SoC02 Ni wakati muafaka sasa wa Jamii kuelewa ukweli kuhusu Ndoa

Stories of Change - 2022 Competition

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Wakuu,

Kuna msemo ambao sikumbuki niliwahi kuusikia au kusoma wapi lakini unasema "it is now or never"
Yaani kama sio sasa basi ni milele.

Ikiwa na maana wakati wa kuchukua hatua ni sasa na tusipochukua hatua basi ni milele!! Pamoja na kwamba naandika makala hii katika mashindano lakini natamani Kila mtu, Kila nyumba, Kila kanisa, Kila msikiti basi usome hii makala.

Kwasasa suala la ndoa sio tu limekuwa gumu Bali limeleta mtafaruku katika jamii, suala la ndoa limefanya watu wavunje urafiki na undugu wao! Suala hili limefanya akili na mioyo ya vijana wengi kuhama na kubadilika kabisa.

Kwa sasa vijana wanaposikia Ndoa akili zao huwapeleka kuwaza suti Kali na mavazi ya gharama, huwaza ukumbi wa kifahari na aina ya vyakula ghali pamoja na gari la kifahari siku ya harusi! Kwa wazazi wakisikia mtoto wao anataka kufunga ndoa basi ni rasmi wameingia katika kipindi Cha kukosa usingizi! Tayari huwaza namna ya kuingia kwa ndugu na jamaa, namna ya kushawishi wadau kuingia kwenye kamati.

Pande zote mbili za wazazi tayari huanza Pilika Pilika ambazo hupelekea kuingia kwenye madeni makubwa! Nadhani kwa Sisi tunaosoma Uzi huu tutakubali namna ambavyo tumedai au kudaiwa michango ya harusi!! Sina haja ya kueleza zaidi kuhusu suala hili lakini Sasa nirudi kwenye mada yangu!


NDOA NI NINI?

ndoa ni makubaliano ya watu wawili ( kwa hapa kwetu wa jinsia tofauti) kukubaliana kuishi pamoja kama mke na mume,

Na Kisha wazazi wa pande zote mbili kukubaliana na watoto hao ikiwemo suala la mahari! Kule kanisani au msikitini ni kuitangaza ndoa kwa watu! Na kwakuwa watu Wana serikali Yao ndipo sasa mchungaji au shekhe ATASAJILI NDOA KWA NIABA YA SERIKALI!

Narudia Tena mchungaji au Shekhe anasajili ndoa , hafungishi ndoa! Ndio maana pale kwenye Cheti wanatambulika kama wasajili! Sasa nataka kusemaje? Jamii ikielewa suala hili kuwa ndoa ni Yale makubaliano tu na kule kanisani au msikitini ni suala la kuirasimisha tu basi tutapunguza Ile Presha na ulimbukeni ambao Hauna maana! Ndio maana wenzetu wengine wanaweza kufunga ndoa wakiwa watu 6 tu kanisani.

Ni wajibu wetu sote kuwajulisha watoto wetu kuwa ndoa sio mavazi ya kifahari, ukumbi na vyakula ghali! Bali Yale makubaliano ambayo wanaingia! Na kizazi kikielewa suala hili basi hakuna Tena mambo ya kununiana au kuingia katika madeni ambayo hayana ulazima.


SASA JE SHEREHE ZISIFANYIKE?

Jibu ni sherehe zifanyike kwa uwezo wa muoaji , na sherehe isiwe kipaumbele Cha kwanza! Na isiwe lazima! Hakuna haja ya kuingia madeni!! Kama unaweza sherehe fanya! Kama huwezi sherehe acha! Suala ni makubaliano!


SASA NINI KIFANYIKE?

1. Katika ngazi ya familia wazazi wanao wajibu wa kuongea na watoto wao kuhusu umuhimu wa ndoa, na faida na hasara za harusi! Kipaumbele kiwe ndoa na isiwe harusi! Mfano wazazi wanaweza kuwaleleza watoto wao kwanini wasitumie gharama kubwa kuandaa sherehe kuliko kipato Chao ili kuepusha madeni baada ya sherehe! Inahuzunisha sana Kwa jinsi jamii inavyochukulia suala la ndoa! Utakuja vijana wanaishi kabisa kama mke na mume lakini ukiwaambia habari za kufunga ndoa (kuirasimisha) wanakuwa wakali wakisema hawawezi kumudu gharama za sherehe! Vile vile kwa wazazi hujikuta wakiwa katika msongo wa mawazo kisa harusi!!

