda jopo la wataalamu 16 (8 toka Zanzibar na 8 toka Tanganyika) litakaloandika katiba mpya kwa niaba ya watanzania.

Natamani kuliona Tanzania nitakayiongoza ikiwa na:-
1. Serikali ndogo yenye mawaziri 5 na manaibu waziri 5.
2. Cheo cha makamu wa rais nitakifuta. Rais akiachia madaraka kwa sababu yoyote ile nafasi yake itajazwa kwa uchaguzi kama wafanyavyo Namibia.
3. Wabunge watakuwa 2 tu kwa kila mkoa. Mmoja mwanamke na mmoja mwanaume. Watapatikana kwa kugombea kama inavyofanyika hivi sasa. Kutakuwa na kura za kumpata mbunge wa kike na kura za kumpata mbunge wa kiume.
4. Nitafuta kitu kinachoitwa pension. Ili kutenda haki na kujenga usawa kwa wazee wote kila mtu atapatiwa posho. Posho hii itakuwa sawa kwa kila mzee, awe mkulima, awe mstaafu wa shirika la umma ama ikulu. Wote watapewa posho moja. Maana wote wamelitumikia taifa moja ktk nyadhifa na kazi tofauti. Thamani ya mzee Kikwete na mzee Matonya mkulima wa huko Dodoma vijijini wana thamani sawa, kwahiyo watahudmumiwa kwa usawa.
5. Afya itatolewa bure kwa watoto wote walio chini ya miaka 5, walemavu na wazee. Wengine wote watachangia, bila kujali ni mjamzito ama la.

6. Vyeo vifuatavyo nitavifuta. RC, DC na DED.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu mbariki Sexless
Nakushauri hapo kwa "DC&DED abaki DED
 
1. Imagine Makamba wizara Moja tu imemshinda leo uje umuongezee mzigo wa wizara nyingine kama nne azisimamie ataboronga vibaya! Nchi ya sita Kwa ukubwa Africa haiwezi kuwa na mawaziri watano mkuu? Fikiria nchi ndogo kama Israel ambayo kijiografia inaingia zaidi ya mara 20 Kwa Tanzania lakini ina Baraza lenye mawaziri 37, kama ni rahisi kihivyo basi naamini hata wao wangepunguza.

2. Kufuta cheo Cha makamu wa raisi na kuitisha uchaguzi wa taifa pale raisi anapofariki itaongeza gharama Kwa wananchi kwani chaguzi zinatumia fedha nyingi mno. Ni bora waziri mkuu abebe vyeo vyote viwili Yani awe makamu wa raisi na waziri mkuu. Itungwe Sheria kwenye katiba itakayo ipa bunge nguvu ya kuchagua raisi mpya kutoka chama husika pale inapotokea raisi(incumbent) amefia madarakani na raisi huyo mpya atakaepigiwa kura na bunge atakuwa ni interim president yaani raisi wa muda mpaka pale utakapo fika muda wa uchaguzi mkuu

3. Swala la wabunge kuwa wawili Kwa kila mkoa ni gumu sana kutekelezeka (practically). Idadi ya wabunge huongezeka kulingana na idadi ya watu, mfano huwezi ukawa na mbunge mmoja anawakilisha watu milioni tano, itakuwa ngumu kuwafikia wote na kuwasilisha kero zao serikalini. Matokeo yake kuna makundi makubwa ya watu wataachwa nyuma kwenye swala la maendeleo hivyo kuongeza mzigo wa umaskini. Nashauri at least viti maalum vifutwe na badala yake kuwe na uwiano kati ya wagombea wa kike na kiume kwenye vyama vya siasa alafu yaongezwe majimbo machache kulingana na idadi ya vile viti maalum vilivyofutwa ili kuwa karibu zaidi na wananchi.

4. Kuhusu kufuta pension ni kumnyang'anya mtu haki ya jasho lake ambalo amelifanyia kazi kihalali. Nakushauri tu uhakikishe kuwe na usawa Kwa kila mstaafu kulingana na kipato chake. Punguza gap kati ya viongozi na watumishi wa kawaida.

5. Afya bure itahitaji maandalizi na mipango madhubuti, sio swala la kisiasa ambalo utaamua tu kutoa tamko kisha litekelezwe. Unaweza kuliwekea mipango na maandaliz ndani ya miaka mitano ya kwanza alafu utekelezaji ukaanza muhula wa pili. Afya bure Kwa watu huenda sambamba na ukuaji wa Pato la ndani, hivyo ili uweze kufanikiwa ni lazma uanze kuimarisha sekta nyingine kwanza kama vile uwekezaji, viwanda na kuboresha mazingira ya biashara yawe rafiki Kwa wananchi. Ndani ya miaka mitano kama hayo yakifanikiwa basi itakuwa rahisi kuboresha sekta za afya kwani hata mapato ya TRA yataongezeka.

6. La mwisho nakushauri ufute vyeo vya DC lakini DED na RC wabaki. Hawa ndo watendaji wa Moja Kwa Moja wa serikali kuwatoa hawa unaweza kutengeneza mianya ya upigaji na kurudisha nyuma taifa. Asante.
 
Back
Top Bottom