Pamoja na wote wanasiasa wanajaribu kufuata trend ya wananchi. Kwasasa tred ipo kwenye kudai haki, kupinga sheria mbovu, kupinga utekaji, undugu, u bara na u zanzibari, kupinga rushwa na kutaka haki kwa kila mtu bila kujali chama. Sasa kwa misingi hiyo hata ndani ya CCM kuna wengi hawapendi mwelekeo na wamegoma kabisa kutetea hoja. Sasa imebaki serikali inategemea dola tu kuzuia hoja za watanzania badala ya kuzijibu, kuzuia vyama vya watanzania kama Chadema kwasababu wana hoja nzito, sasa hayo yote badala ya kusaidia yanazidi kumfanya Mama asipendwe na Watanzania. Kila kitu ni fake