2. Kanisani elimu itolewe! Unaweza kusema afadhali kidogo waislamu katika suala la ndoa huwa hawana mambo mengi lakini hata wao siku hizi mambo ya sherehe za ukumbini zimeanza kuenea kwa kasi! Elimu ya Ndoa ikianzia huko makanisani ambako ndiko kamati zinaanzia basi inaweza kuokoa hiki kizazi! Kwasasa watu wanawaza zaidi "kufunikana" kuanzia suti mpaka aina ya mapambo ya kuweka kanisani! Hakika suala hili Sio dogo kama tunavyodhani!

3. Jamii iweke uelewa katika suala la ndoa zaidi kuliko sherehe za harusi! Watu wasinuniane kisa michango ya harusi! Jamii ichukulie michango ya harusi kama hiari na sio nichangie ili nikuchangie! Na usiponichangia sitakuchangia! Na ole wako nikuchangie usinichangie! Hivi ninavyoandika Uzi huu Kuna urafiki umevunjika kabisa na chanzo kikubwa ni michango ya harusi!

4. Kwa VIJANA (wanaotaka kufunga ndoa) lazima waelewe kuwa hakuna uhusiano wowote wa sherehe kubwa na maisha mazuri kwenye ndoa! Na kuwa Kuna maisha mengine marefu baada ya sherehe kubwa! Na vile vile suala la kupata zawadi n.k halina ulazima wowote!

Nimeona sehemu nyingine mojawapo ya sababu inayowafanya vijana kutaka kufanya sherehe kubwa ni kuwaza zawadi na "vitu" vingine ambavyo hudhani ni muhimu katika kuanza maisha! Nataka niwaambie kwa jamii yetu ya Sasa wengi wanachanga pesa ili waje kula mapochopocho kwenye sherehe! Wale wanaoweza kuchanga na wakaja na zawadi pia wanaweza kukuletea zawadi hata bila sherehe!! Hivyo vijana lazima waelewe suala hili na kuepusha mlundikano wa mambo ambayo hayana ulazima baada ya Ndoa!


MWISHO
Ni wajibu wetu sisi sote kubadilika na kuanza kuishi kwa kukubaliana na wakati tulio nao! Kwanini tulaumiane kisa Michango? Kwanini undugu na urafiki uharibiwe kisa Michango ya harusi?

Kwanini vijana washindwe kufunga ndoa eti kwakuwa. Hakuna sherehe!!?

Tukubali kubadilika na Hakuna ulazima wowote wa kufanya sherehe Bali mipango ifanyike ya vijana kufunga ndoa na kuishi kwa amani!
 
Nime kupigia kura !!!

Chapisho zuri naona kwenye bandiko lako linalo zungumzia matatizo ya ndoa, umeweka dhana Kama vile "sherehe, nyumba na magari".

Mimi naomba niongelee "ndoa za jinsia moja"

Hili ni tatizo kubwa Sana katika ndoa ambalo jamii na serikali inaitajika lisilifumbie macho, Jamii inatakiwa ihakikishe vijana waliopo ndani yake wana kwenda na njia iliyo sahihi.

Kwamba vijana wapate elimu juu ya tatizo la ndoa ya jinsia moja na serikali ihakikishe swala hili nyumba kwa nyumba na vijana washirikishwe kutokomeza ushoga na ndoa za jinsia moja kwa ajiri ya kuwakuza vijana kimwili, kiakili na kiroho.

Tukitokomeza ndoa za jinsia moja tutakuwa tunajenga taifa bora na imara kwa ajiri ya vizazi vyetu vijavyo.
 
Sawa, hongera.

Ndoa nyingi kwa sasa ni kama fashion tu.

Taasisi imekuwa ngumu, ila vijana acha waoane.

Michango ndo challenge.
 
Nimepanga kuoa bila harusi lakini ikitokea nikafanya sherehe italingana na uwezo wangu kwakua pia sipendi kuchangiwa.
 
Ndo ya jinsia moja hii nahis Inategemeana na Tamaduni za jamiii fulani, kwa mfano tamaduni zetu sisi watanzania ni kitu cha Ajabu sana kwa tamaduni zingine duniani ni kawaida. Ni muhimu kuzidumisha Tamaduni zetu hizi ndoa haziwezi kuwepo .
 
Back
Top Bottom