Jokate: UWT imekagua utekelezaji wa ilani katika mikoa 17, wilaya 185 na kata 883 Tanzania Bara

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
UWT CHINI YA MWENYEKITI MAMA MARY CHATANDA IMEKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI KATIKA MIKOA 17, WILAYA 185 NA KATA 883 TANZANIA BARA - KATIBU MKUU JOKATE

Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu chini ya Mwenyekiti wetu Mama Mary Chatanda (MCC) wamefanya ziara za kukagua utekelezaji wa ilani ndani ya mikoa17 hadi sasa na kufika katika jumla ya Wilaya 185 Pamoja na Kata 883 Tanzania bara"

"Kupitia ziara hizo zimeendelea kutuonesha kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Ndugu. Samia Suluhu Hassan"

"Tumebaini Miradi mingi imeelekezwa katika kutatua changamoto za wananchi, katika sekta ya Afya tumeweza kupunguza idadi ya vifo vya akina mama na watoto"

"Tafsiri yake ni kuwa serikali imezidi kuongeza miundombinu ya afya hasw katika kuboresha na kununua vifaa tiba vya kisasa na kutoa hamasa kwa akina mama kujifungua katika vituo vya afya."

"Tumekagua miradi ya maji sehemu mbalimbali pamoja na elimu ambapo tumeshuhudia ujenzi wa shule za wasichana zenye hadhi ya juu na uwepo wa mabweni pamoja na shule za mchanganyiko kupitia miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Boost"

"UWT imeweza kuishauri serikali katika sehemu zote tulizoona mapungufu kuwajibika kwa haraka katika kutatua changamoto ya aina yoyote ile"

Ndugu. Jokate Mwegelo
Katibu Mkuu wa UWT - Taifa

📍Lumumba - DSM
🗓️ 7 Machi, 2024
 

Attachments

  • IMG-20240307-WA1366.jpg
    IMG-20240307-WA1366.jpg
    42.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom