Ukweli usiopingika: 50/50 Imekuja kuua ndoa za kidini

Youngblood

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
18,967
55,069
Ndoa nyingi za siku hizi zinavunjika kwasababu zinaendeshwa kidini katika ulimwengu wa kisasa.

Ndoa za kileo zinafaidisha wanawake zaidi kuliko wanaume, ukweli mchungu zaidi ni kwamba sheria nyingi zilizopo katika nchi nyingi duniani zinambeba mwanamke kuliko mwanaume kwenye migogoro ya ndoa na familia.

Mpaka sasa sijaona hoja za msingi za wanaowapiga spana kataa ndoa,eleezeeni vijana faida za kuingia kwenye ndoa ambazo waliopo nje ya ndoa hawazipati ili washawishike!

Asilimia kubwa ya wanaokataa ndoa wana wasiwasi na imani za kikoloni ( kikristo na kiislam) kwa hiyo kuwaeleza umuhimu wa ndoa kwa maandiko haisaidii chochote sababu wenyewe wana wasiwasi na yanayosemwa katika hizo imani.

Mengi yasemwayo kuhusu ndoa katika imani hizo ni kinyume kabisa na uhalisia wa maisha ya sasa.

Ndoa za kisasa hazijakaa kidini zimekaa kisiasa na usasa, huwezi kuendesha ndoa za kisasa kwa kututumia imani za dini,ni uongo,

KATAA NDOA wana hoja ya msingi kwa upande wao,50/50, utandawazi,na feminist wamekuja kuuwa ndoa za kidini rasmi.
 
Ndio Maana Ndoa Ya Sasa Ikitoboa 2 Years Anniversary Inabidi Tuandae Tunzo.
Utakuta ndoa ni ya kiislamu au kikiristo,lakini wanandoa wenyewe wanaishi kisasa ndani ya ndoa hiyo.
Ndoa za kidini zina sheria zake na miiko yake,lakini utakuta wenye ndoa hasa wanawake hawataki kufuata hiyo miiko.

Hiyo ndoa haiwezi kutoboa mwaka.
 
Ndoa nyingi zinavunjika kwasababu zinaendeshwa kidini katika ulimwengu wa kisasa.

Wanaohusianisha KATAA NDOA na ushoga na usagaji,ni wapuuzi...
Ndoa za kidini, kimila, kiserikali na hata kipagani zote ni mawazo na mipango iliyosetiwa na Binadamu wala hakuna guarantee au warranty ya kusababisha ndoa iwe nzuri kwa 100%, muhimu sana ni maelewano bora kimahusiano.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is work.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ndoa nyingi zinavunjika kwasababu zinaendeshwa kidini katika ulimwengu wa kisasa.

Wanaohusianisha KATAA NDOA na ushoga na usagaji,ni wapuuzi

Ishu ni ndoa za kisasa,na hawa kataa ndoa wana hoja ya msingi kwa upande wao.

Ndoa za kileo zinafaidisha wanawake zaidi kuliko wanaume huo ni ukweli mchungu.

Mpaka sasa sijaona hoja za msingi za wanaowapiga spana kataa ndoa,eleezeeni vijana faida za kuingia kwenye ndoa ambazo waliopo nje ya ndoa hawazipati ili washawishike!

Kitu kingine asilimia kubwa ya wanaokataa ndoa wana wasiwasi na imani za kikoloni ( kikristo na kiislam) kwa hiyo kuwaeleza umuhimu wa ndoa kwa maandiko haisaidii chochote sababu wengi wana wasiwasi na na yanayosemwa katika hizo imani.

Ndoa za kisasa hazijakaa kidini zimekaa kisiasa na usasa, huwezi kuendesha ndoa za kisasa kwa kututumia imani za dini,ni uongo,

50/50, utandawazi,na feminist wamekuja kuuwa ndoa za kidini rasmi.

Sio ndoa za kidini

SEMA NDOA ZA KIKRISTO

Dini ya kiislamu haina ndoa za 50 / 50
 
UKINZANI WA NDOA UKO KWENYE SHERIA:
SHERIA YA ASILI, SHERIA YA MAUMBILE MWANAUME NI KICHWA, KIONGOZI (NDIO MSINGI WA NDOA KUDUMU)
SHERIA ZA NDOA/SERIKALI, SHERIA ZA ULIMWENGU MKE NI KICHWA, KIONGOZI.(NDIO SBB YA ANGUKO LA NDOA)


 
Back
Top Bottom